Kero ya Meseji za matangazo ya mitandao ya simu

Singidan

JF-Expert Member
Aug 24, 2015
876
923
Habari wakuu!

Leo Asubuhi nimeamka nakutana na meseji ya tangazo la vifurushi, Mara kidogo Kama saa mbili hivi napata nyingine, yaaan kwa siku napokea meseji zaidi ya 5 kwa mtandao mmoja, ukienda voda na mitandao mingine Ni hivyo hivyo...

Aisee, hii inakera Sana, yaan kea siku unapokea zaidi ya Meseji 15 ktk mitandao yote na hazina maana yoyote...

Hi kero nimeulizia hata rafiki na Jamaa zangu was karibu nao wanapata usumbufu wa namna hiyo.

Mtu unakaa umetulia Mara unasikia twiitwiiii. Unaangalia meseji inasemaje Mara oooh Songesha...... Sasa Nani mwenye shida ya kusongesha kiasi fulani.

Aisee tunaomba mjirekebishe.....huduma zenu tunazipenda ila matangazo ya usumbufu yamekuwa mengi.... Maaana mmeona namba zenu mkipiga tunakata Sasa mnafowadi tu.
 
Ebhana me ndo wananikera hatari inbox yangu imejaa mesej zao tu.nasemaga nifanyaje nisizipate hizo mesej
 
Back
Top Bottom