KERO: Vodacom gawio kwa hisa 2018 haliendi sawa na dividend policy, kwanini mnawaibia watanzania

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,452
3,065
Sera ya Gawio ni walau 50% ya net profit, kwa net profit ulioishia 31 Machi 2018 kila hisa ilistahili gawio la wala 38TZS, inakuwaje kampuni inatoa gawio la 17.33TZS?

Hali hii inadumaza wawekezaji wazawa na ni ulaghai kwa wananchi. Nakumbuka pia IPO ilifanyika faulo kubwa kwa kuuza hisa za IPO kwa wageni yaaani raia wasio wa TZ, Haya makosa yanaumiza wawekezaji wazawa, Je serikali na CSMA au DSE wanafutilia hali hizi?

Kama kuna maelezo sahihi kuhusu hali hiyo ni vema tufahamishwe.
 
Hisa sio lazima kugawiwa kwa wanahisa.. Bodi ina uwezo wa kuamua kugawa au kuacha kutoa gawio.... Shukuru hata hilo gawio la 17%... Wangeweza kuamua wasitoe kabisa
 
Wawe wanatoa elimu kwa wananchi kua japokua wananunua hisa,watambue kua wanaweza kugawiwa gawiwo au wasigawiwe,uone mwitikio wa wajinga watakaojitokeza kununua HISA.

Elimu iko wazi iwapo kampuni imepata faida, gawio ni kuanzia 50% kuendelea, mwaka 2017 walitoa 60%. kazi ya wakurugenzi ni kupendekeza iwapo iwe 50% au zaidi na wala sio chini ya 50%
 
Sera ya gawio inafanyakazi pale tu amnbapo kampuni imepata faida, hapo ndo suala la 50% of the net profit or above linaingia bila zengwe
 
Iwapo Serikali haitalinda wawekezaji kwa kuhakikisha kampuni zinafuta sera zilizojiwekea itakuwa shida ya serikali sasa, maana ndio inatuhamasisha kuwekeza badala ya watz kuwa watazamaji pekeee
 
Elimu iko wazi iwapo kampuni imepata faida, gawio ni kuanzia 50% kuendelea, mwaka 2017 walitoa 60%. kazi ya wakurugenzi ni kupendekeza iwapo iwe 50% au zaidi na wala sio chini ya 50%
Inabidi tukupe elimu ya hisa... Kampuni kupata faida sio kigezo cha kupewa gawio.. Kampuni inaweza kupata faida ndogo lakini thamani ya hisa ikashuka ... Hapo ndio bodi inaamua ilipe au isilipe gawio...... Ukinunua hisa wewe subiri zipande thamani uziuze .....ukisubiri gawio utaishia kupata stress kila siku..
 
Back
Top Bottom