Kero: kituo cha mabasi mailimoja, kibaha

Kaudunde Kautwange

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
1,625
1,619
Habari wana jukwaa..

Kama wewe umewahi tumia hiki kituo cha mailimoja, kibaha, kungojea usafiri wa basi au daladala utakuwa shahidi kwa haya nitakayo sema.

Kila gari likiingia hapo kituoni, wakati wa kutoka lazima gari hilo lilipiwe ushuru, lakini cha ajabu hakuna maboresho yoyote ya kituo, kituo wakati wa mvua kinakuwa kero kubwa sana.

Hakuna sehemu ya abiria kukaa wakati wakiwa wanasubiri usafiri, magari hayana sehemu maalumu za kuegesha wakati wa kupakia abiria.

Magari yanaingia bila mpangiro, yaani hakifanani na vituo vingine, kituo kinafanana na uwanja wa mpira.

Jamani wahusika, lifanyieni kazi suala hili.

Nawasilisha.
 
Ni kweli kituo cha maili moja ni kero kabisa kumebana sana hapohapo taxi zimepaki hapohapo biashara ndogondogo! Yaani kero usiombe kweli mvua inyeshe
 
Hasa wakati mabasi yanatoka kwenda njia ya Moro... coaster zinakaa sehemu ya kutokea na kugombea abiria pale na kusababisha kifoleni uchwara hadi kero!
 
Back
Top Bottom