Chamoto
JF-Expert Member
- Dec 7, 2007
- 8,327
- 17,523
Wakati nikiwa mdogo hakukua na Omo wala Blue band Tanzania, badala yake tulikuwa na Tan bond, sabuni za Mbuni (za mche) pamoja na Foma (sabuni ya unga). Baiskeli tulikuwa na kiwanda chetu pale Mwenge (Dar) kinaitwa Swala. Bata haikuwepo Tanzania, tulikuwa na maduka yetu ya viatu vya Bora.Na Yale maboksi matupu ya Surf, Colgate, Palmolive, Kiwi, Lactogen, baiskeli za Raleigh, matairi ya baiskeli Avon, Omo, Lifebuoy, makopo ya Blue Band, Milo, maziwa ya KCC, Kimbo, Cocoa na vinginevyo vingi mlivyokuwa mkipamba majumbani mwenu na kupiga navyo picha mmeshikilia mkononi! Zile taksi za Arusha Namanga zilizokuwa zikishindana nenda rudi mchana kutwa kupeleka watu shopingi Namanga! Na zile kanga za Mombasa zilizokuwa zinafichwa ndani ya matairi ya mabasi! Na matanki ya malori! Na yale magari ya Aspro, Cafenol, viatu vya Bata, Surf na Fixture Films yaliyokuwa yanafanya matangazo ya biashara ukiacha matangazo ya bidhaa za Kenya Radio Tanzania! Ninakushauri tena acha uliyokuwa ukiimba kwenye nyimbo za halaiki.
Hakuna hata bidhaa moja ya Kenya iliyokuwa inatengenezwa mwaka 1960 hivi sasa haipo! Zote bado zinatengenezwa na zipo.
Kumbe wewe ni bwana mdogo sana, huijui historia ya nchi yako. Ndiyo maana Magufuli juzi alimwagiza Ndalichako aangalie upya mitaala na ufundishaji wa historia ya Tanzania.