Kero ya usafiri Kimara-Mbezi too much, serikali mtuangalie!

Cicero

JF-Expert Member
Jan 20, 2016
2,924
3,072
Wasalaam wadau.
Kwa wale mnaokaa mbezi mnafahamu kero kubwa ya usafiri hususan jioni kutokea Kimara.
Natoa rai kwa serikali mtuangalie na sisi ikiwezekana mabasi ya mwendokasi yatoke Mbezi mpaka Mjini moja kwa moja au hata mradi mzima wa BRT uendelezwe ufike Mbezi kabisa.
 
Mi sidhani hata kama hiii kero wanaiona, ni tabu mno, afadhali hata yale magari ya mbezi yawe yanaanzia Ubungo terminal, kuliko hivi sasa,
 
Wasalaam wadau.
Kwa wale mnaokaa mbezi mnafahamu kero kubwa ya usafiri hususan jioni kutokea Kimara.
Natoa rai kwa serikali mtuangalie na sisi ikiwezekana mabasi ya mwendokasi yatoke Mbezi mpaka Mjini moja kwa moja au hata mradi mzima wa BRT uendelezwe ufike Mbezi kabisa.
Mbunge wenu ni nani huko? Wakilisha kilio chako kwake...ili awakilishe maombi yake kwa Serikali kuu kupitia Chama Tawala.
 
Maamuzi yalifanywa na watu wanaoendeshwa ndani ya VX.

Usitegemee mkombozi hapo.
Miradi hufanyika kwa awamu kutokana na upatikanaji wa fedha..Huwezi kupanga kufanya kitu ambacho huna hela zake.. Sasa wangepanga ufike Mbezi kwa hela zipi? Bado kuna uwezekano ikaja awamu nyingine kwa hiyo wanaweza wakaenda huko unakopendekeza au wankaenda bara bara nyingine maana mahitaji ni makubwa kuliko uwezo
 
Kwa fununu zilizopo, awamu ijayo inapita Nyerere Road na kwenda Tegeta na mbagala.
 
Na njia ya Mbagala ina wakazi wengi sana. Ambao wanalalamika foleni ya Kimara/Mbezi waende Mbagala ndo watajua adha ya foleni kule
 
Back
Top Bottom