Kero: Kukatika kwa umeme mara kwa mara Lindi

Drjacka92

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
445
522
unnamed%2B%2810%29.jpg


TANESCO Tunakuangazia Maisha, ndio kauli mbia yao shirika la umeme Tanzania, lakini kwa mkoa wa Lindi hii kauli ni kinyume kabisa.

Sijui kwa mikoa mingine lakini binafsi naweza sema mkoa wa Lindi ndio mkoa unaoongoza kwa kero yakukatika kwa umeme Tanzania.

Lindi ndio mkoa ambao haiwezekani siku kuisha bila umeme kukatika tena bila taarifa na unakatika zaidi ya Mara tatu nakuendelea tena inakuwa kama mchezo hivi, unakata Mara unarudi yani ni shida tuu. Mpaka baadhi ya wakazi mkoani humo wanasema kwamba labda kuna wanafunzi wa field wanafundishwa kwavitendo namna ya kukata nakurudisha Umeme.

Ndio mkoa ambao umeme ukikatika Mara moja kwasiku basi watu wanapongeza kwamba Leo TANESCO wamejitahidi. Kiukweli wanarudisha nyuma maendeleo, watu wanaofanya shughuli zao kwakutegemea umeme wanateseka mno.

Yani kwa miaka miwili mfululizo nimeshuhudia kila Jumamosi umeme unakutwa saa mbili asubuhi unarudishwa saa kumi na mbili jioni na ndio siku wanayoitolea taarifa, lakini mpaka sasa hawamalizi marekebisho yao. Siku nyingine Umeme unakatwa saa nane na nusu usiku zaidi ya Mara mbili, sijui usiku kama ule huwa wanarekebisha kitu gani wakati mchana walishakata zaidi ya Mara tano.

Wahusika wa mambo haya mimi nawaambia wananchi wanateseka sana, nakama kuna uzembe fulani katika Organisation yenu naamini Ipo siku mtu atakosa kazi, jirekebisheni, mnakera sana.

Nawasilisha kwa hatua zenu muhimu.
 
HAWA MAMENEJA WA TANESCO WA LINDI & MTWARA SIJUI VP .MTWARA NAKO KUNA TATIZO KAMA HILO LA LINDI .KUNA RAFIKI YANGU KULE ANALALAMIKA.
 
Back
Top Bottom