Kero: Utaratibu wa ku re-new line matatizo tupu

i411

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
906
290
Ninawaletea experience yangu ilionitokea baada ya kupoteza SIM card yangu. Ilikuwa ya ijumaa kuu sikuiona, basi ijumaa kuu nikaamkia voda wakani jazia form niipeleke polisi service ilikuwa powakabisa. Sasa huko polisi madudu yao sijui nani alianzisha huu utaratibu na akawapa mamlaka polisi kusimamia kitu simple kama hiki isitoshe unatakiwa kulipia mia tano tuu na akazani polisi watakuwa very happy kuifanya hii kazi lol. Yaliyonipata huko mpaka leo sijapata huduma. Nilienda urafiki kituoni ijumaa nilimkuta mdada service yake ilikuwa nzuri aliniambia mhasibu hayupo mpaka jumanne ndo naweza pata hiyo risiti ya malipo form alikuwa nayo.

Akanishauri labda niende Oysterbay, ilivyofika huko nikakutana na afande mmoja akanielezea kuna utaratibu mpya online na unalipia huko. Nikamwambia nilishafanya hiyo process akaniambia basi nenda Chuma cha kwanza wataweza kukusaidia zaidi lakini akaniambia mara nyingi hawana bando la mtandao so inawezekana nisisaidiwe manake serikali kama haijaelewa majukumu yaliyowakabizi. Sasa nilivyofika humo chumba cha kwanza, nikamkuta mama mmoja Yani kwanza nimeingia namsalimiaanakukata jicho nini shida. Namwambia polisi report nimepoteza simcrd yupo na komputer ananiambia njoo jumanne leo hatuna bando.... nikamwambia hata nimuunganishe kwenye simu yangu akaniambia nisimfundishe kazi nije jumanne.

Yani hapo unaishiwa nguvu namiye hela niliyokuwa naitegemea kwa ajili ya sikukuu ilikuwa kwenye simcard hiyo. Ndo nimesubiria leo nikaenda mpaka central kwasababu kupo karibu na ofisini sasa nimefika huko itaratibu ulikuwa shakala baga nawale wamama wanaotoa hiyo huduma hawana kabisa customer service yaani wanaona watu kama watuhumiwa tuu na kuwajibu kwa madharau nilikaa pale masaa mawili mengine siwezi simulia ngojea niache..wakati anachukuwa maelezo nilipowaambia ninahisi simcard ilipotea nikiwa kwenye basi wakaniuliza wapi nikawaambia mbezi beachi wakaambiana muandikie Kawe wakagonga muhuri niende Kawe.

Sasa ikawaambia nishafika huku nusu siku nimepotezea hapa mnataka niende tena Kawe nanyie mnaweza toa Huduma. Majibu niliyopata hapo nilikuwa mdogo tuu nikaondoka. Nimefika Kawe saa kumi naambiwa wao hutoa hiyo huduma saa tatu mpaka saa saba. Jamani hii kitu inaingia akilini kweli?

Huyu aliyeona ili wazo zuri polisi wetu watukufu kujaza fomu Za shilingi miatano kweli hayajui masilai mapana ya jeshi letu la polisi.

Miye ushauri wangu haya mambo yarudi kwenye wenye mitandao yao tuhakikiwe na vitambulisho vya taifa ambaye hana aje kujieleza huko polisi
 
Mimi huwa nawaambia kuwa bahati mbaya simu imedondokea chooni ..ili kuepuka mambo ya kwenda kuripoti ..maana hayo majamaa ni masumbufu
 
Juzi nilikwenda ofisi ya CCM. mbona huko polisi ni kama bar ukilinganisha na ofisi za chama?
 
Natumaini Mh. Waziri atasoma hapa na kutoa maelekezo , pengine sisi raia kuna kitu hatujaelewa au pengine Polis wenyewe
 
Tatizo police frustration nyingi mshahara kidogo na kutii amri bila kuhoji mpaka vichwa vinayumba.

Hapo unatengenezewa mazingira ya kupenyesha muamala lakini napo unatengenezewa mazingira ya kukamatwa kama mhalifu (kutoa rushwa).

Yani loss report ni Tshs 500/- tu lakini unazungushwa mara bundle mara nenda wapi ili umfinye afande utake kumkatia ten akusaidie chap lakini hapo hapo ukamatwe kwa kesi uliyoenda kuitafuta mwenyewe (rushwa).

We komaa nao tu hata wakikuambia nenda CCP Moshi poa funga safari kachukue loss report maana hao jamaa hawakawii kukupa jalada la kesi ya mtu mwingine.
 
Pole Mkuu fanya subira utapata line yako tu lakini hao viumbe ni wasumbufu sana mm naamini kazi yao haina baraka ya Mungu bali inalaana

Mm nilipotezaga Simu yenyewe nikawaendea Cyber Crime aisee nilikula Dana Dana nenda rudi mpaka nikaona simu yangu nimeshaitoa sadaka niachane nayo
 
Ungemalizana nao kibingwa, 5k unachukua risiti yako freesh kabisa
 
Wakati nipo centra polisi jana nipo kwenye mstari na wenzangu zaidi ya kumi akaja binti wa chuo analia lia tukamwambia atuelezee shida yake.... alasema kaibiwa kwenye mwendokasi kila kitu na leo anamtiani ashazungushwa tokea asubuhi saa hiyo ilikuwa tano na robo mtiani saa sita basi tukamwambia aende moja kwa moja awaambie shida yake wamsaidie... alivyoingia akawa anajingata ngata wakamchangia kama mpira wa kona na wanaona mtu anatetemeka anashida na anamtihani bado walikuwa wanampa majibu ya chooni mpaka wanazengo tukaingilia ndo akasikilizwa kwa shingo upande akapata hiyo risiti.

Yani huu mfumo ubadilishe polisi wasubirie waalifi wao watoane huko kwa maelfu hii ya kwenda kuangalia utumbo wao kwa miatano siyo kabisa. Siasa jamani zisiingie kwenye huduma Za kijamii mambo ya kijamii yaachwe kuwa huru kwenye jamii huko polisi yabaki makosa.

Tusiwaongezee kazi zisizo za taaluma yao hawajafundwa kutoa huduma kwa wateja bali ni kupambana na wahalifu. Basi kwenye yale madawati ya lost report angalau muwaweke watoto wa chuo wa field huko kama itaratibu huu wa lost report mnauona unamaana kupitia polisi.
 
Ungemalizana nao kibingwa, 5k unachukua risiti yako freesh kabisa
Yani mwanazengo inabidi uzuge zuge sana kituo ni... Yani kaofisi ni kadogo unakuta wapo kama watatu hivi na siye wanazengo kibao tunasubiri hiyo huduma mlangoni. Alafu wenzao nao wanawaletea ishu kama hizo zinamalizwa faster tukiwa tunaona lakini wanakuwa wamekaa tuu humo ndani ukiingia unawaona wamevimba tuu wanatamani wangekuwa barabarani wanakimbiza roli Za mchanga siyo kucheza na peni
 
Wakati nipo centra polisi jana nipo kwenye mstari na wenzangu zaidi ya kumi akaja binti wa chuo analia lia tukamwambia atuelezee shida yake.... alasema kaibiwa kwenye mwendokasi kila kitu na leo anamtiani ashazungushwa tokea asubuhi saa hiyo ilikuwa tano na robo mtiani saa sita basi tukamwambia aende moja kwa moja awaambie shida yake wamsaidie... alivyoingia akawa anajingata ngata wakamchangia kama mpira wa kona na wanaona mtu anatetemeka anashida na anamtihani bado walikuwa wanampa majibu ya chooni mpaka wanazengo tukaingilia ndo akasikilizwa kwa shingo upande akapata hiyo risiti. Yani huu mfumo ubadilishe polisi wasubirie waalifi wao watoane huko kwa maelfu hii ya kwenda kuangalia utumbo wao kwa miatano siyo kabisa. Siasa jamani zisiingie kwenye huduma Za kijamii mambo ya kijamii yaachwe kuwa huru kwenye jamii huko polisi yabaki makosa. Tusiwaongezee kazi zisizo za taaluma yao hawajafundwa kutoa huduma kwa wateja bali ni kupambana na wahalifu. Basi kwenye yale madawati ya lost report angalau muwaweke watoto wa chuo wa field huko kama itaratibu huu wa lost report mnauona unamaana kupitia polisi.
Mtiani ndo kitu gani
 
Back
Top Bottom