Kero yangu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kero yangu.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kashaija, Sep 4, 2009.

 1. K

  Kashaija JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Natanguliza salaam kwa wana jukwaa wote.

  Kama kuna kitu kinanikera sana basi ni foleni isiyo ya lazima inayosababishwa na askari wa usalama barabarani katika makutano ya barabara ya Morogoro na Mandela.

  Askari hawa, wana upendeleo wa kuita magari ya upande mmoja (Morogoro - Dar na Dar Morogoro) huku wakiacha foleni ya kukatisha tamaa kwa magari ya ya upande mwingine (Bugrn - Mwenge na Mwenge - Bgrn).

  Hivi sababu ni nini? Maana anaweza kuita magari ya upande mmoja kama nilivyoeleza hapo juu kwa muda wa dak. hata 20, baada ya hapo anaita kama magari kumi tu kwa upande wa Bgrn - Mwenge, matokeo yake foleni ya Mandela inakuwa ndefu mpaka External. Je wahusika wakuu hawalioni hili? au tuamini maneno ya mtaani kwamba Askari wanaokaa kwenye makutano hayo wanapewa kitu kidogo na madreva wa mabasi ya kwenda na kurudi mikoani ili wawapitishe haraka?

  Mtakumbuka Askari mmoja alishawahi kupigwa pale na Mwanajeshi kwa sababu ya ujinga huu.
   
 2. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #2
  Sep 4, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Labda sababu njia ya Moro - Dar ni njia moja kubwa sana kwa magari yanayoingia na kutoka Dar ukilinganisha na njia ya Buguruni- mwenge ni njia ndogo ya magari yanayozunguka hapa town tu.

  Ni muhimu kwa Serikali kuweka fly over pale ili kuondoa huo utata.

  Subiri fly over 2020.

  Pole sana
   
 3. M

  Myamba Senior Member

  #3
  Sep 4, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni kweli pale Ubungo pana tatizo hilo. Isipokuwa nadhani wanafanya vile kwa kuwa njia ya Moro-Dar or Dar-Moro ni kubwa. Kama watabalance magari ya pande zote, basi magari yanayoingia mjini yatakuwa na foleni ya kusikitisha.

  Nadhani kinachoweza kufanyika ni kutengeneza vizuri barabara zisizopitia Ubungo (kama ya Mbezi Mwisho - Mbezi Beach nk), lakini in long run waangalie uwezekano wa kuwa na fly-overs kwenye junction zote muhimu (kama Ubungo, Mwenge, tazara, nk).
   
Loading...