Kenyatta akwepa kuhudhuria mkutano wa 18 wa viongozi wakuu wa nchi za Afrika Mashariki!

Ni kweli. Ila kwa hili kuna zaidi ya KAWAIDA. Maana angependa aungwe mkono na wenzake katika uchaguzi wao huko. Ama unaonaje kwa hili mkuu.
Kwani hao wenzake ni wapiga kura huko Kenya??

Acha kuonesha udhaifu wako waziwazi. Kabudi katueleza tutumie staha!!
 
1: Kwa nini unajielekeza kwamba labda tumemuudhi?. Ka yy ndio anaona aibu kwa aliyotutendea unaonaje hapo?

2:Unasema c kawaida yake kukosa mikutano hii. Je kola anapokuja huwa nchi yake ipo ktk mchakato wa uchaguzi?

Watanzania hebu tujiheshimu na mawazo yetu au ndio vyeti??

LET US ALSO KNOW YOUR SPECULATION ABOUT, PRESIDENT KAGAME? . Turn also to economic reasons.

Analyse President Museven very revealing speach, the clue is encrypted in it
 
Wana JF si kawaida marais kukosa kukutana hasa katika mikutano muhimu ya viongozi wa nchi za Afrika Mashariki.

Lakini jambo la kushangaza rais wa Kenya Uhuru Kenyatta AMEKWEPA kuhudhuria mkutano huu wa 18 wa HEADS of STATES ambao utafanyika hapa kwetu Tanzania na badala yake amemtuma Makamu wake wa rais. Mh William Ruto.

Kwa mtu wa kawaida atasema "Kwani kuna ubaya gani kama ana DHARURA?"
Ukweli ni kwamba hili SUSIO la MAKSUDI.
Waingereza wanasema "Giving it a wide berth/ KUJIWEKA MBALI."
Sikatai huenda wameongea kwenye simu na rais Magufuli na kutoa UDHURU wake. Lakini hata ni hivyo naamini hivyo ni visingizio vyake tu.

Diplomatic PUNDITS/wachambuaji wa mambo ya Kidiplomasia wanaweza kujua zaidi WHY NOW?
Naamini kuwa KUNA SABABU isiyompendeza kutoka kwetu Tanzania.

Ikizingatiwa huu ungekuwa ni mkutano wake wa mwisho kabla ya uchaguzi , hivyo ilikuwa ni FURSA NZURI sana ya kuomba KUUNGWA MKONO na MARAIS WENZAKE ili achaguliwe tena mara nyingine.
Ila sasa amewakwepa na Kutuma MSAIDIZI wake.

Hii ni kama ANATUTUMIA UJUMBE fulani ambao ni lazima TUUTAFSIRI haraka tuuelewe na tufanye kinachohitajika.

KUTOHUDHURIA huku kunaonyesha kuudhika kwake kwa namna moja ama nyingine Maana mikutano kama hii huwa hakosagi!

SWALI :Nini hasa ambacho huenda tumemuudhi hadi kutohudhuria mkutano MUHIMU kama huu?
Na je ni namna gani tunawez KUPOZA DHANA zake KIDIPLOMASIA bila ATHARI/Negative effects on our relationship na jirani zetu?

Kwani rais wako Magufuli amekacha kuhudhuria mikutano mingapi ya muhimu zaidi ya huu wa jana.??

Acha speculations. Kenyatta ana mambo ya muhimu ya kufanya zaidi ya kuhudhuria vikao kama hivi vya kinafiki
 
Kwani rais wako Magufuli amekacha kuhudhuria mikutano mingapi ya muhimu zaidi ya huu wa jana.??

Acha speculations. Kenyatta ana mambo ya muhimu ya kufanya zaidi ya kuhudhuria vikao kama hivi vya kinafiki
VIKAO vya KINAFIKI? Then unajua jambo tusilolijua. Hebu tueleze basi mkuu.
 
Rais Kenyatta kutohudhuria ni sababu amerejea Kenya kutoka ziara ndefu ya kwenda Uingereza na China. Pili kama inavyoeleweka uchaguzi mkuu wa Kenya upo karibu sasa amerudi ili apange mikakati ya uchaguzi huo.
Tuache kupiga ramli.

Wewe ni msemaji wake?
 
Hapo tunaweza kumsamehe rais Magufuli maana alikuwa bado ni WAZIRI na si MTAWALA.
Huu uvumi wa kupendelea upande mmoja Rais wetu angetoa msimamo ili kupunguza dhana kutoka upande ule mwingine!.
i suggest, endelea kufuatilia uhusiano wa hawa wawili hata baada ya Magu kuukwaa urais. Usiwe msahalifu hivyo
 
Peleka mbali diplomasia zako uchwara kwani JPM ameskip mikutano mingapi huko nje? Why not UK? Kwani hana vipaumbele vyake au udhuru muhimu; hata hivyo what are VP's for? Mara ngapi hapa Mama Samia ametuwakilisha nje?! Wacha ukajura bhana watu wafanye kazi na sio kuhangaika na njozi zako!
 
katika marais sita wa EAC, ni wangapi walihudhurua na wangapi walituma wawakilishi katika kikao cha kawaida cha jana?
 
Kwani hao wenzake ni wapiga kura huko Kenya??

Acha kuonesha udhaifu wako waziwazi. Kabudi katueleza tutumie staha!!
Si kuonyesha UDHAIFU ni kufikiria critically.
Acha nikupe mfano.
The INCUMBENT/Rais aliyeko madarakani sasa wa Kenya ni Uhuru Kenyatta.
Mara kwa mara nchi zilizo na UHUSIANO BORA hasa kama zetu ja JUMUIYA ya AFR-MRKI. MARAIS husaidia rais aliyeko MADARAKANI ili WAENDELEZE SERA na MAONO waliokuwa WAMEYAPANGA.

Wakati mwingine huwabidi kufanyiana KAMPENI za WAZI WAZI kwa kutuma VIONGOZI wa ngazi za juu KUMPIGIA debe the INCUMBENT ili ACHAGULIWE tena.

Mfano mzuri, Rais Kenyatta amefanya hivyo UGANDA wakati wa kampeni za Museveni kuwania AWAMU ya uongozi. ALITUMA MAWAZIRI na WANASIASA waliobobea ili kumfanyia KAMPENI.

Miongoni mwa WALIOENDA huko kumpigia debe ni HUYU Mh Ruto aliyepiga Kampeni naye huko Uganda AKIWAOMBA Waganda WAMCHAGUE tena.

INCUMBENT kwa INCUMBENT huitajiana hasa NYAKATI kama hizi.
Hiyo ndo maana yangu. Tunaweza ku sugar coat na kuruka ruka but that REMAINS my HYPOTHESIS!
 
Sababu nyingine ni Tanzania kuruhusu Odinga (NASA) kujenga data center nchini kwa ajili ya kudukua uchaguzi wa Kenya.
 
kenyata yuko busy na international platforoms uyu wa kwetu yuko kajifungia ndani anacheza draft yakubadilisha viongozi tuuu anasubiri matajiri wamfate izo dreamliner zake zitaishia EA
 
Kachukizwa na serikali kula rambi rambi ,kifo ambacho hata yeye Kenyatta alisikitika na kuomboleza hadharani .

Bora hujaja Kenyatta ungejiambukiza milaana bureeee hao waliokuja wanaendana nae
 
Nadhani Kagame na Nkurunziza pia hawakuhudhuria. Ikumbukwe pia kuwa Kenya na Rwanda waliishaonyesha mwelekeo wa kusaini ule mkataba tata wa EPA,hii ikiwa ni kwa maslahi ya nchi zao kibiashara. Kufanikiwa kwa mkataba wa EPA kunategemea kukubali kwa pamoja na kuusaini kama jumuia ya Afrika mashariki. Tanzania, Burundi na Uganda wana msimamo tofauti na Kenya+Rwanda. Nadhani hao wawili hawakutaka kuwepo ili kuepuka fedheha ya kuona mkataba walioupigia buruji ukichinjiwa baharini.
 
Sababu nyingine ni rais wetu kuruhusu Odinga kujenga data center nchini kwa ajili ya kudukua uchaguzi wa Kenya.
Hiyo data centre iko wapi? Unaweza kutoa msaada wa kuionyesha kwa manufaa ya serikali ya Kenya? Unaiamini sana internet protocol adress yako achani kuposti vitu msivovijua.
 
Viongozi wa Afrika Mashariki wanamtaka Raila Odinga kwa sababu ndo wanayeendana nae kimatendo na kimtazamao!!! Uhuru kaishawasoma ndo maana anawapotezea!!! Pia Uhuru ni level nyingine compared to the rest ambao wamezifanya/wanataka kuzifanya nchi wanazoziongoza kama za kwao binafsi!!!!
 
Hapo tunaweza kumsamehe rais Magufuli maana alikuwa bado ni WAZIRI na si MTAWALA.
Huu uvumi wa kupendelea upande mmoja Rais wetu angetoa msimamo ili kupunguza dhana kutoka upande ule mwingine!.

Sio kila jambo ni la kutoa msimamo! Wakati ule alipendelea Odinga, mm naamini hana sababu ya kuugeuka msimamo wake! Ila abake nao kimya kimya, sisi tuongee mwisho wake tutatulia!!!!
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom