Kenyatta asema hakuna fedha za kuwaongezea wafanyakazi mishahara

miss zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
2,908
2,000
NAIROBI,KENYA

RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta amesisitiza kwamba hakuna fedha za kuwalipa wauguzi wanaogoma akiwataka wafanyiakzi wote wa serikali kustahamili hali ya uchumi inayokabili taifa kwa sasa.

Alisema hayo alipokuwa akizungumza kwenye ziara yake huko Kisii. Rais alisema serikali ina mambo mengi ya kufanya na wala sio kuongezea wafanyakazi mishahara kila mwaka.

Kauli yake imuengwa mkono na kinara wa ODM Raila Odinga ikiwa ni siku tano baada ya wauguzi wanaogoma kukaidi agizo la kusitisha mgomo wao.

Wakati huo huo Rais Kenyatta aidha amewaonya wale wote wanaoedeleza ufisadi serikali akisema watakabiliwa kisheria.
 
mr.London

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
2,786
2,000
Ukishashika madara tena kila kitu ni rahisi kutamka otherwise maneno haya asingethubutu kuyatamka kwenye siku zake za campaign za kuchaguliwa kuwa rais
 
pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
10,778
2,000
Huwa unashinda online ukitafuta negative news about Ke!!!
Sometimes post positive tukuone serious.
Nadhani kwenye kila habari kuna 'positive side'. Kwenye hizi habari za rais Uhuru Kenyatta na manesi ni wazi kwamba 'labour unions' za Kenya zina ukomavu wa hali ya juu kwenye masuala ya kutetea haki za wafanyikazi. Maanake rais U.K. alianza kwa kuwatishia kwamba mgomo wao ni haramu na kwamba wote watafutwa kazi. Ila hizo 'kelele' za rais ziliambulia patupu, hawatishiki ng'o 'wamekaa ngumu'!
 
Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
2,239
2,000
Huwa unashinda online ukitafuta negative news about Ke!!!
Sometimes post positive tukuone serious.
Binafsi sion kama Negative ila tukubali ukweli kila mtu kwa nchi zetu za africa mashariki ana hali mbaya ya kiuchumi..! kinachokera watu wanalipwa kila mwezi pesa lakini wanataka wao ndiyo wanaongezewa kila mwaka! wanatamani kuishi maisha ya juu..! Sipendi hii hali ifike mahali ata walio ajiriwa nao wajue mtaani huko serikali ina mambo mengi ya kufanya si kuongeza mishahara ya watumishi tu pekee.

Bora kwenu Kenya ila ingekuwa ndiyo Rais wa Tanzania kasema haya na siasa zetu za kipuuzi watu wangeimba mpaka basi na kulianya mtaji wa kisiasa. IFIKE MUDA TUAMBIZANE UKWELI.
BIG UP KENYATA KWA KUSEMA UKWELI.
 
Amesema ukweli sio kwa kupenda kwake ila ni hali ya mifumo aliyoipata ikitumika. Nchi nyingi za Afrika hazijatambua, maanake tunafanya vitu vya ajabu sana, yaani mwanasiasa analipwa hela nyingi zaidi ya wale ambao juhudi zao ndio zinaendesha nchi kwa kiwango kikubwa. Walimu,manesi, watumishi wa umma kwenye ngazi za chini. Tulichanganyikiwa zamani.
 
REDEEMER.

JF-Expert Member
Feb 22, 2015
8,957
2,000
Deni la SGR linatafuna 68% ya revenues zote za Kenya mnategemea uhuru afanyaje? Em tulieni huko nchi imegoma kwenda.
 
mwaswast

JF-Expert Member
May 12, 2014
12,712
2,000
Nipo sahihi kusema manesi wa Kenya wanalipwa vyema kuliko madaktari wa TZ?
 
Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
5,711
2,000
Watakuja watanganyika wasifia kila kitu Cha Kenya hapa napo watasifia sana na kumpongeza UK.
 
joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
16,664
2,000
Amesema ukweli sio kwa kupenda kwake ila ni hali ya mifumo aliyoipata ikitumika. Nchi nyingi za Afrika hazijatambua, maanake tunafanya vitu vya ajabu sana, yaani mwanasiasa analipwa hela nyingi zaidi ya wale ambao juhudi zao ndio zinaendesha nchi kwa kiwango kikubwa. Walimu,manesi, watumishi wa umma kwenye ngazi za chini. Tulichanganyikiwa zamani.
Wakenya lazima mkubali kujifunza vitu vingi sana toka Tanzania. Tanzania tulipitisha Sera ya kuwepo na ulinganifu wa vipato vya mishahara, yaani kusiwe na tofauti kubwa ya mishahara ya watu serikalini, ila kama kawaida yenu ya kujifanya ninyi mnajua kila kitu, mlipinga na kutubeza, sasa matokeo yake ndio kama hii migomo isiyokwisha, haiwezikani mbunge analipwa 15 times ya mwalimu au Nurses, wakigoma mnasema serikali ina mambo mengi ya kufanya, wapunguzieni hao wabunge kama mtaona migomo ya Mara kwa Mara, kila mmoja atajua kweli serikali haina pesa za kutosha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
22,756
2,000
'Siwezi kuongeza Mshahara kwa kiwango hicho mnachokitaka, Na Kama nyongeza hiyo ya Mshahara ndio sharti pekee la kunipa kura Basi sitaki kura zenu...'-Jakaya Mrisho Kikwete 2010

Watu wakazusha Kuwa Jakaya kakataa kura Za Wafanyakazi Kumbe ule ulikuwa Ukweli Mchungu

Leo Hii wanakumbuka Hata ile Nyongeza ya wakati wa Jk waliyoita Ni kiduchu maana Mzee Baba Chuma Cha Pua Hata ile Annual Increament ya Kila July iliyokuwa Haina Mjadala kaipeleka Kwenye Standard Gauge Na Stiglers Gauge

Mapumziko Mema Mwamba wa Siasa Za Ukanda wa Mashariki Na Pembe ya Africa
 
REDEEMER.

JF-Expert Member
Feb 22, 2015
8,957
2,000
Eti Rithlead rako rimefichwa wapi na modeleta?Nimeona ukiraramika na kumtukana. Usiwe unareta uchafu kwa hii section
Uzi mbona upo hot sana, najua moderator alieuhamisha ni Mkenya sababu kumekuwa na double standard humu, uzi unaoisema vibaya Tanzania ukiletwa na mkenya unaachwa utamalaki na hakuna wa kuugusa lakini tukileta vitu konki vya Tanzania haraka unapeperushiwa mbali

Kikubwa ni kwamba ujumbe umewafikia kwamba Tanzania sio level yenu, yaani tuna project mpaka tunachanganyikiwa, siku sio nyingi nitawaletea tena bonge la project kiwanda chenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya bidhaa 8 kikubwa balaa.
 
Kijibabu

JF-Expert Member
Apr 3, 2016
343
500
'Siwezi kuongeza Mshahara kwa kiwango hicho mnachokitaka, Na Kama nyongeza hiyo ya Mshahara ndio sharti pekee la kunipa kura Basi sitaki kura zenu...'-Jakaya Mrisho Kikwete 2010

Watu wakazusha Kuwa Jakaya kakataa kura Za Wafanyakazi Kumbe ule ulikuwa Ukweli Mchungu

Leo Hii wanakumbuka Hata ile Nyongeza ya wakati wa Jk waliyoita Ni kiduchu maana Mzee Baba Chuma Cha Pua Hata ile Annual Increament ya Kila July iliyokuwa Haina Mjadala kaipeleka Kwenye Standard Gauge Na Stiglers Gauge

Mapumziko Mema Mwamba wa Siasa Za Ukanda wa Mashariki Na Pembe ya Africa
zile changamoto alizopata JK kutoka kwa wafanyakazi hasa madaktari na walimu Chuma hakiwezi kuzimudu kabisa ndio maana kinajihami zisitokee. Muda mwingine JK anapomuita Chuma huku anacheka huwa naona kama anamkejeli kiaina

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom