Kenyela unawatetea polisi waliopiga raia waumini

mwandiga

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
1,506
661
Kamanda kenyela nilikuwa nakuheshimu lakini nilivyokusikia kwenye ITV jioni hii ukisema polisi hawakuvamia waumini wa kanisa la Efatha wala kuwapiga, kwa walioona taarifa ya habari ya juzi wakati wa tukio hilo linarushwa, wataujua ukweli, polisi waliwapiga sana waumini,walidiriki kuwapiga mateke, vichwa,makofi waumini waliowakamata licha ya kuwa walikuwa chini ya ulinzi na hawakuonyesha unprofitable wowote. Hivi polisi wetu tz wanachojua ni kupiga tu!

Au kwa kuwa watz hatuwashtaki kwa kukiuka haki za mtuhumiwa? Jana nimeona kwenye msiba wa Kanumba polisi walikuwa wanawapiga watu ili wasogee!

Hii tabia haina dawa? Kenyela kuongea uongo kwa matukio yaliyorushwa na ITV ni kuwatetea polisi kwa kujua walichofanya au ni kuonyesha kuwa kila wafanyacho polisi ni sahihi? Hivi hakuna sheria ya kuwashtaki polisi wanapompiga mtuhumiwa aliye chini ya ulinzi na hakuonyesha resistance yoyote na ushahidi wa video upo? Mm naona ni wakati muafaka wa kuanza kuwashtaki kama sheria inaruhusu.

Tuchangie hapa kwa lengo la kutatua hili tatizo kwani linazidi kushamiri siku baada ya siku na jinsi ambavyo hatua hazichukuliwi kwao wanapata kichwa wanaendelea na upigaji.
 
Back
Top Bottom