Kero ya miziki inayopigwa nje nyakati za usiku !!!

Maarifa

JF-Expert Member
Nov 23, 2006
4,568
2,911
Mimi ninaishi pembezoni mwa JIJI la DSM. Kuna KERO inayosnisumbua na hata siju nianzie wapi ama nimalizie wapi.
Hivi kuna sheria yoyote itakayoweza kutulinda wakazi against Makelele ya MIZIKI hasa kuanzia siku za IJumaa na Jumamosi? Kuna hizi sehemu ambazo hutumiwa na watu kunywa na kula. Zina majina lukuki! Mara kadhaa sasa ikifikia Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi Huwa kuna Kelele za kutisha!! KUBWA MNO. Kwani kuna bands hupiga live! NJE katika sehemu hizo ambazo zimezungukwa na makazi ya watu. Kuanzia saa 2 usiku mpaka saa 6 au mpaka 8 usiku wa manane kuna mfululizo wa miziki yenye makelele. Hivyo kwa wale walioko nyumbani karibu na maeneo hayo, huwezi kulala ama kusoma kitabu au hata kungalia any program katika luninga.
Sasa je JIJI na serikali za mitaa au watu wa mazingira wansemaje?
Ni kwa nini isiwekwe sheria ya entertainment ianayohusiana na makelele yote iwe ndani ya majengo na sio nje?? Je kwa sisi tunaokerwa tufanyeje?
 
ndugu,hayo ndio matunda ya kuishi kwenye SOCIETY ISIYO JUA WALA KUFUATA AU KUZINGATIA SHERIA(SERIKALI NA WANANCHI WAKE)
sheria zote zipo,wapi kumbi za starehe zijengwe,wapi kuwe na gereji,wapi watoto wacheze lakini wameamua/tumeamua kufumba macho na kuvunja sheria...aliyejenga ambae ni raia kama wewe na aliempa kibali cha ujenzi(mtendaji serikalini) wote wanajua nini wanafanya.
Kuna muda maalum wa kufunga bar zilizo kwenye makazi na kiwango cha sauti ya muziki unaoruhusiwa kupigwa maeneo hayo lakini HAKUNA ANAYEJALI WALA KUZINGATIA HIZO SHERIA, na matokeo ndio hayo kila baada ya nyumba bar
hapa kijijini ninapoishi watu wanazingatia sheria,ukipiga muziki wako hovyo wanakijiji wanaita polisi wanamalizana na wewe,kila mtu anajua saa ngapi azime muziki wake,saa ngapi bar zifungwe aidha ni weekend au week days
jaribu kuwaona mamlaka husika labda,i mean BIG LABDA wanaweza kuwasaidia muishi kwa amani
 
Tatizo ni kutupiana lawama na majukumu.
Ukienda Polisi wanasema kazi ya mtendaji wa mtaa. Mtendaji wa mtaa anasema nenda kwa mkurugenzi wa manispaa maana hao ndio wanato avibali, Mkurugenzi wa Manispaa anasema Hiyo ni watu wa Biashara na Leseni. Ukienda huko wanakuambia nenda kwa watu wa mazingira nao wanakuambia nenda kalalamike poilisi ama nenda mahakamani kama unaushahidi!! NGOMA!!! Hivi humu JF si kuna wanasheria ndiyo maana naomba ushauri ao maana hao watanieleza kitu cha uhakika. Then I will take action. Hata kama ni kurekodi sauti za kelele hizo na muda ili uwe ushahidi Swali nina haki gani kisheria kurekodi bila kuambiwa nimekiuka sheria?
KISA
Zamani sana wakati nakaa nimepanga Mwananyamala Kuna jirani yangu alikuwa na Radio yake akawa anafungua sauti ya juu nyumba nzima hatusilizani, ukimwambia apunguze ndiyo anaongeza halafu anafunga chumba. One day mpangaji mwenzetu alienda akakodisha High powered sterio na Maspika makubwa. Akaja akatyuni halafu akakaa kimya. Yule wa makelele alipowasha tu tukamwendea akatubeza kama kawaida yake. Basi huyu jamaa na Strerio zake za kukodisha Akawasha na sauti yake kama ulikuwa hujala tumbo lilikuwa linatetemeka! Then yule wa siku zote akakerwa sana akazima. Tangu siku hiyo ikakoma. Je hii yahawa jamaa ni wengi we need Big brother support!
 
hili ni tatizo kubwa sana hasa maeneo ya kimara, ubungo riverside, mabibo na maeneo mengine, sheria zipo lakini watkelezaji ndio wahusika wenyewe wenye kumbi hizo za starehe, tabu tupu bra Maarifa, ila kuna solution kutoka kwa waathirika wewe subiri tu utaanza kuisikia
 
Mimi ninaishi kimara temboni sasa waweza kujua ninaongea nini!
 
Mimi ninaishi kimara temboni sasa waweza kujua ninaongea nini!
inawezekana tunaishi maeneo jirani bra ni tatizo kubwa sana lkn kama nilivyosema waathirika tunakuja na solution, wewe subiri tu, tumechoka na kuchoka sio kukata tamaa ni kupambana kutatua tatizo hata kwa faida ya watoto wetu, watoto hawasomi wala wagonjwa hawapumziki kwa amani ni midundo mpaka asubuhi
 
SInza mitaa ya Vatican, Nyuma Lion Hotel Pembeni kushoto kuna T-Garden Bar ikifika ijumaa pale Vatican ama wanakuwepo sometimes AKUDO au Akina Nyoshi ama Twaarab, jamani hapalaliki au na nyumba za jirani utakuta kuna Harusi ya Kiswazi watu wanakesha na mchiriku aaah jamani nchii hii hakuna utawala wa kisheria
 
bra chimunguru, na utaambiwa hapo kuna serikali ya mtaa inayoweza kutunga sheria ndogndogo na kuzisimamia pasipo uoga ila kutokana na uzandiki na ujinga uliokolea watu wanapiga makelele mpaka asubuhi, inabidi sisi waathirika wenyewe ndio tutoke na wazo la kumaliza tatizo
 
Ukifuatilia sana Wenzetu wazungu hupenda kuishi mazingira gani utakuta ni mbaali sana na mijini hata karibu na vijipori nafikiri hili tatizo lilishawapata zamani sana ndiyo maana hata wakienda nje ya nchi zao basi huchukua tahadhari where should my accomodation be..... hii ni tofauti na wahindi na waafrika ambao makazi yao mengi ni karibu na vimiji au mijini kabisa ambako kuna makelele na masumbufu ya kila aina! Jamani tununue viwanja misugusugu ....
 
Lukuvi nakumbuka mwaka jana alizungumzia sana suala hili, alizungumzia utungwaji sheria ndogo ndogo kwa ajili ya monitor haja mabar yaliyojaa kila kona ya mji.....hili limeishia wapi? au zilikuwa nguvu za soda?
 
Nafikiri kwa Wagombea Uongozi wa Mwaka huu hilo liwe mojawapo ya changamoto tutakzowapa wakati wa kampeni. Ukianzia Madiwani na Wabunge Ingawa nina mashaka sana kuwa tutapewa ahadi zilezile tulizozoea za kasi mbadala, nguvu za soda, na mapovu mengi!!
 
afadhali wewe bado unategemea miracles toka kwa serikali itakayochaguliwa!!!! Ngoja tusubiri tuone!!!

ukweli ni kwamba sheria zipo tatizo ni enforcement!!!!!
 
Ukifuatilia sana Wenzetu wazungu hupenda kuishi mazingira gani utakuta ni mbaali sana na mijini hata karibu na vijipori nafikiri hili tatizo lilishawapata zamani sana ndiyo maana hata wakienda nje ya nchi zao basi huchukua tahadhari where should my accomodation be..... hii ni tofauti na wahindi na waafrika ambao makazi yao mengi ni karibu na vimiji au mijini kabisa ambako kuna makelele na masumbufu ya kila aina! Jamani tununue viwanja misugusugu ....
Nauli ya kwendea kazini bra Kimbweka ndo maana tunajibanza uku otherwise kwanini nisiende kujichimbia Kunduchi bana nile na upepo asubuhi nawahi misele yangu ndani ya mkoko wangu
 
#13
post_new.gif
Today, 12:12 PM
Sipo
user_online.gif

Sipo in the picure with his friend

mkuu sipo nifafanulie hicho ki-blurei....!

HALAFU THEN AVATA YAKO NIMEIKUBALI SANA!..inanikumbusha 1989
 
inawezekana tunaishi maeneo jirani bra ni tatizo kubwa sana lkn kama nilivyosema waathirika tunakuja na solution, wewe subiri tu, tumechoka na kuchoka sio kukata tamaa ni kupambana kutatua tatizo hata kwa faida ya watoto wetu, watoto hawasomi wala wagonjwa hawapumziki kwa amani ni midundo mpaka asubuhi

inawezekana nyie majirani kweli ..tafuteni namna ya kukaa mjadili tatizo hili
 
Ndiyo maana nimeleta hapa ili tupeane mawazo kwanza halafu ndiyo tuform some sort of pressure group. Maana mtu mmoja huwezi Unless ni KOVA mdogo!!! Kwani hapa wapo wengi mkituchangia your opinion then hata tukiamua kukutana kupanga mikakati tunakuwa na hadidu za rejea.
 
Back
Top Bottom