Kero ya kusubirishwa kupisha msafara ya viongozi barabara za mikoani haivumiliki hakika viongozi mnatuumiza sana kwa hili

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Hakika huu ni UNYAPARA mambo leo!

Barabara za mikoani kila kuchwao zinapitiwa na kila aina ya binadamu;
  • Wenye afya na wagonjwa wote wanategemea barabara hiyo hiyo.
  • Wazima na maiti wote wanapitidhwa hapo
  • wenye haraka na wasiyo na haraka
  • Wenye bidhaa za kuoza na zisizo oza
  • Wenye pesa ya kula na wasiyo na akiba ya kula..
  • Madakitari na waganga
Kungandishana barabarani kupisha msafara wa viongozi hakika inaumiza sana!
  • Viongozi kwa hili Mnaharibu sana ratiba za watu,
  • mnaharibu sana bajeti za watu
  • Mnakwamisha matukio mengi sana ya watu
  • Mnapanda mbegu ya chuki pasiposababu ya msingi
  • Punguzeni Unyampara huu!
Pendekezo!
  1. Mnaonaje viongozi mkapanda ndege halafu magari yenu mkayakuta huko?
  2. Mnaonaje mkatoa japo taarifa siku moja kabila ili watu watafte mbadala wa safari?
  3. Mnaonaje mkatumia hata elkopita ili kuepusha acha kwa binadam wenzenu
Viongozi msichokijua ni hiki
Huenda sheria na kanuni za PSU/ task force zipo vizuri, lakini utekelezaji wa trafiki huko barabarani unafanyika kwa uoga ili kurinda kibarua!

Yamkini inatakiwa dakika 10-15 za kusubilia kiongozi! LAKINI TRAFIKI HUKO BARABARANI RTO/DTO huwa wanaamua kuwagandisha watu (2~3)hrs KWA HOFU TU ya kulinda kazi wakati kiongozi hata bado hajaamka!

EBU FIKILIENI
Kuna watu wanatoka mikoa ya mbali sana anapogandishwa 3hrs ni hasara kubwa sana.
(Mnachokifanya ni sawa na Uhujumu uchumi wa wanaichi wenu wenyewe)

Viongozi tambueni huko barabarani Kuna watu wanawahisha dawa za mgonjwa ambazo yamkini zikiwahi saa moja tu mgonjwa angepona, lakini hufariki kwa sababu ya misafara yenu!

Nitoe RAI kwa Viongozi na wale PSU fuatilieni zile ODA mnazowapa Trafiki wafunge njia! Hakikisheni Zinajali mda!

Wapeni updates ya misafara yenu matrafiki huko barabarani ili wafanye kazi kwa weledi! Kuna trafiki huko barabaranj huwa hata hawajui Exactly estimate ya msafara hadi hudiliki kutumia simu zao kupiga simu kwa wenzao!

Tunaomia ni RAIA! Viongozi na PSU tunaomba hili mliangalie Upya!
 
Hili suala la viongozi kufunga barabara linaboa sana. Leo Kimara asubuhi masaa 3 na mchana huu masaa 3 tunasubiri kiongozi ambaye alikua na ziara zake huko kibaha.

Napendeleza yafuatayo

1. Serikali iwe inatoa taarifa siku moja kabla kwamba barabara itafungwa kwa muda wa masaa fulani ili wananchi wajue na watafute njia nyingine za kupita.

2. Watumie hata helkopta badala ya magari hasa kwa safari za mijini.

Baadhi ya watu leo hawaja fanya kazi kwa sababu ya kufungwa kwa barabara.
 
Na leo Kassim kapita kwenda na kurudi Morogoro road na kwenda DODOMA sijui kuna hali gani huko barabarani
 
Hii kitu inakera sana, Siku moja nilikuwa posta kipindi cha Obama , barabara ilifungwa karibu zaidi ya saa8, nikakosa paper chuo. It is absurdity, kufunga barabara kwa muda mrefu kama huo, wakati hata kiongozi mwenyewe hajaamka.

Mi nadhani isizidi nusu SAA na ifungwe tu pale musafara wake unapokaribia. Siyo MTU yuko morogoro nyie mumeshafunga barabara mzima kuanzia mbezi hadi posta.
 
Na leo Kassim kapita kwenda na kurudi Morogoro road na kwenda DODOMA sijui kuna hali gani huko barabarani
Sitasahau nilidamka mapema saa 8 usiku kutoka kigoma, nilipofika manyoni tukagandishwa 3hrs, wakati malengo ilikuwa ni kutoboa dar mapema 1290km
 
Hili suala la viongozi kufunga barabara linaboa sana. Leo Kimara asubuhi masaa 3 na mchana huu masaa 3 tunasubiri kiongozi ambaye alikua na ziara zake huko kibaha.

Napendeleza yafuatayo

1. Serikali iwe inatoa taarifa siku moja kabla kwamba barabara itafungwa kwa muda wa masaa fulani ili wananchi wajue na watafute njia nyingine za kupita.

2. Watumie hata helkopta badala ya magari hasa kwa safari za mijini.

Baadhi ya watu leo hawaja fanya kazi kwa sababu ya kufungwa kwa barabara.
Huenda Trafiki hawapewi UPDATES za misafara! Ndiyo maana huwa wanatugandisha kibubu bubu kwasababu hawapewi exactly time ili wafunge dakika 5kabla
 
Mara nyingi Msongamo husababishwa na viherehere vya Matrafiki kuwahi kufunga barabara wakati hata Kiongozi mwenyewe ndio kwanza kapelekewa Maji Bafuni...!!!
 
Huenda hawana taarifa au hawana radio call
 
Hakika huu ni UNYAPARA mambo leo!

Barabara za mikoani kila kuchwao zinapitiwa na kila aina ya binadamu;
  • Wenye afya na wagonjwa wote wanategemea barabara hiyo hiyo.
  • Wazima na maiti wote wanapitidhwa hapo
  • wenye haraka na wasiyo na haraka
  • Wenye bidhaa za kuoza na zisizo oza
  • Wenye pesa ya kula na wasiyo na akiba ya kula..
  • Madakitari na waganga
Kungandishana barabarani kupisha msafara wa viongozi hakika inaumiza sana!
  • Viongozi kwa hili Mnaharibu sana ratiba za watu,
  • mnaharibu sana bajeti za watu
  • Mnakwamisha matukio mengi sana ya watu
  • Mnapanda mbegu ya chuki pasiposababu ya msingi
  • Punguzeni Unyampara huu!
Pendekezo!
  1. Mnaonaje viongozi mkapanda ndege halafu magari yenu mkayakuta huko?
  2. Mnaonaje mkatoa japo taarifa siku moja kabila ili watu watafte mbadala wa safari?
  3. Mnaonaje mkatumia hata elkopita ili kuepusha acha kwa binadam wenzenu
Viongozi msichokijua ni hiki
Huenda sheria na kanuni za PSU/ task force zipo vizuri, lakini utekelezaji wa trafiki huko barabarani unafanyika kwa uoga ili kurinda kibarua!

Yamkini inatakiwa dakika 10-15 za kusubilia kiongozi! LAKINI TRAFIKI HUKO BARABARANI RTO/DTO huwa wanaamua kuwagandisha watu (2~3)hrs KWA HOFU TU ya kulinda kazi wakati kiongozi hata bado hajaamka!

EBU FIKILIENI
Kuna watu wanatoka mikoa ya mbali sana anapogandishwa 3hrs ni hasara kubwa sana.
(Mnachokifanya ni sawa na Uhujumu uchumi wa wanaichi wenu wenyewe)

Viongozi tambueni huko barabarani Kuna watu wanawahisha dawa za mgonjwa ambazo yamkini zikiwahi saa moja tu mgonjwa angepona, lakini hufariki kwa sababu ya misafara yenu!

Nitoe RAI kwa Viongozi na wale PSU fuatilieni zile ODA mnazowapa Trafiki wafunge njia! Hakikisheni Zinajali mda!

Wapeni updates ya misafara yenu matrafiki huko barabarani ili wafanye kazi kwa weledi! Kuna trafiki huko barabaranj huwa hata hawajui Exactly estimate ya msafara hadi hudiliki kutumia simu zao kupiga simu kwa wenzao!

Tunaomia ni RAIA! Viongozi na PSU tunaomba hili mliangalie Upya!
Kufunga barabara eti kisa msafara wa kiongozi tena waziri ni umasikini tu.
Inawezekana akapita na shughuli zikaendelea bila kusimamisha chochote.Kimachowasumbua viongozi wa Tanzania ni kupenda umaarufu tu hawana jipya.

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Viongozi was kiafrika ndo wanapenda hivo.... Jamaa wanajiona Miungu watu Sana Yani wanainjoy wakikutwa mmepigwa kamba ndefu ili yeye apite tu....

Tuko nyuma sana Afrika... Nchi zilizoelendelea hakuna uboya Kama huu.... Wananchi wanaheshimiwa bkoz walishapigania haki zako huko nyuma watu walishapigania Hadi wafalme wao huko wakipigania haki na heshima zao
 
Bongo kuwekwa 3hrs kawaida sana
 
Usafiri wa anga pia ni salama zaidi kuliko wa barabarani.
Mbona tumewaachia anga lao kwanini wanatubana barabarani?
Waoneeni huruma waliwaweka madarakani jamani
 
Back
Top Bottom