Kenyan Elections 2007: End Of An Era (error?)

Kenyan-Tanzanian

JF-Expert Member
Nov 7, 2006
302
2
--------Kenya Yakaribia Kanaan-------

Jamvi la kihistoria la mabepari wa kibaada-ukoloni nchini Kenya sasa ni bayana litajifunga mwishoni mwa mwaka huu. Hali hi ya kihistoria ambaye itaona mamlaka ikihamishwa toka katikati ya nchi hadi mashinani kwa namna mbalimbali (devolution of power) imetokana kukubalika kwa chama cha ODM na mgombeakiti cha urais, Raila Odinga - mwanawe muanzilishi wa siasa za upinzani nchini Kenya, Marehemu Mzee Jaramogi Oginga Odinga.

Raila ambaye alikuwa kizingiti muhimu katika ile jahazi ya kisiasa NARC iliyomng'oa Rais Mstaafu Moi mamlakani 2002 sasa anazidi kuvuma kama Musa ambaye waKenya waliowengi walidhani yupo ndani ya Rais Kibaki ila kwa maoni yao hawajaiona Kanani yake hadi wasasa. Mwaka wa 2005, baada ya Katiba Mpya iliyoonekana kuwa itazidikuzikita mizizi za mabepari waKenya na wameoziteka asasi za serekali kati (yaani centralized government)kupingwa vikali na wanachi waKenya wakiongozwa na Raila Odinga, Kibaki aliwatimua Raila na wenzake wengi tuu licha ya wao kumsaidia Kibaki mwenyewe kuingia ikulu japokuwa alikuwa kalazwa London baada ya ajali iliyotokea akiwa kwenye kampeni (2002).

Hivi leo, kila kuchao, kura za maoni, akina mama na maseela mitaani, wakongwe na watoto vitongojini kote nchini wanakubali kwamba Serekali ya ODM (Raila na wenzake waliotimuliwa na Kibaki)sio siri au ndoto tena ila wazo nyeti ambalo wakti wake umewadia. Uvumilivu umefika tamati. Mbegu ya fikra ya kisiasa iliyopandwa na waIngereza, ikapaliliwa na Serekali ya awamu ya kwanza ya Kenyatta pamoja na zile zilizofwata za Moi na Kibaki (sasa wanamlea mwanawe Kenyatta aiitwayo Uhuru pengine ariidhi Kibaki), mbegu hiyo imepanda mti wa sintofahamu nchini ambayo ni lazima ikatwe.

Nayo ile mbegu ya fikra ya kisiasa ya makamu wa Rais wa kwanza nchini chini ya Kenyatta yaani babke Raila aliyeitwa Jaramogi Oginga Odinga kumbe iliota hata ndani ya miiba. Sasa imewadia wakati ambayo mti huo wa kwanza wa siasa yaani ule wa Kenyatta ni lazima ukatwe ili ule mwingine yaani wa Jaramogi umee. WaKenya wanasema hapana Kibaki asiendelee kwasababu wako tayari kujaribu matunda ya uhuru yanayomea kwa mti tofuati wa kisiasa.

By voting for Raila and by proxy Jaramogi (posthumously)Kenyans will be symbolically saying to the Kibaki-Moi-Kenyatta clan a collective:

"No to centralized government that has only favoured central province, central government officials, central towns, central capital, central human capital, central education and other institutions, central literature, central anticolonial history, central intellectuals, central judiciary, executive and legislative arms of governance and all that have made an unjust centre to hold for four decades and yes to decentralization in all its forms, major and minor (from politics to literature)".

Hivi ndio maana najiunga na wananchi wenzangu watokao maeneo ambayoyamekuwa pembeni mwa ulaji wa keki ya kitaifa kubashiri kuwadia kwa serekali ya awamu ya nne yenye ari, kazi, nguzu mpya na hata mawazo mapya ya uongozi nchini. Karibuni ODM. Tawaleni Kenya.

Hizi hapa picha mbali mbali zinazotuweka hai ndani ya bahari hili la homa ya kisiasa au ukipenda "Election Fever".

1. [media]http://www.youtube.com/watch?v=wz3pXskASz4[/media]
2. [media]http://www.youtube.com/watch?v=tpZhJaJVbMI[/media]
3 http://www.youtube.com/watch?v=eiTfaoVBW9Y
4. [media]http://www.youtube.com/watch?v=dlusA1FcjtY[/media]
5. [media]http://www.youtube.com/watch?v=OjmGlaUJbKk[/media]
6. [media]http://www.youtube.com/watch?v=MSQ4ec_Lc78[/media]
7. [media]http://www.youtube.com/watch?v=HLm6vPCM61U[/media]
8. http://www.youtube.com/watch?v=_SMhwfswdCE
9. http://www.youtube.com/watch?v=FUtphQDc4Lk

PS: Ingawaje siasa za Kenya zimefananishwa na mawimbi ya bahari yaani zinaweza badilika wakati wowote ule na kupuliza upande tofauti na ule wa awali, hatakiwi mtu kuwa na akili za Albert Einstein kubashiri ni upande upe kati ya ODM (RAILA) na PNU (KIBAKI) utaingia Ikulu ya Nairobi, Januari 2008. Discover Raila, The Enigma of Kenyan Politics at www.raila2007.com

ODM! MAISHA BORA KWA WAKENYA WOTE (CCM! MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA)

http://www.youtube.com/watch?v=2RRLLaq2VM8
 
Isije kutokea kama huku maisha bora kwa kila mtanzania halafu imekuwa Maisha Duni kwa kila mtanzania.
Naishi na Rafiki zangu wakenya hapa wanatoka Central (ukikuyuni) hawataki kabisa kusikia Raila anavuma, ukiuliza sababu ya kumkataa Raila eti Hajataili.
Mmmoja anayetokea maeneo ya Mwambao ambako nadhani ndiyo kwenye umuhimu mkubwa wa wagombea wote wa Urais anakiri kwamba Kibaki ana kazi kubwa sana ya kushinda safari hii. Tusubiri tuone maana sisi wengine mambo ya Siasa za Kenya zinatupita kushoto kidogo.

Na ni vipi Musyoka akatengana na Raila?
 
@Sahara Voice,

Nashukuru kwa message yako.

Basi hao marafiki hizo ndio siasa zao eti! Lakini hata wenyewe wanajua kwamba Kibaki anastaafu December. Kura za maoni zinazofanywa na kampuni nne tofauti kila baada ya wiki mbili zinaonyesha Raila akiwa maarufu zaidi nchini. Anaongoza na 50-54%, akifwatwa na Kibaki 36-39% halafu Kalonzo 8%.

Kwa wakati huu Raila ni maarufu na anaongoza katika majimbo sita. Kibaki anaongoza jimbo lake la Eneo ya Kati (Central) huku Kalonzo akiongoza jimbo atokako la mashariki (Eastern). Zilizosalia (Western, Rift Valley, Nyanza, Nairobi, Coast na North Eastern) zote zinasema Raila Tosha! Na ama kweli atosha.

Issue ya Kalonzo kutengana na Raila sio simple. Kalonzo alikuwa anaamini kwamba yeye ndiye atateuliwa na ODM kuwania kiti cha urais kwa tikti ya chama hiyo. Lakin kulikuwepo na wanowania wengine saba akiwemo Raila. Wanne kati ya hawa wakajiuzulu' na kumwunga Raila mkono. Mmoja akajiondoa na mmoja akamwunga Kalonzo. Basi, Raila akamwachia Kalonzo chama kiitwacho ODM-KENYA na kuanzisha kipya kiitwacho ODM original. Akahama na wanne hao.

Kalonzo hakupiga hesabu zake vizuli. Angesoma ramani ya hisia nchini na aone kwamba siasa za sasa zimejengwa kwa misingi ya rika. WaKenya wengi wanasema awamu na muda ya wanasiasa wakongwe (65 years and above) imewadia na nilazima wafunganye waondoke mamlakani.

Raila sasa yuko na miaka 63. Asingelipata tikiti mwaka huu, asingelitoboa next time yaan 2012. Kwajili wakati huo wengi wakiwemo maadui zake wangemwona mzee na hawangemchagua. Ilikuwa bayana basi kwamba wale wenzake ambao ni wachanga kumliko wajiuzulu, waungane naye alafu yeye pia atawapasapot akistaafu. Kalonzo ambaye pia ni mchanga kuliko Raila hakuelewa hii hesabu, akadinda na sasa avuta mkia.

Wengine wanabashiri atanunuliwa na Kibaki waungane kumpinga vikali Raila. Lakini hata ukiweka 38+8 yaani asilimia ya kura zao za maoni pamoja utapata 46% na Raila angali atashinda akiendelea na 50 au 54% ameyopata tokea Septemba.

Siasa za Kenya ni siasa za kuungana kwa makabila zinazowakilishwa na vyama fulan fulan ili zipinge kabila zingine zinazowakilishwa na vyama fulani pia. Kwa sasa waKenya wasiotoka mkoa wa Kati (yaani wanaotoka mikoa zingine sita ukisahau ile ya Kalonzo) wanasema mkoa wa kati, kabila hiyo pamoja na chama chao PNU (anayotumia Kibaki) ni lazima zipatie kabila zingine nafasi pia wao wakule matunda ya uhuru. WaLuhya, waSomali, waJaluo, WaKalenjin na makabila zingine ndogo ndogo pamoja na jamii michanganyiko ziishizo mijini zipo ndani ya ODM original na zitashinda na Raila kwajili ya uzito wa namba zao.

waKikuyu na mabinamu zao kama vile waMeru, waEmbu na kabila zingine ndogo wako ndani ya PNU na wanasapot Kibaki.

Asikudanganye mtu, siasa za Kenya ni zaKikabila na juu hapa nimekupa picha halisi kuhusu siasa za huku. Basi Raila ni mLuo akiingia ataidhinisha katiba iliyobungeni iitwayo Katiba Bomas. Itaifanya Kenya iwe serekali ya majimbo kama vile Ujerumani, Nigeria, India, na US. Kila jamii itapewa nafasi kubwa ndani ya utawala wa jimbo lao. Serekali haitaishi Nairobi iliyozingirwa na jamii na mkoa moja yaani waKikuyu na mkoa wa Kati. Wajaluo, waLuhya, na wengine hawatasubiri maendeleo yaleyetwe toka Nairobi na serikali ya PNU.

Ndani ya katiba mpya kila mgombeaji aliyemuunga mkono Raila (Naiori&Nyanza province)atapata cheo. Mudavadi (Western) anayewakilisha waLuuhya atakua Vice President. Katiba mpya itajenga ofisi ya Waziri Mkuu ambaye atakuwa na makamu wawili. Ruto anayewakilisha waKalenjin (Rift Valley) atakuwa PM. Balala anayewakilisha waSwahili (Coast) atakuwa makamu wake wa Kwanza na Ngilu (anayetumiwa kumpinga Kalonzo Eastern province atakuwa naibu wapili na atasawasisha hesabu za kijinsia). Makabila mengine yanayosapot Raila yatapewa mamlaka katika uwaziri. Kama vile waSomali, waMaasai, waBorana, etc wanaotoka (North Eastern Province).

Hii sio habari hakika lakini kama sapota wa ODM ambaye nipo kwenye kamati mojawapo ya ODM inayompigia debe waziwazi Raila, ninapata picha fulan inayojitokeza kama hii hapa niliyokupatia.

Serakali ya majimbo ndio itaiwezesha Kenya kukata minyololo ya utovu wa usawa wa kiuchumi. Utovu huu ndio unachangia pakubwa ukabila nchini because inazifanya kabila zingine zinazojihi masikini kudhania kwamba waKikuyu wengi ni matajiri kwajili wako katikati ya chini ya Kenyatta na Kibaki.

Wacha tuzidikuikagua kinyang'anyiro hiki.
 
