KERO: Matumizi mabaya ya muda wa viongozi wetu watukufu!

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,694
787
Ndugu,

Watanzania wenzangu, binafsi nawakubali sana watu wa zamani, kwa sababu kila walilolifanya wakati huo lilikuwa na maana kubwa wakati huo na hata baada ya muda mrefu. Hivyo ni jambo zuri kuendeleza yale ambayo ni mazuri, lakini kwa vyovyote vile sio kila la zamani liendelezwe.

Hata hivyo viongozi hao hawakupenda vizazi vijavyo yaani kama kizazi chetu kuwa kama dodoki tu... kwamba tusiendeleze hata yale ambayo kwa vyovyote vile ni kero kwa kila mdau.

Ninazungumzia jambo la kuwasindikiza na kuwapokea viongozi wakuu kila mara wanaposafiri kwenda nje ya nchi especially kwa kutumia njia ya anga... wakati huo safari zilikuwa chache sana na ilikuwa maana sana kusindikizana na kupokeana... lakini kwa sasa mmmmhhhh.

Hivi ina maana gani rais akisafiri kumfanya makamu wake, waziri mkuu, mkuu wa mkoa etc. kwenda aidha kumuaga au kumlaki? ina faida gani kwa wananchi? inawaongezea nini? je inaondoa umaskini kwa kiasi gani? Je hao wadau wenyewe waziri mkuu na team yake wakienda kumsubiri Rais kwa masaa 2-4 yanasaidia nini? Askari wetu wa barabarani kila mara kuwafanya badala ya kulinda usalama barabarani badala yake kupitisha misafara ina tiga gani?

Wadau binafsi hili linanikera maana binafsi sijui objective yake na faida yake kwa sasa naamba msaada kuwambiwa wajamani.

Wako Mtiifu
Kasheshe
 
Back
Top Bottom