Kero za january

NewDawnTz

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
1,667
362
:heh:

Wandugu ukweli kabisa hakuna mwezi siupendi kama wa January.

Hii January ni kero jamani (japo sijui kama na kwa wengine pia ni kero).

Mimi bado kid wangu mdogo ndo kwanza anagonga shule ya awali sa hizi hivyo sina pressure sana za kumsomesha.

Ila ngoma iko kwa majirani na ndugu. Requests za kukopesha ada watoto waende shule ziko kibao mpaka zinanikera. Sijui ndo wakiona kale ka mkweche kanakonipeleka ofisini wanajua nina ka-SACCOS ndani au vipi?

Wengine Dec walijitanua mpaka wakachanika msamba kudondokea kwenye mitaro, ila leo wanaomba 50 au 70 kupeleka watoto shule.

Hivi ni mimi tu au na wengine yanawakuta? Hebu niambieni mnafanyaje??

Me choka mpaka nawaza nibadili ratiba ya likizo iwe Janurai alafu natimikia mbali nisigongane nao nje ya geti home kwangu
 
Ni kweli mwezi wa kwanza huwa na changamoto nyingi hasa ukizingatia kuwa mwezi wa kumi na mbili kuna sikukuu mbili ambazo hakuna mzazi au mlezi anayeweza kuepuka kuzigharamia,ndio maana unaona watu wengi ikifika mwezu huu wa kwanza wanatafuta sehemu ya kupata msaada.
Si kama ni kujitakia ila inategemea na namna mtu anavyoishi,jaribu kuwavumilia kwani shida haina mwenyewe na kama huwezi kuwasaidia basi uwe mkweli na watakuelewa kuliko kufikiria kukaa mbali nao,kumbuka kuwa wewe ni jirani hivyo ipo siku utahitaji msaada toka kwao hata kama usiwe wa kifedha kama wao watakavyo sasa.
 
Kwa issue ya ada kama kweli una uwezo wape tafu ila michango ya harusi na kitchen party wapige chini!
 
:heh:

Wandugu ukweli kabisa hakuna mwezi siupendi kama wa January.

Hii January ni kero jamani (japo sijui kama na kwa wengine pia ni kero).

Mimi bado kid wangu mdogo ndo kwanza anagonga shule ya awali sa hizi hivyo sina pressure sana za kumsomesha.

Ila ngoma iko kwa majirani na ndugu. Requests za kukopesha ada watoto waende shule ziko kibao mpaka zinanikera. Sijui ndo wakiona kale ka mkweche kanakonipeleka ofisini wanajua nina ka-SACCOS ndani au vipi?

Wengine Dec walijitanua mpaka wakachanika msamba kudondokea kwenye mitaro, ila leo wanaomba 50 au 70 kupeleka watoto shule.

Hivi ni mimi tu au na wengine yanawakuta? Hebu niambieni mnafanyaje??

Me choka mpaka nawaza nibadili ratiba ya likizo iwe Janurai alafu natimikia mbali nisigongane nao nje ya geti home kwangu

unaishi uswahilini halaf unaogopa mikopo? acha kutuyeyusha bana!
 
kwa kweli ni ngumu na ina mambo mengi ila hatuna budi kuvumilia na kukabiliana na changamoto zinazojitokeza,pole sana mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom