Kero: Dhuluma ya ajira kwa watu wenye ulemavu

Ajira-Walemavu TZ

New Member
Mar 9, 2018
1
0
Watu wenye ulemavu Tanzania ni kundi dogo la watu wasiozidi hata 2,000,000 kwa bars na visiwani ila ni kundi linaloongoza kutaabika mitaani ukiachana na Makundi ya Wagonjwa,Wafungwa na Wakimbizi hapa Tanzania.

Tanzania kupitia jitihada za Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete iliweka sheria maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu ijulikanayo kama "Sheria ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010".

Katika sheria hii baadhi ya mambo mazuri yaliainishwa yahusianayo na masuala ya Ajira kwa Watu wenye ulemavu hususani kwenye Ibara ya 31 na 32.

Baadhi ya hayo mambo ni kama:

1.Kila Mwajiri mwenye wafanyakazi ama Waajiriwa kuanzia 20 na kuendelea ahakikishe 3% kati ya hao wawe ni watu wenye ulemavu(kwa taasisi Binafsi na za umma)
Swali :
-Ni Taasisi ngapi za Serikali zenye jumla ya wafanyakazi 300ambao kati ya hao 9 ni watu wenye ulemavu???
-Ni taasisi ngapi za binafsi zinafanya hivo??
-Je Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kama chombo pekee kinachoratibu michakato ya Ajira serikalini kinawajibikaje kwa Waajiri wa taasisi za Umma ili kuhakikisha sheria hii inatekelezwa kikamilifu??
-Je ni kweli kwamba Sekretarieti ya Ajira katika utumishi wa umma hausiki kwa namna yoyote ile na utekelezaji wa sheria hii kama anavodai Naibu Katibu wake???
2.Kila mwajiri ahakikishe anapeleka ripoti ya utekelezaji wa sheria ya watu wenye ulemavu kuhusu waajiriwa wake ambao ni watu wenye ulemavu kwa Kamishna wa Kazi kila mwaka.

Swali :
-Ni waajiri wangapi wa taasisi Binafsi na Umma wanawasilisha ripoti hizo kwa Kamishna kila mwaka??
-Kama jibu ni ndiyo je huwa wanawasilisha ripoti sahihi kwa kkiasi gani??
-Je ripoti hizo huwa zinafanyiwa kkazi ??
-Kama jibu ni ndiyo kwann idadi kubwa ya watu wenye ulemavu wasio na Ajira inazidi kuongezeka kila kukicha??
-Je waajiri huwa huwa wanakaguliwa kuhusiana na utekelezaji wa sheria hii ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010,Sheria ya kazi ya mwaka 2004 na Mkataba wa kimataifa wa Watu wenye ulemavu wa mwaka 2010??

-Kama hawakaguliwi ;Serikali haioni kwamba ina-dump sheria hizi na kusababisha sisi watu wenye ulemavu kuwa dumped vilevile?
 
Mkuu bodaboda zinaongeza walemavu kila kukicha,so idadi ya walemavu wasio na ajira nayo itaongezeka pia,

Halafu sio kwamba kila mlemavu basi hutaka kuajiriwa,wengine wanafanya shughuli zao binafsi.
 
Hili linahitaji mjadala wa kitaifa.
 
Back
Top Bottom