Kero ya matuta ya barabarani yasababisha madereva kupita kwenye barabara ya vumbi

MGOME

Member
Dec 4, 2011
33
5
Hii nimeishuhudia jana wakati nasafiri kuja Mwanza kwa basi nikitokea Dar ambapo barabara kati ya Shinyanga na Ilula kuna tuta kila baada ya mita 200 kiasi sasa imewalazimu madereva wote Wa mabasi kurejea barabara ya zamani ya kupitia Old Shinyanga ambayo ni ya vumbi ili kuepuka kero hii.

Jamani je ni halali kweli highway kuwa na matuta mengi kiasi hicho kiasi cha kusababisha kero? Je hali ipo na nchi za wenzetu au ni bongo tu? Maendeleo tutayafikiaje kwa kutumia muda mwingi barabarani? Na uharibifu wa magari inakuwaje?

My take: Mamlaka husika naomba zichukue hatua za kuondoa haya matuta na kuweka alama za barabarani na kuweka
 
kujenga matuta imekua kama fashion. Nini shinyanga, njoo dar kipande cha kuanzia ubungo hadi kibamba uone matuta yake!!!!
 
Ujinga wa madereva, maana ukiweka road signs, road marking and road signals hawazifuati. Wao ni kuchapa mwendo tu. Na hata hayo matuta bado hayawatoshi. Sijui tufanyeje?
 
Hii ni Tatizo la Ten percent!! Issue hii ya Matuta ipo kwa Tanroad Manager wa Mkoa!! Ni rahisi kutuma vikampuni vyake vya Mfukoni Kuweka Matuta ili kujipatia Riziki!! Katika hali ya Kitaalamu Matuta yanakuwa na standard Drawings ambayo Ofice Kubwa kama Tanroads wanatakiwa wawe nayo!! Lakini naona Hakuna!! Kila mtu anajenga Tuta kutokana na Hisia!! Magufuli Amka Utuokoe!! Ni jana tu nimesikia Mtu kapata ajali arusha na Kufa kutokana na ukubwa wa Tuta na dereva Hakuliona!!

TANROAD TUOKOENI JAMANI MSIWE KAMA KILA KITU MLIDESA HATA UPEO WA KUFIKIRI MMEISHIWA!!!
 
Ujinga wa madereva, maana ukiweka road signs, road marking and road signals hawazifuati. Wao ni kuchapa mwendo tu. Na hata hayo matuta bado hayawatoshi. Sijui tufanyeje?
Ni ujinga wao ila Ujue ni ajali nyingi Tu zinasababisha vifo kutokana na haya Matuta!! Siku Moja utakuwa mmojawapo ndio Utajua Ubaya na umuhimu wa Matuta!! In principal Matuta Mengi Yamewekwa Unprofessionally!! Kama Enzi ya Ujima
 
kuna matuta mengine kama ya viazi, ukiwa na saloon au ki-vits, tumia ujanja woooote lakini lazima ikwangue chini.

Inabdi kuwe na sheria ya kuwashtaki tanroad kwa uharibifu wa magari ya watu
 
Ujinga wa madereva, maana ukiweka road signs, road marking and road signals hawazifuati. Wao ni kuchapa mwendo tu. Na hata hayo matuta bado hayawatoshi. Sijui tufanyeje?

jaman sasa ivi tuna mkongo wa taifa, kwanini serikali isifunge speed camera na kukusanya mapato for every speeding car?
 
Ni ujinga wao ila Ujue ni ajali nyingi Tu zinasababisha vifo kutokana na haya Matuta!! Siku Moja utakuwa mmojawapo ndio Utajua Ubaya na umuhimu wa Matuta!! In principal Matuta Mengi Yamewekwa Unprofessionally!! Kama Enzi ya Ujima

Kwenye red umemaliza kabisa na isitoshe wengine ni wapumbavu kabisa hebu kumbuka ajali ya "air shengena" . Utaamini umemaliza kabisa. Hapo kwenye bluu jitazame vizuri kwenye u-great thinker wako.
  • Ajali ya new force hivi karibuni maeneo ya nyororo- Iringa ni mwendo kasi umeondoa roho za wapendwa wetu na kuacha wengi vilema.
  • Ajali ya Shabibu bus miaka hiyo karibu na milima ya Lukumbulu mpaka mwa Ruvuma na Iringa aliacha wachache vilema huku wengi wakipoteza maisha katika mashindano ya mwendo kasi kati ya bus hilo na lilikuwa zainabu.
  • Gari la Mizigo la Dandoo mbuga ya mikumi lilipoparamia kundi la nyati na kuleta hasara kubwa pale mbugani kutokana na mwendo kasi wa dereva mjinga.
  • Ajali ilitokea 1996 pale eneo la sabasaba iringa mjini basi la abiria lililokuwa linaelekea kihesa kwa mwendo kasi huku dereva akishangilia ushindi wa timu ya Yanga 6-1 dhiti ya timu ya Morocco. Katika mbwembwe hizo aliigonga town hiace na kuua abiria wote kwenye hiace pamoja na dereva. Nakumbuka alipona conductor wa hiace. Just imagine! Uamuzi wa serikali ni kuweka matuta eneo hilo ili kupunguza ajali(siyo Kuondoa kabisa) maana madereva ni wajinga sana mkuu
  • Kuna bus la zuberi mlima sekenke liliacha njia na kuchochora porini baada ya kumshinda dereva kutokana na mwendo kasi, vifo na majeruhi kama kawaida.
  • Singida pale kuna bus moja(Sikumbuki vema jina) mwaka 2007 lilipinduka konani likiwa katika mwendo kasi na baadae kuungua moto. Vifo na majeruhi.
  • Umesahau "Air Msae" miaka ya 90+?
Idadi ya ajali za kipumbavu namna hii ni nyingi na ndo chanzo cha serikali kudhani pengine matuta yatasaidia kupunguza ajali hizo. Lakini hata wangewekewa matuta kama ghorofa ni kazi buuure. Fikiri kwa mfano:-
  • Nahodha wa MV Bukoba ungemwekea tuta sehemu gani kuokoa maisha ya wapendwa wetu.
  • Nahodha wa Mv Spice Islander mtafutie tuta standard basi au hata pengine
  • Dereva wa hiace iliyopata ajali karibu kabisa na stand kuu ya mabasi pale Mbeya.
Mkuu idadi ni ndefu na haina mfanowe. Ujinga+Upumbavu huo ndo ukweli kwa madereva wetu.
 
jaman sasa ivi tuna mkongo wa taifa, kwanini serikali isifunge speed camera na kukusanya mapato for every speeding car?

Serikali itakuwa ya kijinga sana uruhusu, yaani uruhusu mwendo kasi ili kuongeza kipato? Tazama serikali inapata laki3 for every speeding car (kwa mafano) na hapohapo hiyo car ikapata ajali kutokana na mwendo kasi na kuua abiria wote kwenye bus!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom