kibol
JF-Expert Member
- Apr 24, 2012
- 4,512
- 2,730
Ni kweli Viongozi wa Afrika wamekosea sana ila kwa hili nawaunga mkono,Hiki chombo cha ICC ni cha kinafiki sana mwanzoni na mimi nilikitetea kama wewe juu ya kuwakamata Viongozi wanaokiuka haki za binadamu ila baada ya kushindwa kuwakamata akina Blair na Bush kwa kuua raia wasiokuwa na hatia Nchini Iraq ndipo nilianza kukidharau na double-standard zake.
binafsi kiliposhindwa kumshtaki bush kwa uhalifu wa kivita na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliopelekea umwagikaji wa damu kwa raia wasiokuwa na hatia wa iraq na afghanistan sina imani nacho hata kidogo, mtoa mada yupo sahihi kuwa crush viongozi wetu kwa hoja zao walizozitoa, pengine kwake yeye hazina mashiko.......labda wamekosea tu ktk kutoa sababu za sisi kujitoa lakini umuhimu wa kujitenga na icc upo na ni mkubwa mno, hawa si wazazi wetu tuogope kuachana nao