Kero: Tabia ya Polisi ripoti na Photocopy za huduma za Kipolisi ni Kero

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,720
2,000
Habari Wakuu,

Hakuna kitu kinachozungusha au chenye kero kama Polisi Report. Yaani watakuzungusha hadi unyooke, labda utoe rushwa.

Polisi wana tabia mbaya sana, unaenda ukiwa na tatizo, wanakusikiliza halafu wanakupa kalatasi ukatoe photocopy. Mbaya zaidi hawataki copy moja, wanataka copy tano wakati tatizo lako ni copy moja tu.

Nlienda kurenew line yangu Mlimani city, wakaniambia niende kuleta Polisi report, wakashauri kituo cha karibu cha Polisi ni Urafiki. Wakanipa kalatasi nikaenda nayo Polisi Urafiki Shekilango.

Nlipofika Urafiki Polisi wakasaini ile kalatasi nliyotoka nayo Voda, wakanambia niende Usalama Magomeni nikalipie Mia tano. Nlienda Magomeni Usalama nikalipa fee yao wakanipa risiti nikaenda nayo Polisi Urafiki.

Urafiki wakasema subiri. Hadi nianze kuhudumiwa ishafika saa nane. Tukaitwa baada ya hapo nikapewa Kalatasi nikatoe copy tano, hapo hapo karibu na kituo kuna Stationery copy moja wanatoa kwa 500/=. Ukiwapa Polisi copy hizo tano, wanatumia moja nyingine wanabaki nazo. Hadi mizunguko iishe ishafika saa tisa.

Nikaenda Voda na kalatasi ya Polisi. Nlivyofika wakanambia nitaje namba za watu watano ninaowapigia mara kwa mara. Mimi huwa napigia watu watatu tu. Nlikasirika sana.... Usmbufu kila sehemu. Ila POlisi ndo walinizungusha sana... nauli ya nenda rudi.

Hii tabia ya kuagiza Copy kibanda cha jirani inakera sana. Kwanza hata ukienda pale wakiwa wamekata umeme copy zote utakazo za Polisi unapata. Inaonekana ni ofisi ya Familia ya Polisi.
Badilikeni.

NB: Ukitaka ulahisi, andaa elfu tano au elfu kumi hivi ya kusafisha viatu, Yaani hutazungushwa, kalatasi zote utapata hapo hapo tena haraka sana. Utaondoka huku unapiga mluzi.
 

rip faza_nelly

JF-Expert Member
Feb 19, 2018
3,989
2,000
Naona uliamua tu kujipotezea mda wako. Ni kwel hii ktu ni kero sana lakin Mambo mengine yaache km yalivo mana huku hutapata unachokitaka.
 

wildfish

JF-Expert Member
May 28, 2014
962
1,000
Acha kuwa na roho ya kimasikini kopy tano tu ulizowatolea polisi ndo zinakuuma hadi unakuja kulialia hapa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom