Kenya yatangaza kutopokea mahindi Tanzania na Uganda

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Mamlaka ya Kilimo na Chakula ya Kenya imesema uchunguzi umebaini kuwa mahindi yayoingia kutoka Tanzania na Uganda sio salama kwa matumizi ya wakenya

Wamesema mahindi hayo yana kiwango kikubwa cha mycotoxins, hasa aflatoxins na fumonisins ambazo yanajulikana kusababisha saratani

Sumu hizo zimesababisha vifo vya wakenya wengi kwa miaka, hali iliyosababisha wachukue hatua ya kuacha kupokea mahindi kutoka Tanzania na Uganda

Aidha wamesema wataendelea kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na nchi wazoshirikiana nazo kibiashara na wanasubiri kuona washikadau wakilizungumzia tatizo hilo
==
1614971110985.png
 

Attachments

  • Aspergillus_flavus_and_aflatoxin_contamination_in_the_maize_value.pdf
    715.2 KB · Views: 11
the real issue hapa ni kama kweli mahindi kutoka uganda na Tanzania zina level ya juu ya hizi mycotoxins....tuache hizi shallow minds kuona kila kitu ni vita. In civilized societies matters health wanazichukulia serious sana
Umenena kweli kabisa. Serikali yetu ilifanya kuna kipindi ilikosea sana, yaani maafisa kilimo wale wa mpaka vijijini waliondolewa, kwa sehemu kubwa kwa sababu ya maslahi binafsi ya wanasiasa wachache, so wakulima wameendelea kulima with no utalaamu na uhifadhi na matokeo yake ndiyo hayo.

Wewe cheki tu hata Tanzania, yaani cancer mpaka vijijini, kuna hiki kituo cha ufafiti ya kilimo ukiwatembelea hakika utaacha kula ugali. Mimi tangu nijue hilo nilishaacha kula ugali wa mahindi ni muhogo kwenda mbele.

Nadhani wizara ya kilimo waweke mkakati maalumu, wawarejeshe au waajiri maafisa kilimo waende vijijini wasaidie wananchi namna ya kuvuna na kuhifadhi chakula. Yaani hata kwenye maghala yetu ni tatizo.

Kuna jamaa yangu mzigo wake wa tani moja ya karanga ulizuiliwa kuingia UK, ikabidi urudi bongo na kuuteketeza.
 
Umenena kweli kabisa. Serikali yetu ilifanya kuna kipindi ilikosea sana, yaani maafisa kilimo wale wa mpaka vijijini waliondolewa, kwa sehemu kubwa kwa sababu ya maslahi binafsi ya wanasiasa wachache, so wakulima wameendelea kulima with no utalaamu na uhifadhi na matokeo yake ndiyo hayo...
Kwanza njugu huwa ina aflatoxin sana hata kushinda mahindi ikiwa hutoihifadhi kwa njia inayostahili. Halafu wazungu wakipima wapate aflatoxin hata kidogo tu basi mzigo wako unakataliwa.
 
Back
Top Bottom