Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 10,259
- 29,659
Wakuu natumaini wote ni wazima, nawasilisha taarifa hii ambayo ninaamini kwa wakazi wengi wa Dar es salaam hasa maeneo ya Tegeta, Bunju, Mikocheni, Ubungo nakadhalika mtakuwa mmeiona, ambapo taa za kuongozea magari "Traffic Lights" katika makutano ya barabara ya mwenge zimekuwa hazifanyi kazi kuanzia mwanzo wa wiki hii yani Jumatatu ya tarehe 06/06/2016.
Hakuna taarifa yoyote kutoka vyombo husika kama kuna matengenezo yanayoendelea na kibaya zaidi kuanzia saa tatu asubuhi (9:00am) mpaka saa kumi jioni (4:00pm) "trafiki polisi" huondoka eneo hilo na kuacha kuongoza magari ambapo inakuwa ni usumbufu sana kwa sisi watumiaji wa barabara hiyo kwa maana mabavu hutumiwa zaidi na madereva ili kuweza kuvuka eneo hilo.
Ninaamini JF ni mtandao wenye nguvu unaoweza kutumika kuwafikishia wahusika taarifa hii kama kweli walikuwa hawafahamu mpaka wakati huu ambapo zimepita takribani siku tano toka tatizo hilo lijitokeze.