Kero gani nitapata nikijenga karibu na mashine ya kusaga?

BrownRange

JF-Expert Member
Dec 25, 2020
927
1,190
Wakuu habari.

Nimebahatika kununua kiwanja, viwanja vyetu vya skwata, Ila niliyepakana naye anaweka mashine ya kusaga. Je niendelee na ujenzi wa nyumba ya kuishi, au ni kero gani naweza kupata nikijenga

Naomba mawazo yenu
 
Kero yake ni ndogo kuliko kujenga karibu na msikiti au kanisa la walokole.
Naishi karibu na makanisa mawili,moroviani/Efatha kazi inaanza tokea ijumaa kukesha hadi jumapili jioni, wakianza kulia sasa hiyo midundo ya maspika hakuna kulala,

Pia kuna msikiti karibu huyu shekhe akiamua kuongea kwa maiki kama kameza betri.
 
Labda Kama mashine unafanya kazi usiku.
My friend usije ukakosea kujenga karibu na lindo la Hawa dada utamu a.k.a changudoa.
Utasikia kila aina ya matusi, harufu ya bangi, kondoπ kuzagaa nje kwako, barazani kwako Kama huna fensi Ni gesti especially siku za mvua au mida ya saa nane usiku.
Ninayo moja Sinza kila mpangaji akiingia ndani ya mwezi anahama na Kodi hadai.
 
Kero yake ni ndogo kuliko kujenga karibu na msikiti au kanisa la walokole.
Hii ya kanisa la walokole noma. Nkiwah panga nyumba yani kumbe ukuta wa ule uzio wa nyumba upande wa pili kuna kanisa la walokole, kila jion wana ibada wanafungulia mziki muda mwingine hadi saa tatu usku. Jumapili kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa saba. Huo mziki sasa.
Ilifika kipnd nikazoea nikawa hata wakpga makelele si notice muda mwingine kama kuna kelele.
 
Sehemu nyingine ambayo hutakiwi kujenga Ni karibu na bar, mganga wa kienyeji, jambazi au gesti Kama zile za Mbagala za buku tano self yenye kunguni. (Mbagala mkoje lkn? Dar nzima mnaongoza kwa mabaya))
 
Utazoea tu, labda ku shake kwa umeme napo utazoea tu na kunaweza kusitokee pia.

Nilikua nimesahau kuhusu nyuki, ila uzuri nyuki wa mashine haumi 😂
 
Aaah hapo kuku wako watapata pumba bure kabisa, kikubwa tega mlango wa banda kuelekea kwenye mashine kisha zifungulie tu yani, hutanunua chakula ya mfugo kabisa na vikuku vya mboga hutakosa!
 
Back
Top Bottom