KERO ya Walokole: JE, watengwe na makazi ya watu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KERO ya Walokole: JE, watengwe na makazi ya watu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Konzogwe, Jun 21, 2009.

 1. K

  Konzogwe JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 441
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Ninakaa jirani na makanisa ya kilokole,basi usiku kucha wanapiga kelele tena wakitumia vipaza sauti! Jamani! Usingizi hamna! Kama ningekuwa na sauti serikalini ningependekeza makanisa haya yajengwe mbali na makazi ya watu kama machinjio tu la sivyo wasali kwa sauti za ustaarabu bila maspika.Wanatukera sana!
   
 2. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ni wewe uliye jenga karibu na kanisa au kanisa limejengwa karibu na nyumba yako.

  Ushauri wa bure hama ukanunue sehemu nyingine.
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Sio makanisa tu hata ukiwa karibu na msikiti, alfajili pia ni hivyohivyo
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kaazi kwelikweli..hivi sheria za nchi zinasemaje? Maana nimesikia wenzetu Kenya soon wataanza kutumia sheria za kudhibiti kelele kwa umbali usiopungua mita 30..hapa kwetu sheria zikoje?
   
 5. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Thinkpad,

  Ushauri wako mzuri, ila ungelimpa ushauri MZURI SANAANA ingelikuwa mswano zaidi. Si umwambie tu "AJIUWE" ili aachane na haya matatizo ya dunia? Hapo utakuwa umetoa ushauri wa maana sana sana mkuu.

  Hili la makelele kwa kweli hata mie hunitibua. Inatakiwa ipitishwe sheria hata kama na Wakuu wa Mikoa iwepo saa ya kuwapa watu kulala. Hamna mdundiko wala mkwaju. Hamna kanisa wala msikiti.
  Kuna baadhi ya nchi nasikia wana kitu kwa mfano kuanzia saa 4 au saa 5 usiku, inabidi eneo lote liwe kimya na hii inaenda hadi saa 12 asubuhi. Ila si kuwa wao hawana sherehe. Ukitaka kufanya sherehe basi waweza waomba majirani zako na mkaimaliza kienyeji, au kama ni sherehe kubwa sana, na iko nje, kama tuseme sherehe za kiserikali, basi matangazo yanawekwa kwenye nyumba za watu kuwataarifu kuwa kutakuwa na usumbufu.

  Kwa Tanzania, na kupenda raha kwetu ukijumlisha na tabia yetu ya kudandia treni za umeme kwa mbele, hii imekuwa kero kubwa sana. Mwisho wa KERO za namna hii ilikuwa pale Magomeni. Upande mmoja Waislam na msikiti wao na juu MASPIKA makubwaa, na huku nako Walutheri na maspika yao juu ya kanisa makubwaa. Wakaelekezeana haya maspika, na ukiwauliza sasa mnamhubiria nani? Wao wanajibu "Mtu wa barabarani". Sasa kama waishi hapo karibu...........

  YEs, makelele kutoka kanisani, misikitini, nk nyakati za usiku ni kero kubwa sana. Time to STOP this Tabia. Wao wajifunze kuishi na sisi na si sisi tujifunze kuishi nao, WALA VYA BURE HAWA!!!
   
  Last edited: Jun 21, 2009
 6. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Abdu,

  Tatizo siyo umbali na mita, tatizo na hicho kipimo kinachoitwa decibel (dB). Hiki ndiyo kilitakiwa kiwe kinatumika. Kama wakifahamu ni safi ila kama hukifahamu, basi hiki ni kama chombo cha kupimia speed ya gari ila sema chenyewe kinapima UKUBWA?? wa sauti. Ukizidisha speed basi itaonekana na unalipa faini au kupewa adhabu. Ingelitakiwa ijulikane, kwa mchana na dB ngapi na usiku ni dB ngapi. Ukizidisha, basi adhabu unaipata, labda uwe umetoa taarifa mapema na watu kuombwa msamaha kuwa kutakuwa na fujo wakati wa usiku hadi saa..... maana mtoto wangu anachezwa....
   
 7. T

  Tujisenti JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2009
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa kweli makanisa ya walokole yanakera sana hasa kwenye mikesha.Vile vile ile SWALAAAAAAAAAAAAA ya waisilam asubuhi ni kero
   
 8. K

  Konzogwe JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 441
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  NIJIUWE!!! da,nahisi umetoroka MILEMBE HOSPITALI.
   
 9. O

  Omugasi Member

  #9
  Jun 21, 2009
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ukishangaa ya musa utastaajabu ya firauni, jamani kuna eneo fulani pale nafikiri panaitwa darajani' kama unatoka kamata na kuelekea keko-chang'ombe, au kama unaenda barabara ya ghala la madawa, hapa kwa chini yake kumejengwa msikiti na kanisa hapohapo tena la walokole, sasa bifu linaanza kwenye kuhakikisha kila mtu anatumia maspika kwa hari kasi na nguvu mpya.Mabwana wale kilichobaki ni kushikana mashati tuu, sijui serikali za mitaa hazina wenyewe?
   
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  Jun 21, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hiyo lugha yako ungeirekebisha, sio makelele bali watu wanamwabudu Mungu katika Roho na Kweli. Tunatakiwa tuvumiliane kwa sababu hizo unazoitwa 'kelele' mitaani kwetu. Mabaa, vipaza sauti vya misikiti saa kumi usiku vile vile mchana, kule Kipawa-kelele za ndege, sitaji mabomu ya Magala kuyavumilia hayo atayataja Lukuvi ni nyingi mno! Laiti watu wa mipango miji na Idara ya Ardhi wangefanya kazi zao sawasawa haya yote yasingetokea. Utahamisha kanisa leo unashangaa mtu mwingine anapewa eneo hilo hilo anajenga baa! This happens ONLY IN TANZANIA!
   
 11. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #11
  Jun 21, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  ushindwe na ulegee!!!!
   
 12. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #12
  Jun 21, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ndugu KONZOGWE, ukicheza wewe ndo utahama si walokole.
  Mbona wanachofanya ni maombi si kelele?
   
 13. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #13
  Jun 21, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Afadhali umemweleza ukweli.
  Wanafanya hivyo kulingana na Maandiko Matakatifu ya Mungu aliye hai:
  Psalms:150:3: Praise him with the sound of the trumpet: praise him with the psaltery and harp.
  Psalms:150:4: Praise him with the timbrel and dance: praise him with stringed instruments and organs.
  Psalms:150:5: Praise him upon the loud cymbals: praise him upon the high sounding cymbals.
  Psalms:150:6: Let every thing that hath breath praise the LORD. Praise ye the LORD.
  Maneno mengine kama ni msamiati chukua English Dictionary. Ubarikiwe!
   
 14. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #14
  Jun 21, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tuko pamoja sana mkuu.
   
 15. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #15
  Jun 21, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  wewe unayeongea hivyo kuwa walokole wanakukera, hujui kitu, Mungu na akusamehe kabisa, tena tema mate chini. hujui kama pengine wanakuwa wanakuombea wewe na nchi yako ukae salama ndo maana unakuwa na hata muda wa kulala? wanaomba kwaajili yao, kwaajili ya watz wote, kuomba Mungu atuepushe na vita na majanga mbalimbali. hao ni watu muhimu sana kuliko vile unavyofikiri. Mungu yupo pamoja nao.

  Pili, umeleta mada hii, angalia sana. ukisababisha chochote kutokea kwa hao walokole, Mungu wao atawapigania, na lolote litakalotokea kwao kutokana na uchochezi wako utalilipia garama. hakika utaadhibiwa. najua ninachoongea.

  Unatakiwa umjue Mungu, tena kwa nguvu kwasababu hauelewi kwa hali ya kawaida. usisubiri hadi uugue kansa, pressure na magonjwa ya ajabu ndo ukimbilie kwa walokole haohao wakakuombeee. achana na walokole, waache wamwabudu Mungu wao, ambaye ndo Mungu unayetakiwa kumwabudu hata wewe. angalia sana, wenzio wamewagusa walokole wakadondokea pua, usiende kichwakichwa. kama hauamini endelea vita yako dhidi ya walokole, ndo utaona kama wana Mungu au la. hujafa hujaumbika, usitukane mamba wakati hujavuka mto. usifikiri kila anayeomba na kulia hana akili. kuna siku utajajua. Mungu na akusaidie, namwomba Mungu akufumbue akili ili uokoke, pengine utaepuka adhabu. Amina.
   
 16. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #16
  Jun 21, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Pamoja sana mheshimiwa.
   
 17. K

  Koba JF-Expert Member

  #17
  Jun 21, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  ...hakuna mtu amewazuia kumwimbia mungu wenu lakini sio kupigia watu wengine makelele,tatizo lenu mnafikiri kila mtu anatakiwa kuabudu mungu wenu na nimegundua walokole wengi wamechanganyikiwa tuu!
   
 18. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #18
  Jun 21, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  na msalipo msiwe kama watu wa mataifa ambao upayuka payuka, ili kila mtu awasikie
   
 19. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #19
  Jun 21, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  He he he ..yangu macho..naona watu ingukuwa laivu haya majibizano watu wangeshashikana mashati kwa jina la Bwana..lol
   
 20. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #20
  Jun 21, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160

  Hama, hakuna aliye kulazimisha kukaa hapo. lol

  Waislam wanapo amsha NCHI NZIMA saa kumi za hasubusi, hiyo si KERO. LOL
   
Loading...