Kero ya ukosefu wa maji majumbani ndani ya jiji la Mwanza wakati miundo mbinu ya mabomba ipo specific kata ya Mhandu

Baba JB

Member
Dec 7, 2021
17
18
Wanabodi,

Hii nchi ina kero za ajabu ajabu sana ambazo kwa watu waliostaarabika ni mambo ya aibu lakini kwetu sisi linaonekana kama ni jambo la kawaida sana.

Serikali imetumia kodi za wananchi wake kuweka huduma kwa watu ili kuhakikisha maisha yanakuwa bora na wananchi hao wanapolea kwa mikono miwili kabisa na kuunga mkono juhudi hizo kwa kuchangia gharama kuweka mabomba ndani ya makazi yao lakini jambo la ajabu mambomba hayo yanageuka kuwa mapambo yasiyokuwa na maana yoyote ile maana watu tunakaa hadi wiki ya tatu sasa maji hayatoki bombani hakuna taarifa yoyote kutoka mamlaka husika wala nini unabaki unashangaa.

Wonderful enough ni kuwa hakuna hata kiongozi anayeliangalia hili sio mwenyekiti wa mtaa wala diwani au mbunge wote wanaona ni sawa tu. Shida ya kuchaguliwa viongozi iko hapa.

Watendaji wa serikali yetu hivi haya mnayafanya kwa manufaa ya nani? Niliwahi kuuliza huko nyuma nikaambiwa kuwa hilo huwa ni dili la watu wa mamlaka na wafanyabiashara ya kuchotesha maji. Wananchi wanapokosa maji majumbani wanalazimika kununua kwa wafanyabiashara mfano kwa sasa tunanunua maji dumu moja kati ya Tsh. 500 hadi Tsh. 1000 inategemea na umbali.

Hivi ndugu zangu hii ni haki kweli? Watanzania tuteseke na mangapi? Kero kwenye kila kitu iwe ni barabara, umeme, huduma za afya, elimu, maji yaani kila kitu ni kero tu hebu tupumzisheni basi na hivi vingine ambavyo havina ulazima wa kutufanyia hivi. Wenye mamlaka oneni aibu basi mlishughulikie hili nasi walau tuone thamani ya kodi zetu mnazotukamua kila kukicha huku zikizidi kuongezeka kama vile mko kwenye mashindano ya kuongeza kodi.
 
Hapo Mwanza mjini kuna sehemu zina shida ya maji haswa, na hujaingia ndani ndani vijijini huko pamoja na kuwepo Ziwa Victoria.

Jiji hilo na lina kero hivi.
 
Niliskia kuna pump imeharibika huko mabatini,walisema last week ingetengamaa ila bado mambo sio mambo ila kiufupi miundo mbinu ya maji mwanza ni ya hovyo sana hii idara haiko makini hata kidogo nimeshuhudia mipira ikivuja zaidi ya miezi kadhaaa tena barabarani ila haishughulikiwi ,kukatika maji au kutopatikana maji katika jiji hili ni uzembe wa hali ya juu maana ziwa halina kiangazi wala masika.......
 
Ungeenda Ofisini ungepewa majibu sahihi muone technical Manager wa hapo
 
Mkuu hata Buswelu huku tena ndio usiseme maji huwa yanatoka mara moja Kwa wiki J4 Tu . Na ki wiki 3 sasa no water . Kwa kweli hii nchi ni ya ovyo Sana basi Tu
 
Ziwa lipo jirani lakini kuna shida ya maji..poa tu hakuna namna bebeni tu ndoo kichwani

Ova
 
Niliskia kuna pump imeharibika huko mabatini,walisema last week ingetengamaa ila bado mambo sio mambo ila kiufupi miundo mbinu ya maji mwanza ni ya hovyo sana hii idara haiko makini hata kidogo nimeshuhudia mipira ikivuja zaidi ya miezi kadhaaa tena barabarani ila haishughulikiwi ,kukatika maji au kutopatikana maji katika jiji hili ni uzembe wa hali ya juu maana ziwa halina kiangazi wala masika.......
Shida ni kuwa mamlaka inapewa target ya kukusanya mapato tu na sio kujikita kutoa huduma kwa wananchi. Laiti kama wangekuwa wanaangaliwa jinsi wanavyotoa huduma basi mamlaka nyingi zingekuwa tayari zimevunjwa maana wanachofanya ni upuuzi tupu
 
Niliskia kuna pump imeharibika huko mabatini,walisema last week ingetengamaa ila bado mambo sio mambo ila kiufupi miundo mbinu ya maji mwanza ni ya hovyo sana hii idara haiko makini hata kidogo nimeshuhudia mipira ikivuja zaidi ya miezi kadhaaa tena barabarani ila haishughulikiwi ,kukatika maji au kutopatikana maji katika jiji hili ni uzembe wa hali ya juu maana ziwa halina kiangazi wala masika.......
Hiyo pump inachukua muda gani kutengenezwa? Huu ni uzembe wa hali ya juu kama ni kweli hiyo ndiyo sababu basi kuna watu hawastahili kuendelea kuhudumu kwenye nafasi zao ndani ya hiyo mamlaka
 
Back
Top Bottom