Ten years later Raila bado hajapata kiti cha urais na hatawahi tawala Kenya. Siasa za Kenya ni Wakenya tu wanaozielewa.
 
Ten years later Raila bado hajapata kiti cha urais na hatawahi tawala Kenya. Siasa za Kenya ni Wakenya tu wanaozielewa.
Upende usipende,huyu ndiye mkenya anayeaminika na wengi,,,,si wale wakulipa watu wajaze uwanja ndio aonekane yuko na following pia.
Labda waendele kumuibia .
 
Upende usipende,huyu ndiye mkenya anayeaminika na wengi,,,,si wale wakulipa watu wajaze uwanja ndio aonekane yuko na following pia.
Labda waendele kumuibia .
Hao wengi mbona hawapigi kura au si wakenya ni waganda? Hivi vitimbi vyake ndo vinampotezea kura. Kwa sarakasi Raila yupo sawa. Lakini hakuna anayemuamini ikifika kwenye uongozi. Alikuwa na miaka yake mitano ya kufanya kazi kama waziri mkuu, lakini hakuna kipya tulichokiona kando na kulialia kuhusu mkate nusu mara mkeka nusu na kuwabebesha 'security detail' wake choo kila alipoenda kwenye mazishi.
 
Hao wengi mbona hawapigi kura au si wakenya ni waganda? Hivi vitimbi vyake ndo vinampotezea kura. Kwa sarakasi Raila yupo sawa. Lakini hakuna anayemuamini ikifika ni uongozi. Alikuwa na miaka yake mitano kama waziri mkuu, lakini hakuna kipya tulichokiona kando na kulialia anataka mkate nusu, mkeka nusu na kuwabebesha 'security detail' yake choo kila alipohudhuria mazishi.
Mnaiba kama wajinga, errors ata mtoto mdogo anaona.
election ya date 26 ilifungua watu macho
 
Mnaiba kama wajinga, errors ata mtoto mdogo anaona.
election ya date 26 ilifungua watu macho
Labda uliibiwa wewe mwenyewe, kwenye ndoto. Acha ya oktoba 26, ambayo kama nakumbuka vizuri matokeo yake yalikubaliwa na mahakama ya kilele. Tuchape rewind kidogo, hadi agosti nane. Justice Maraga na wenzake walibatilisha matokeo ya uchaguzi huo. Mlisherehekea sana na kusifu mahakama lakini hata mahakama yenyewe haikusema kuna kura zozote zile zilizoibiwa. Uongo wa NASA hata usemwe mara mia utabaki kuwa uongo tu. Yaani mlizabwa kofi kama la sokwe akimchapa mbwa koko! Ngoma bado, 2022 itafika tu, na wembe utakuwa ni ule ule!
 
Ulienda shule kusoma,
kuna vitu inaonekana tu...
si eti sababu mtu ni mkikuyu lazma you support UHURU.
hiii ujinga lazma tutawacha,jamaa yeye anapigania tumbo na familia yake wewe umekaa hapo ati sycophant....
 
Anayetaja makabila ni wewe. Umeshindwa kujibu hoja yangu hapo juu kuhusu hiyo ndoto yako ya wizi wa kura. Sychophant ni wewe, ambaye unapoteza siku yako nzima kuapisha mtu afu baada ya hiyo anaenda nyumbani kwake! Unataka tuunge mkono mambo ya kipuuzi eti kwasababu tu rais Uhuru Kenyatta ni mkikuyu? Hadi sasa hivi ni nchi ngapi ambazo marais wao wamejitokeza kumpa 'rais Raila' hongera zao? Nitajie hata moja tu! Kwahivyo kila mtu hajui ukweli isipokuwa nyie wahaini wa NASA? Fungua macho wewe!
 
Ukweli utabaki kuwa ukweli.
watu ka nyinyi ndio mnafanya jamii yetu kila mtu atuchukie.
Odinga hajawahi shindwa since 2007 na watu wanajua vizuri.
RAILA ndio ataunganisha kenya kwa ujumla.
hizi akili za kiuthamaki hazitatusaidi.
Nchi ikiporomoka jamii yetu ndio itaumia zaidi juu ya less fake politicians.
kwetu tuko 5 but mmoja tu ndio anaamini uhuru.
MT.kenya too is shifting
 
Jamii yenu mkiwa na nani? Uliyekufahamisha kuhusu ukoo wangu ni nani? Ml. Kenya ni mlima tu, wananchi ndo wanaopiga kura, tena wanavopenda wala hakuna yeyote ule aliyewashurutisha! Raila aunganishe nchi? Hehehe, we jamaa bana. :D Hata kuapishwa kwake tu watu walikuwa wanaongea kilugha chao. Kama Raila hajashindwa hata uchaguzi mmoja tafadhali nitegulie kitendawili hiki; Magavana wa Jubilee, 34, NASA, 13! Niendelee kuhusu wingi wa maseneta, waakilishi wa wanawake, wabunge, na madiwani wa Jubilee au hiyo itakuwa kazi ya ziada kwako? Mji nimekupa Moyale. Haya basi, hadithi njoo!
 
Ten years later Raila bado hajapata kiti cha urais na hatawahi tawala Kenya. Siasa za Kenya ni Wakenya tu wanaozielewa.
Usijifanye hujui kilichotokea..... Huyo ruto ambaye yupo serikalini leo, by then alidai kura ziliibwa na ndio alianzisha mauaji kwanni usimfate umuulize what really happened hawakuingia ikulu???

Kivuitu alishasema alimtangaza ambaye hakushinda sasa unajifanya hujui kipi kilitokea
 
Hao wengi mbona hawapigi kura au si wakenya ni waganda? Hivi vitimbi vyake ndo vinampotezea kura. Kwa sarakasi Raila yupo sawa. Lakini hakuna anayemuamini ikifika kwenye uongozi. Alikuwa na miaka yake mitano ya kufanya kazi kama waziri mkuu, lakini hakuna kipya tulichokiona kando na kulialia kuhusu mkate nusu mara mkeka nusu na kuwabebesha 'security detail' wake choo kila alipoenda kwenye mazishi.
Hakuna alilofanya?? Vp kuhusu katiba hii ya sasa mliyojidai nayo kma si kelele za Raila kupinga ile mbovu iliokuwa proposed 2004 kma sikosei unafkiri mngepata serikali za ugatuzi lini??? Katiba ndio moyo wa nchi na huwezi kuzungumzia katiba mpya ya kenya bila kumtaja raila nyie endeleeni tu kuiba kura lakini ukweli utabaki kuwa Raila ndio baba wa siasa za kenya
 
Kelele za Raila, baba wa siasa, hayo ni maneno uliyoyatumia wewe. Katiba tuliipigia kura sisi sote. Alilia sana ili katiba ibadilishwe lakini ilikuwa ni kwa manufaa yake si kwa wakenya. Hiyo hiyo katiba ndo inatumiwa kumpiga kiboko. Lakini kwa uongozi zero, alitafuna pesa za Kazi kwa Vijana. Soma kitabu cha Miguna Miguna utaelewa ufisadi wa Raila. Urais, hatauona ng'o! Abaki huko huko upinzani anakong'aa!
 
Mkuu we ni kabila gani?? Just asking maana kwa kenya kabla hujauliza msimamo wa kisiasa lazma ujue kabila la mtu ili usimchoshe!!!
 
Mkuu we ni kabila gani?? Just asking maana kwa kenya kabla hujauliza msimamo wa kisiasa lazma ujue kabila la mtu ili usimchoshe!!!
Baba yangu, kabila tofauti na mama. Babu yangu upande wa baba, kabila tofauti na bibi. Usitake niingie kwenye somo la biologia. Najitambua kama mkenya tribe-less! Lugha za asili naongea kimeru, kikikuyu na kimaasai cha kuunga unga pia. Sasa wewe tegua hicho kitendawili mwenyewe.
 
Kumbe unatokea central corridor!!! Basi nimeshapata majibu yote niliyotaka....
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Back
Top Bottom