Kero: TCRA mlisema local channel ni bure mbona zinalipiwa?

Hizi mamulaka zinakuaga fasta sana kwa mambo yanayohusu serikali lakini kusimamia sheria zinazowapa faida wananchi zipo slow sana
 
Habari Tanzania , Startimes inapenda kuwapa utaratibu wa namna ya kuweza kupata LOCAL CHANNEL BURE kwenye King’amuzi chako kama ifuatavyo :

1. FTA - Dikoda ambazo zinabakiza chaneli za nyumbani bure ( Free Local Channel )
a. DTT(Antenna) FTA =Tsh 89,000/=
b. DTH (Dish) FTA = Tsh 135,000/=

2. Subsidized TV Dikoda hizi niambazo hazibakizi chaneli za nyumbani.
a. DTT Subsidized TV Decoder ( Antenna ) = Tsh 34,000/=
b. DTH Subsidized TV Decoder ( Dish ) = Tsh 78,000/=

Endapo ulinunua Subsidized TV decoder na unahitaji kuona local channel bure - FTA Decoder , inabidi ufike dukani kwetu, ukiwa na dikoda yazamani na utaweza kupatiwa decoder ingine ya FTA, maelezo zaidi 0764700800.

Kubadili dikoda ya antenna kuwa FTA ni Tsh 55,000/=
Na kubadili dikoda ya Dish kuwa FTA ni Tsh 57,000/=

[HASHTAG]#startimesTZ[/HASHTAG]
[HASHTAG]#mfalmewaburudanizafamilia[/HASHTAG]
star times.jpg
 
wizi juu ya wizi...umeibiwa kuku unaenda kwa mganga anakwambia lete mbuzi kuku wako atapatikana....duh
 
Huu ni wizi wa wazi wazi!
Startimes wanachofanya ni biashara ya ving'amzi siyo kutekeleza Sheria!

Sheria inawataka watoa huduma wote wakiwemo star times "kuonesha channel za ndani bure"

Suala la aina za ving'amzi hata kama wamiliki walipewa bure halizuii channel za ndani kuonekana!!
 
Startimes nilishawapigia simu na kuwambia kuwa sitalipia king'amuzi chao na nitafanya kampeni ya kuhakikisha wateja wao ninaowafahamu wasilipie na wanaotaka kununua ving'amuzi wasiingie kwenye mtego wao.
Hii ilikuja baada ya kutufanyia uhuni wa kuongeza bei za ving'amuzi bila ya kutupa taarifa wateja. Unalipia bei uliyoizoea unajikuta unaletewa sms kuwa utatazama hadi tar fulani. Humalizi mwezi.
 
Jmos nilienda pale startime bamaga head office... wanasema ili upate local channels free lazima ununue card mpya....Hawa jamaa TCRA wamefel kuwadhibiti
 
Back
Top Bottom