Kero ya makanisa ya Kilokole/ Pentekoste

Hulali ndugu??

Nadhani sheria za ufunguzi wa hizi nyumba za ibada kwa sasa inabidi ziangaliwe upya!!

Huwezi kwenda kufungua nyumba ya ibada katikati ya makazi kwa kubadilisha matumizi ya nyumba!! Namaanisha mtu alijenga nyumba kwa ajili ya makazi anageuza linakuwa kanisa au msikiti!!! Au ana kinafasi kimebaki katika eneo lake basi anajenga kanisa hapo likiwa linapakan kabisa na nyumba za makazi ya watu!!

Mbona Wakatoliki hawafungui makanisa hovyohovyo? Na makanisa yao waliweka mbali na makazi. Wenzetu walijua juu ya hii kero
Kabisa mkuu kama ulikuwepo hili kanisa mwanzo lilikuwa nyumba ya mtu ya kuishi akaona auze sasa ndio wameanzisha kanisa aisee mkuu unaijua kero acha tu ibada watu wanapolalamika sio ibada tena tukashindwa kulala bora hata wangekuwa wanaweka sauti ya chini wanawasha sauti ya juu kabisa sasa sisi hapa home ndio tupo karibu sana tunaangaliana na dirisha kiukweli ni usumbufu sana
 
Nunua emp jammer yenye voltage kubwa ..kabonyeze kwenye mavyombo yao ...vitaharibika na kuingia mpaka wakome...maana yesu hakuagiza watu waleteane kero
hapana mkuu ni ngumu kufanya ivyo inatupasa tuelewawe kwa kutumia lugha tu sema hawa wenzetu wanajifanya wanamjua mungu sana kuliko watu wote duniani
 
Biblia pia nayo kuna kipande imesema

"Kesheni mkisali na mkiomba kwa maana hamjui saa wala siku ambayo mwana wa adamu atarudi"
Mkuu upo sahihi kabisa lakini hawakumaanisha watu wakeshe kwa mikerere ya mispika kukera watu usiku wa manane mbona romani, kkkt, sabato, moraviani ibada zao za kistaarabu sana
 
Mbona madrasa za Dar es salaam huku Temeke kila Ijumaa wanakesha huku sauti za spika zikiwa juu kabisa sijaona ukianzisha uzi?
Mbona bar zinafunguliwa kila leo na kelele nyingi hulalamiki?
 
Muandike barua, pitisha wana mtaa wasaini, muungane, nakala kwa serikali ya mtaa, kata na mkuu wa kituo.

Tuliwakomesha mtaani kwetu, siku hizi 'wanang'ang'ana na Bwana' kwa staha..

Everyday is Saturday................................ :cool:
Mkuu napokea ushauri wako naufanyia kazi kwakweli sio kwa mikerere hii
 
Kuna kkanisa kpo mtaan kwetu,wameshakishtakia sana mpaka polis lakin hawaachi,sema mim npo mbal kdogo ila ningekuwa karibu nao nisingekosa dawa ya kuwakomesha
Mkuu aya makanisa ni kero sana kwakweli sio wastarabu hata kidogo sio sawa kabisa usiku kucha mikerere mchana mikerere tunapumzika sangapi
 
Kabisa mkuu kama ulikuwepo hili kanisa mwanzo lilikuwa nyumba ya mtu ya kuishi akaona auze sasa ndio wameanzisha kanisa aisee mkuu unaijua kero acha tu ibada watu wanapolalamika sio ibada tena tukashindwa kulala bora hata wangekuwa wanaweka sauti ya chini wanawasha sauti ya juu kabisa sasa sisi hapa home ndio tupo karibu sana tunaangaliana na dirisha kiukweli ni usumbufu sana

Anzeni kwa kwenda serikali za mitaa, muhoji uhalali wa kuwepo hilo kanisa! Wakishindwa panda ngazi mpaka mtafikia suluhu, hiyo si sawa hata kidogo!!
 
Hem tuletee hicho kifungu

Matayo 24:42-51
Neno: Bibilia Takatifu

42 “Kwa hiyo kesheni, kwa maana hamjui ni siku gani ataka pokuja Bwana wenu.
43 “Lakini fahamuni kwamba, kama mwenye nyumba angalifahamu ni saa ngapi za usiku ambapo mwizi atakuja, angalikaa macho asiache nyumba yake ivunjwe. 44 Kwa hiyo ninyi pia lazima muwe tayari kwa maana mimi Mwana wa Adamu nitakuja saa ambayo hamnita zamii.”

Napia nakumbuka hata kitabu cha waefeso kama kilizungumzia hii statement, nikikumbuka kifungu chake ntakiweka hapa
 
Usiende popote nakushauri.
Waambie majirani mnaokereka mkanunue au mkakodi zile speaker kuubwa, halafu zielekezeni zote kanisani, wakianza makelele nanyie fungulieni muziki mpaka sauti ya mwisho uelekeo wa kanisa.

Wakizima zao nanyi mnazima, wakiwasha nanyi mnawasha. Watakuja kuomba mpunguze sauti nanyi mnawapa kero zenu.

Au fungueni bar nyumba jirani yao weka muziki pale tu wanapoanza mikelele.
Kabisa mkuu kuna kipindi tulikuwa tunafanya ivyoo tunawasha sauti na sisi ya juu wakawa wanakuja kuomba sasa kwa sasa wamekuja kwa kasi sana kiasi cha wananchi kukerwa sana na hii tabia
 
Mbona madrasa za Dar es salaam huku Temeke kila Ijumaa wanakesha huku sauti za spika zikiwa juu kabisa sijaona ukianzisha uzi?
Mbona bar zinafunguliwa kila leo na kelele nyingi hulalamiki?
Mkuu hili kanisa lipo kwenye makazi ya watu kabisa katikati hapo mwanzo ilikuwa nyumba ya mtu sasa imeizwa tukajua ataishi mtu tunashangaa wakafungua kanisa
 
Mkuu upo sahihi kabisa lakini hawakumaanisha watu wakeshe kwa mikerere ya mispika kukera watu usiku wa manane mbona romani, kkkt, sabato, moraviani ibada zao za kistaarabu sana
kwan hayo madhehebu uliyoyataja ni ya kipentekoste?
Mkuu wakat ww unalalamika makelele kumbuka hata wachawi kwny himaya zao nao wanalalamika..wanga na wachawi hawapendi kabisa kelele za maombi, chunguza mtaan kwnu lazima spidi ya kulogana itakuwa imepungua.
 
Mkuu upo sahihi kabisa lakini hawakumaanisha watu wakeshe kwa mikerere ya mispika kukera watu usiku wa manane mbona romani, kkkt, sabato, moraviani ibada zao za kistaarabu sana
Hapana we ndio hujaelewa vizuri ebu soma hapa

ZAB. 98:1-6 SUV
Mwimbieni BWANA wimbo mpya, Kwa maana ametenda mambo ya ajabu. Mkono wa kuume wake mwenyewe, Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu. BWANA ameufunua wokovu wake, Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake. Amezikumbuka rehema zake, Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. Miisho yote ya dunia imeuona Wokovu wa Mungu wetu. Mshangilieni BWANA, nchi yote, Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi. Mwimbieni BWANA zaburi kwa kinubi, Kwa kinubi na sauti ya zaburi. Kwa panda na sauti ya baragumu. Shangilieni mbele za Mfalme, BWANA.
 
Mkuu hili kanisa lipo kwenye makazi ya watu kabisa katikati hapo mwanzo ilikuwa nyumba ya mtu sasa imeizwa tukajua ataishi mtu tunashangaa wakafungua kanisa
Mkuu hili kanisa lipo kwenye makazi ya watu kabisa katikati hapo mwanzo ilikuwa nyumba ya mtu sasa imeizwa tukajua ataishi mtu tunashangaa wakafungua kanisa
Ila wangefungua Guest house usingelalamika mkuu.
 
Nawasalimu wakuu, jamani nisiwachoshe sana kumekuwepo na wingi wa aya makanisa almaarufu ya kilokole au wengine wanayaita ya kipentekoste.

Kiukweli ndugu zangu hapa nyumbani kwa nyuma kuna kanisa moja limekuwa ni kero sana ninavyowaambia hapa tangu jana hatujalala pia na majirani wanalalamika sana kumekuwa na ibada tangu jana mpka mda huu ni midundo mikubwa sana wanaweka jaman nadhani mnatambua vizuri kero hizi,.

Swali langu hivi ni sahihi kwa mda wa usiku kucha kufanya ibada kwa kuweka sauti ya juu sana natambua humu kuna wataalamu wa taasisi husika embu toleeni ufafanuzi yani hapa wadau kila nikitaka kulala siwezi wamefungulia spika sauti ya juu sana, dah yani sijui niwaambieje hili munielewe.
Kama hapo unapoishi umepanga sio kwako hama
 
kwan hayo madhehebu uliyoyataja ni ya kipentekoste?
Mkuu wakat ww unalalamika makelele kumbuka hata wachawi kwny himaya zao nao wanalalamika..wanga na wachawi hawapendi kabisa kelele za maombi, chunguza mtaan kwnu lazima spidi ya kulogana itakuwa imepungua.
Mimi sijakataa maombi napenda sana pia na mimi mwenyewe mkristu mzuri pia nacholalamika usiku wa manane unawezaje kuwasha mziki kwa sauti ya juu sana kwani ukiwasha sauti ya chini mungu hatosikia maombi
 
Hapana we ndio hujaelewa vizuri ebu soma hapa

ZAB. 98:1-6 SUV
Mwimbieni BWANA wimbo mpya, Kwa maana ametenda mambo ya ajabu. Mkono wa kuume wake mwenyewe, Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu. BWANA ameufunua wokovu wake, Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake. Amezikumbuka rehema zake, Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. Miisho yote ya dunia imeuona Wokovu wa Mungu wetu. Mshangilieni BWANA, nchi yote, Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi. Mwimbieni BWANA zaburi kwa kinubi, Kwa kinubi na sauti ya zaburi. Kwa panda na sauti ya baragumu. Shangilieni mbele za Mfalme, BWANA.
Hahahaaha..ndaga fijo nkamu
Tena imesisitiza kwa baragumu..
 
Back
Top Bottom