Kero za barabarani baada ya Kangi Lugola kutumbuliwa

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,783
35,760
Uzoefu wa kusafiri barabarani kabla, baada na wakati Kangi Lugola akiwa waziri wa mambo ya ndani unahusika.

Kangi Lugora alipoteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani, alileta mageuzi makubwa chanya katika idara ya polisi na hasa kwenye kitengo cha usalama barabarani.

Bambika bambika ya makosa yasiyokuwa na kichwa wala miguu vilipungua sana. Wenye vyombo vyama moto pamoja na madereva wakageuka kuwa wadau badala ya kuwa watuhumiwa wa uhalifu sugu na wahanga wakubwa wa rushwa tokea kwa maofisa polisi hawa wa usalama barabarani.

Kwenye haya ikumbukwe mabilioni ya shilingi ya faini ambayo kabla polisi usalama barabarani walikuwa wakijitanabaisha nayo kila leo kama mafanikio ya utendaji wao.

Matokeo ya haya yalikuwa kuchukiwa mno kwa polisi na hata serikali ya awamu ya tano.

Alipoingia mh. Kangi Lugora mambo yalibadilika ghafla. Uonevu na dhuluma za polisi zikashughulikiwa. Matangazo ya pesa za makusanyo yakakoma. Matochi ya kupiga kwa nyuma yakasitishwa. Matumizi ya simu binafsi za mkononi na picha za matochi zikastishwa. Ikawa ni lazima picha ya tochi iwe kwenye tochi si kwenye simu. Ubovu wa gari ukawa ni kosa moja, si tairi, taa, wiper, nk kama makosa tofauti.

Wananchi wakashangilia polisi wakachukia na wakamchukia mno mh. Kangi Lugora.

Hakuna shaka kuwa ni kwa nini wengine leo tunapo sikitika na kuondoka kwa Kangi Lugora polisi hawa wanashangilia na kufanya sherehe nzito maana dua zao zimemfika mwewe.

Hivi sasa hali ni mbaya labda kuliko kabla ya Kangi Lugora. Matochi ya kubambika yamerejea kwa kasi mno. Haya ni yote ya kupigwa mbele na nyuma na picha kutumwa hata umbali wa zaidi km 100 . Makosa ya kunyumbulisha ubovu wa gari yamerejea tena. Rushwa inadaiwa kama deni. Yaani ni vurugu mechi kweli kweli. Tutakimbilia wapi siye?

Inaonekana hawa ndugu wako busy kufidia walichokosa wakati wa Kangi.

Yote haya ni ajabu na kweli. Ina maana labda yote mema aliyofanya Kangi Lugola aliondoshwa nayo?

Shida kweli kweli.

Waziri Simbachawene kazi unayo. Hawa jamaa si wema yawezekana hata mh. Kangi Lugola alitengenezewa zengwe tu kutokana na chuki binafsi.
 
Waziri Simbachawene
Kumekucha Sasa Hivi Kwenye Utendaji
Yaani Picture Ya Torch Inatumwa Kwa Simu Binafsi Umbali Wa Kilometres 100.

Nakukumbusha Waziri Yale Mazuri Ya Mtangulizi Wako Yachukue Uyaendeleze. Epuka Mihemko, Fanya Kazi Kwa Weredi.


Ondoa Kero Haraka Kumbuka Tanzania Ni Kubwa Sana
 
Hili nililisema mapema sana! Hata Mh rais alisema vizara inayomyima usingizi Ni hii ya MAMBO YA NDANI
MAONI.
Nashauri kitengo hiki cha usarama Barabarani kiondolewe police kianzishwe kitengo special km walivyo wa mizani
Kiukweli hili la rushwa linahitaji mbinu mbadara zaidi ya hapo hata tukilalamika tunapoteza mda
 
Hili nililisema mapema sana! Hata Mh rais alisema vizara inayomyima usingizi Ni hii ya MAMBO YA NDANI
MAONI.
Nashauri kitengo hiki cha usarama Barabarani kiondolewe police kianzishwe kitengo special km walivyo wa mizani
Kiukweli hili la rushwa linahitaji mbinu mbadara zaidi ya hapo hata tukilalamika tunapoteza mda
Hao kitengo special wao hawahitaji hela!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Suala inatakiwa madereva wasitembee na cash, kwenye milango iandikwe hakuna pesa iliyobebwa kwasababu yote hayo wanafanya ili kujitengenezea mianya ya kupata rushwa au ni mpango wa serikali kukusanya kodi au pesa ya uchaguzi..

Haiwezekani serikali kwa rasilimali zote walizo nazo washindwe kuondoa rushwa.

NB. Kuto kubeba cash ikiwa ni sheria, matumizi ya technology yasiachwe nyuma, vile vile wananchi tusiogope kupelekwa kwenye mamlaka husika kuliko hawa wahuni wanaobambikia kesi ovyo...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
brazaj, Je angeachwa aendelee na uaziri kisa kawadhibiti traffic polisi?

Ukiwa mzuri kwa upande mmoja na upande mwingine ukawa mbovu wewe unahesabiwa kuwa una dhambi. Hivyo kangi kuwadhibiti traffic kama uanvyodai wewe huku akihujumu uchumi wa nchi bado ni mkosaji kama wakosani wengine.

Lakini pia usihukimu kuwa askari polisi pekee ndiyo wamefurahia kutumbuliwa kwa Lugola. Nina imani ya dhati ww kwa njia moja au nyingine ulikuwa na manufaa na uaziri wa Lugola

Mimi siyo polisi lakini binafsi nilishukuru kufukuzwa uaziri mh huyo. Kilichokuwa kinanichukiza kwa mh huyo ni tabia ya kuwadharau aliyokuwa akiwaongoza na kuwaona kama vinyago fulani na akasahau hao watu wamesomea kazi yao lakini yeye hakuwa amesomea uaziri. Lakini pia akasahau mkuu wa polisi, magereza, fire na uhamiaji anaweza kuwa waziri lakini yeye hawezi kuajiliwa katika nyadhifa zao.

Kwa ujumla Lugola alikuwa na dharau ya kupindukia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
goggles,

Umesema wewe si polisi hili nalo hukuliona kwenye hilo bandiko:

'Yote haya ni ajabu na kweli. Ina maana labda yote mema aliyofanya Kangi Lugora aliondoshwa nayo?'
 
Umesema wewe si polisi hili nalo hukuliona kwenye hilo bandiko:

'Yote haya ni ajabu na kweli. Ina maana labda yote mema aliyofanya Kangi Lugora aliondoshwa nayo?'
Ndiyo maana nikasema wema wako hausafishi ubaya wako. Tenda mema 1000 lakini baya 1 tu linafuta mema yako yooote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom