Kenya's Day of Pride; The Birth of a New Republic

Sasa hile public seal kubwa imefunuliwa na AG na ameiweka kwenye Katiba na sasa Mwanzo mpya umeanza leo. Siasa za kikabila na mashambani /bonde la ufa zaenda kuzikwa
 
Katiba mpya kupigiwa mizinga 28 na huku bendera kubwa ya Kenya ikipeperushwa. Sasa mizinga imeanza kupigwa. Kenyans deserve this.
 
Duh..naona mizinga inapigwa sas abaada ya wimbo wa Taifa kupigwa, ni kama vile wapepata uhuru mpya kabisaaaaa
 
:A S 8: a new dawn for Kenyans


Mkuu umeona hao vijana kwenye matawi ya miti lakini unaweza kuhisi wako vibrant wanaimba wimbo wa taifa na kuwave bandera za nchi yao.....inaonekana sasa uzalendo umewaingia
 
M7 na Kagame naona wapo pia katika meza Kuu. Jamani natumaini hii itaweza kuweka tumaini kwa watanzania nao kuanza kufikiria kuachana na 'kuweka' viraka katika 'godoro lililochakaa':smile-big: na 'kununua godoro jipya'

Bw. Raisi Bashir wa Sudan yupo pia. Je Kenya watamkamata huyu?
 
Chief Justice Hon, Gicheru anakula viapo vyake viwili....cha utii na cha kuitekeleza katiba ipasavyo
 
Sasa zamu ya CJ kula viapo viwili , cha ofisi na utii . CJ ANAKUWA MTU WA KWANZA kula kiapo kwa kutumia katiba mpya.
 
Mkuu nadhani AU walishakuwa na resolution ya kukataa hati ya kukamatwa kwake so kwa nchi zetu yeye anapeta tu

mwendo wa kulindana mpaka pale atakapoachia madaraka kama Pinochet wa Chile. Waafrika ndo tulivyo.
 
Unajua hapo ndo tunatakiwa kubadilika. Kama mtu anamawaa kwanza tuakikishe tunasafisha bala letu then ndo tuanze kulalamika ...kwa kweli Afrika tumezalisha madikteta wengi sana. Kuna mmoja yeye nahisi ni wa Kwanza kwa unyama huyu si mwingine bali rais wa Equatorial Guinea. Jamaa anagereza [kabla ya hapo alikuwa mkuu wa gereza hili kabla ya kumpindua mjomba wake 1979] linatwa 'Black Beach' Ukiingia humo ni balaa! Nchi yake ina watu laki sita na ni ya tatu kwa kuzalisha mafuta kusini mwa jangwa la sahara lakini ni masikini wa kutupwa na huyu dikteta ni tajiri wa kutupwa
 
Naona Amolo Odinga ndo anakula naye kiapo kipya .....anashangiliwa katika kila neno analosema kwenye kiapo.Jamaa mpiganaji sana huyu.
 
Naona Amolo Odinga ndo anakula naye kiapo kipya .....anashangiliwa katika kila neno analosema kwenye kiapo.Jamaa mpiganaji sana huyu.


Au hapo ndo wanasignify kwamba ndiye aliyeshinda mwaka 2008?
 
Back
Top Bottom