Kero katika kuhakiki TIN number TRA Kilimanjaro

kisinja

JF-Expert Member
Sep 30, 2013
241
295
Zoezi la uhakiki wa TIN Number linaendelea mkoani Kilimanjaro na baadhi ya mikoa mingine kwa sasa. Kwa kweli zoezi hilo limekuwa ni usumbufu kwa wananchi kutokana na TRA kutojipanga vizuri. Ofisi za TRA kilimanjaro idadi ya wanaoendesha zoezi ni ndogo sana jambo linalosababisha foleni kubwa sana na kusababisha kupoteza muda mwingi kusubiria huduma.

Leo nimewahi Ofisi za TRA yapata saa tatu asubuhi nikakuta foleni kubwa na kukiwa na mtu mmoja tu anayepitia na kukagua form, inaonekana pia mtandao hauko vizuri suala ambalo linachangia kuchukua muda mrefu kuhakiki TIN,
kwa utaratibu unavyokwenda mwisho wa mwezi huu ambapo zoezi ndio litakuwa linaisha bado watu wengi sana watakuwa hawajahakiki TIN.

Hivyo TRA Tafadhalini sana ongezeni rasilimali watu na vifaa ili zoezi liende vizuri na sio kugeuka kero kwa watu. Ni lazima mjue pia pamoja na raia kuja kufanya uhakiki wanaacha Biashara zao na wengine kuchelewa kazini ili kuhakiki. Dalili si njema sana kwani kuna uwezeano mkubwa kufikia mwisho wa mwezi watu watakuwa bado hawajahakiki kama inavyotakiwa.
 
kwa kweli zoezi hili zima limekuwa ni Kero kubwa mnoooooo. Kuomba kazini kila siku. TRA jipangeni vizuri zaidi!
 
Back
Top Bottom