Kero ya Umeme kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya Ubungo

yello masai

JF-Expert Member
Jan 8, 2016
3,552
3,513
Ni jambo la kusikitisha sana.

Ilikuwa siku ya Ijumaa nilikuwa na shida muhimu sana hapo wilayani Ubungo, niljpofika sikuweza kuhudumiwa kwa sababu umeme ulikatika. Nikaambiwa nirudi Juma tatu.

Leo Juma tatu nimerudi, kabla sijahudumiwa umeme ukakatika tena, tangu saa nne mpaka mda huu saa nane raia tumepiga kambi hapa kwenye ofisi za mkuu wa wilaya tukisubiri umeme urudi tuhudumiwe.

Hivi kweli TANESCO mnakata umeme hovyo na kila siku kwenye ofisi muhimu kama hii?

Hivi kweli serikali imekosa hela za kununua Generator kwa ajili ya ofisi kubwa na muhimu kama hii??

Watu tunatumia nauli kubwa na muda kwenda na kurudi kwa sababu tu ya umeme.

Inasikitisha sana.
 
Kuna kero nyingine iitwayo “ mtandao upo chini” utaisikia daily pale Manispaa ya Ubungo.

Hii inaweza kuchukua hata siku nzima. Are we serious!?
Mkongo wa Taifa huo. Muda wa kazi upo slow kinoma.

eGA sijui wanafanya nini?
 
Nchi ya ajabu sana hii! Watawala wapo juu ya viieite wanakula kiyoyozi lakini issues za muhimu hawana mda nazo.

Ila naamini ndivyo miafrika tulivyo, hata umuweke nani, akiwa straight atapigwa majungu hadi aondolewe..look what they did to JPM.
 
Kabisa. Mpaka nimekaa nikamkumbuka Jamaa. Ujinga na uzembe wa namna hii alikuwa ameupunguza sana
 
Ni jambo la kusikitisha sana.

Ilikuwa siku ya Ijumaa nilikuwa na shida muhimu sana hapo wilayani Ubungo, niljpofika sikuweza kuhudumiwa kwa sababu umeme ulikatika. Nikaambiwa nirudi Juma tatu.

Leo Juma tatu nimerudi, kabla sijahudumiwa umeme ukakatika tena, tangu saa nne mpaka mda huu saa nane raia tumepiga kambi hapa kwenye ofisi za mkuu wa wilaya tukisubiri umeme urudi tuhudumiwe.

Hivi kweli TANESCO mnakata umeme hovyo na kila siku kwenye ofisi muhimu kama hii?

Hivi kweli serikali imekosa hela za kununua Generator kwa ajili ya ofisi kubwa na muhimu kama hii??

Watu tunatumia nauli kubwa na muda kwenda na kurudi kwa sababu tu ya umeme.

Inasikitisha sana.
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANZANIA)

TAARIFA YA KUOMBA RADHI KWA BAADHI YA WATEJA WA WILAYA YA KIBAMBA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Wilaya ya Kibamba linawaomba radhi baadhi ya wateja wake kwa kukosa huduma ya umeme kutokana na hitilafu iliyojitokea kwenye laini yetu majira ya saa 11:45 Asubuhi,tarehe 09/08/2021,siku ya jumatatu.

SABABU YA HITILAFU
Mwananchi kuchoma nguzo ya umeme jirani na chuo cha St.Joseph Magari saba

MAENEO YANAYOHATHIRIA.
Magari saba,St.Joseph,Kwa Mkuu wa Wilaya,Luguruni Enet,Luguruni Mbokomu,Luguruni Brazil,Kwa Mabula na baadhi ya maeneo ya jirani

HATUA ZILIZOCHUKULIWA
Mafundi wetu wanaendelea na kazi ya kuhakikisha huduma ya umeme inarejea kwa wakati

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza

Wasiliana nasi kwa simu na.zifuatazo: Dawati la dharura Tanesco Kibamba: 0677111103/0699111103

Imetolewa na:
*OFISI YA UHUSIANO NA HUDUMA KWA WATEJA- TANESCO KIBAMBA *
09-08-2021
 
Ni jambo la kusikitisha sana.

Ilikuwa siku ya Ijumaa nilikuwa na shida muhimu sana hapo wilayani Ubungo, niljpofika sikuweza kuhudumiwa kwa sababu umeme ulikatika. Nikaambiwa nirudi Juma tatu.

Leo Juma tatu nimerudi, kabla sijahudumiwa umeme ukakatika tena, tangu saa nne mpaka mda huu saa nane raia tumepiga kambi hapa kwenye ofisi za mkuu wa wilaya tukisubiri umeme urudi tuhudumiwe.

Hivi kweli TANESCO mnakata umeme hovyo na kila siku kwenye ofisi muhimu kama hii?

Hivi kweli serikali imekosa hela za kununua Generator kwa ajili ya ofisi kubwa na muhimu kama hii??

Watu tunatumia nauli kubwa na muda kwenda na kurudi kwa sababu tu ya umeme.

Inasikitisha sana.
Eneo nguzo zilipochomwa na kusababisha kukosekana kwa huduma ya umeme
Screenshot_20210809-153526_WhatsApp.jpg
 
Eneo nguzo zilipochomwa na kusababisha kukosekana kwa huduma ya umemeView attachment 1886192
Poleni kwa changamoto hii. Lakini nguzo zilizo kwenye maeneo yenye majani namna hiyo (mapori) zinatakiwa zilimiwe maeneo yanayozizunguka ili mtu akichoma majani moto usifike kwenye nguzo.

Pia hamuoni ni wakati sasa wa kuishauri serikali kuwa na njia mbadala ya kupata umeme wakati wa dharula kama hizi?
Ni sawa kweli ofisi ya mkuu wa Wilaya tena ya jijini Dar es Salaam kukosa Generator?
 
Back
Top Bottom