Kenyan Elections 2007: End Of An Era (error?) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kenyan Elections 2007: End Of An Era (error?)

Discussion in 'Kenyan News and Politics' started by Kenyan-Tanzanian, Oct 26, 2007.

 1. Kenyan-Tanzanian

  Kenyan-Tanzanian JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2007
  Joined: Nov 7, 2006
  Messages: 307
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  --------Kenya Yakaribia Kanaan-------


  Jamvi la kihistoria la mabepari wa kibaada-ukoloni nchini Kenya sasa ni bayana litajifunga mwishoni mwa mwaka huu. Hali hi ya kihistoria ambaye itaona mamlaka ikihamishwa toka katikati ya nchi hadi mashinani kwa namna mbalimbali (devolution of power) imetokana kukubalika kwa chama cha ODM na mgombeakiti cha urais, Raila Odinga - mwanawe muanzilishi wa siasa za upinzani nchini Kenya, Marehemu Mzee Jaramogi Oginga Odinga.

  Raila ambaye alikuwa kizingiti muhimu katika ile jahazi ya kisiasa NARC iliyomng'oa Rais Mstaafu Moi mamlakani 2002 sasa anazidi kuvuma kama Musa ambaye waKenya waliowengi walidhani yupo ndani ya Rais Kibaki ila kwa maoni yao hawajaiona Kanani yake hadi wasasa. Mwaka wa 2005, baada ya Katiba Mpya iliyoonekana kuwa itazidikuzikita mizizi za mabepari waKenya na wameoziteka asasi za serekali kati (yaani centralized government)kupingwa vikali na wanachi waKenya wakiongozwa na Raila Odinga, Kibaki aliwatimua Raila na wenzake wengi tuu licha ya wao kumsaidia Kibaki mwenyewe kuingia ikulu japokuwa alikuwa kalazwa London baada ya ajali iliyotokea akiwa kwenye kampeni (2002).

  Hivi leo, kila kuchao, kura za maoni, akina mama na maseela mitaani, wakongwe na watoto vitongojini kote nchini wanakubali kwamba Serekali ya ODM (Raila na wenzake waliotimuliwa na Kibaki)sio siri au ndoto tena ila wazo nyeti ambalo wakti wake umewadia. Uvumilivu umefika tamati. Mbegu ya fikra ya kisiasa iliyopandwa na waIngereza, ikapaliliwa na Serekali ya awamu ya kwanza ya Kenyatta pamoja na zile zilizofwata za Moi na Kibaki (sasa wanamlea mwanawe Kenyatta aiitwayo Uhuru pengine ariidhi Kibaki), mbegu hiyo imepanda mti wa sintofahamu nchini ambayo ni lazima ikatwe.

  Nayo ile mbegu ya fikra ya kisiasa ya makamu wa Rais wa kwanza nchini chini ya Kenyatta yaani babke Raila aliyeitwa Jaramogi Oginga Odinga kumbe iliota hata ndani ya miiba. Sasa imewadia wakati ambayo mti huo wa kwanza wa siasa yaani ule wa Kenyatta ni lazima ukatwe ili ule mwingine yaani wa Jaramogi umee. WaKenya wanasema hapana Kibaki asiendelee kwasababu wako tayari kujaribu matunda ya uhuru yanayomea kwa mti tofuati wa kisiasa.

  By voting for Raila and by proxy Jaramogi (posthumously)Kenyans will be symbolically saying to the Kibaki-Moi-Kenyatta clan a collective:

  "No to centralized government that has only favoured central province, central government officials, central towns, central capital, central human capital, central education and other institutions, central literature, central anticolonial history, central intellectuals, central judiciary, executive and legislative arms of governance and all that have made an unjust centre to hold for four decades and yes to decentralization in all its forms, major and minor (from politics to literature)".


  Hivi ndio maana najiunga na wananchi wenzangu watokao maeneo ambayoyamekuwa pembeni mwa ulaji wa keki ya kitaifa kubashiri kuwadia kwa serekali ya awamu ya nne yenye ari, kazi, nguzu mpya na hata mawazo mapya ya uongozi nchini. Karibuni ODM. Tawaleni Kenya.

  Hizi hapa picha mbali mbali zinazotuweka hai ndani ya bahari hili la homa ya kisiasa au ukipenda "Election Fever".

  1. [media]http://www.youtube.com/watch?v=wz3pXskASz4[/media]
  2. [media]http://www.youtube.com/watch?v=tpZhJaJVbMI[/media]
  3 http://www.youtube.com/watch?v=eiTfaoVBW9Y
  4. [media]http://www.youtube.com/watch?v=dlusA1FcjtY[/media]
  5. [media]http://www.youtube.com/watch?v=OjmGlaUJbKk[/media]
  6. [media]http://www.youtube.com/watch?v=MSQ4ec_Lc78[/media]
  7. [media]http://www.youtube.com/watch?v=HLm6vPCM61U[/media]
  8. http://www.youtube.com/watch?v=_SMhwfswdCE
  9. http://www.youtube.com/watch?v=FUtphQDc4Lk


  PS: Ingawaje siasa za Kenya zimefananishwa na mawimbi ya bahari yaani zinaweza badilika wakati wowote ule na kupuliza upande tofauti na ule wa awali, hatakiwi mtu kuwa na akili za Albert Einstein kubashiri ni upande upe kati ya ODM (RAILA) na PNU (KIBAKI) utaingia Ikulu ya Nairobi, Januari 2008. Discover Raila, The Enigma of Kenyan Politics at www.raila2007.com

  ODM! MAISHA BORA KWA WAKENYA WOTE (CCM! MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA)

  http://www.youtube.com/watch?v=2RRLLaq2VM8
   
 2. f

  faizoo New Member

  #2
  Oct 28, 2007
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ama for sure ODM ndio maisha bora
   
 3. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2007
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Isije kutokea kama huku maisha bora kwa kila mtanzania halafu imekuwa Maisha Duni kwa kila mtanzania.
  Naishi na Rafiki zangu wakenya hapa wanatoka Central (ukikuyuni) hawataki kabisa kusikia Raila anavuma, ukiuliza sababu ya kumkataa Raila eti Hajataili.
  Mmmoja anayetokea maeneo ya Mwambao ambako nadhani ndiyo kwenye umuhimu mkubwa wa wagombea wote wa Urais anakiri kwamba Kibaki ana kazi kubwa sana ya kushinda safari hii. Tusubiri tuone maana sisi wengine mambo ya Siasa za Kenya zinatupita kushoto kidogo.

  Na ni vipi Musyoka akatengana na Raila?
   
 4. Kenyan-Tanzanian

  Kenyan-Tanzanian JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2007
  Joined: Nov 7, 2006
  Messages: 307
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  @Sahara Voice,

  Nashukuru kwa message yako.

  Basi hao marafiki hizo ndio siasa zao eti! Lakini hata wenyewe wanajua kwamba Kibaki anastaafu December. Kura za maoni zinazofanywa na kampuni nne tofauti kila baada ya wiki mbili zinaonyesha Raila akiwa maarufu zaidi nchini. Anaongoza na 50-54%, akifwatwa na Kibaki 36-39% halafu Kalonzo 8%.

  Kwa wakati huu Raila ni maarufu na anaongoza katika majimbo sita. Kibaki anaongoza jimbo lake la Eneo ya Kati (Central) huku Kalonzo akiongoza jimbo atokako la mashariki (Eastern). Zilizosalia (Western, Rift Valley, Nyanza, Nairobi, Coast na North Eastern) zote zinasema Raila Tosha! Na ama kweli atosha.

  Issue ya Kalonzo kutengana na Raila sio simple. Kalonzo alikuwa anaamini kwamba yeye ndiye atateuliwa na ODM kuwania kiti cha urais kwa tikti ya chama hiyo. Lakin kulikuwepo na wanowania wengine saba akiwemo Raila. Wanne kati ya hawa wakajiuzulu' na kumwunga Raila mkono. Mmoja akajiondoa na mmoja akamwunga Kalonzo. Basi, Raila akamwachia Kalonzo chama kiitwacho ODM-KENYA na kuanzisha kipya kiitwacho ODM original. Akahama na wanne hao.

  Kalonzo hakupiga hesabu zake vizuli. Angesoma ramani ya hisia nchini na aone kwamba siasa za sasa zimejengwa kwa misingi ya rika. WaKenya wengi wanasema awamu na muda ya wanasiasa wakongwe (65 years and above) imewadia na nilazima wafunganye waondoke mamlakani.

  Raila sasa yuko na miaka 63. Asingelipata tikiti mwaka huu, asingelitoboa next time yaan 2012. Kwajili wakati huo wengi wakiwemo maadui zake wangemwona mzee na hawangemchagua. Ilikuwa bayana basi kwamba wale wenzake ambao ni wachanga kumliko wajiuzulu, waungane naye alafu yeye pia atawapasapot akistaafu. Kalonzo ambaye pia ni mchanga kuliko Raila hakuelewa hii hesabu, akadinda na sasa avuta mkia.

  Wengine wanabashiri atanunuliwa na Kibaki waungane kumpinga vikali Raila. Lakini hata ukiweka 38+8 yaani asilimia ya kura zao za maoni pamoja utapata 46% na Raila angali atashinda akiendelea na 50 au 54% ameyopata tokea Septemba.

  Siasa za Kenya ni siasa za kuungana kwa makabila zinazowakilishwa na vyama fulan fulan ili zipinge kabila zingine zinazowakilishwa na vyama fulani pia. Kwa sasa waKenya wasiotoka mkoa wa Kati (yaani wanaotoka mikoa zingine sita ukisahau ile ya Kalonzo) wanasema mkoa wa kati, kabila hiyo pamoja na chama chao PNU (anayotumia Kibaki) ni lazima zipatie kabila zingine nafasi pia wao wakule matunda ya uhuru. WaLuhya, waSomali, waJaluo, WaKalenjin na makabila zingine ndogo ndogo pamoja na jamii michanganyiko ziishizo mijini zipo ndani ya ODM original na zitashinda na Raila kwajili ya uzito wa namba zao.

  waKikuyu na mabinamu zao kama vile waMeru, waEmbu na kabila zingine ndogo wako ndani ya PNU na wanasapot Kibaki.

  Asikudanganye mtu, siasa za Kenya ni zaKikabila na juu hapa nimekupa picha halisi kuhusu siasa za huku. Basi Raila ni mLuo akiingia ataidhinisha katiba iliyobungeni iitwayo Katiba Bomas. Itaifanya Kenya iwe serekali ya majimbo kama vile Ujerumani, Nigeria, India, na US. Kila jamii itapewa nafasi kubwa ndani ya utawala wa jimbo lao. Serekali haitaishi Nairobi iliyozingirwa na jamii na mkoa moja yaani waKikuyu na mkoa wa Kati. Wajaluo, waLuhya, na wengine hawatasubiri maendeleo yaleyetwe toka Nairobi na serikali ya PNU.

  Ndani ya katiba mpya kila mgombeaji aliyemuunga mkono Raila (Naiori&Nyanza province)atapata cheo. Mudavadi (Western) anayewakilisha waLuuhya atakua Vice President. Katiba mpya itajenga ofisi ya Waziri Mkuu ambaye atakuwa na makamu wawili. Ruto anayewakilisha waKalenjin (Rift Valley) atakuwa PM. Balala anayewakilisha waSwahili (Coast) atakuwa makamu wake wa Kwanza na Ngilu (anayetumiwa kumpinga Kalonzo Eastern province atakuwa naibu wapili na atasawasisha hesabu za kijinsia). Makabila mengine yanayosapot Raila yatapewa mamlaka katika uwaziri. Kama vile waSomali, waMaasai, waBorana, etc wanaotoka (North Eastern Province).

  Hii sio habari hakika lakini kama sapota wa ODM ambaye nipo kwenye kamati mojawapo ya ODM inayompigia debe waziwazi Raila, ninapata picha fulan inayojitokeza kama hii hapa niliyokupatia.

  Serakali ya majimbo ndio itaiwezesha Kenya kukata minyololo ya utovu wa usawa wa kiuchumi. Utovu huu ndio unachangia pakubwa ukabila nchini because inazifanya kabila zingine zinazojihi masikini kudhania kwamba waKikuyu wengi ni matajiri kwajili wako katikati ya chini ya Kenyatta na Kibaki.


  Wacha tuzidikuikagua kinyang'anyiro hiki.
   
Loading...