Kenya yapanga kuanza kusafirisha Chai Nyeusi kwenye soko la China

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,006
1,026
082482d8c720412ebdef9bffed8ae9ba.jpg


58643729fd1b43a8b0c4ed4a86510ddf.jpg


80f7d7d1631b412dbdc74bed57801baa.jpg


Kenya inapanga kuanza kuuza chai nyeusi kwenye soko la China kufuatia kuongezeka kwa mahitaji ya bidhaa hiyo kwenye soko la China. Nia hiyo ya Kenya imejulikana kwenye ziara iliyofanywa na balozi mteule wa Kenya nchini China Bibi Muthoni Gichohi, kwenye kiwanda cha chai cha Nduti mjini Murang’a.

Pamoja na ukweli kwamba China ndio chimbuko la chai duniani, na China inazalisha kwa wingi chai ya aina mbalimbali, kutokana na kuongezeka kwa mapato ya wakazi wa kawaida katika maeneo ya mijini nchini China, wakazi wengi wamekuwa wakipenda kuonja chai kutoka maeneo mengine, na chai ya Kenya ni moja kati ya chai zinazopendwa kwenye soko la China.

Kutokana na ongezeko la mahitaji ya chai hiyo, serikali ya China kwa kushirikiana na balozi za nchi mbalimbali za Afrika Mashariki imekuwa ikiweka majukwaa mbalimbali yenye lengo la kutangaza chai hiyo na hata kuwawezesha wateja wa China kununua chai hiyo moja kwa moja kutoka kwa wafanyabiashara na wakulima wa Afrika.

China na Kenya zimekuwa na ushirikiano mzuri katika sekta ya biashara na uchumi. Licha ya changamoto zilizotokana na janga la COVID-10 biashara kati ya pande hizi mbili imekuwa ikiendelea kwa viwango tofauti. Meneja wa kampuni moja ya Chai ya Kenya Bw Benjamin alisema, “tunatumia akaunti ya Meet Africa kukutana na marafiki kwa njia ta TikTok. Kupitia njia hiyo, tunaweza kuwasiliana na kila aina ya watu wa China na kuitangaza chai ya Kenya na utamaduni wa Kenya."

Bw. Benjamin anajua kuwa wachina ni watu wenye uelewa mkubwa kuhusu Chai, kwa kuwa China ni mzalishaji mkubwa wa Chai. Lakini si wachina wengi wanaojua kuwa Kenya ni moja ya nchi zinazozalisha chai kwa wingi barani Afrika, lakini wanapojua kuwa Kenya inazalisha Chai na ni nchi iliyo katika eneo la Ikweta, wana hamu ya kuonja chai ya Kenya. Lakini wakenya nao huwa wanapata fursa ya kuonja chai ya China.

Mbali na kuuza chai kupitia jukwaa la mtandao, wakenya pia wananufaika na fursa mbalimbali za biashara ya mazao ya kilimo zinazotolewa na China kwa nchi za Afrika. Moja ya fursa hizo ni kuruhusu makampuni ya Kenya kuingia China na kushiriki moja kwa moja kwenye maonesho ya kimataifa yanayofanyika hapa nchini China.

“Mara nyingi huwa tunatembelewa na baadhi ya watu karibu na duka letu la chai, na tunakaa na kuzungumza nao kwa muda mrefu, tukionja chai ya kung fu na kubadilishana uzoefu. Uzuri wa utamaduni wa chai wa Kichina hufanya mawasiliano haya kuwa ya kipekee", alisema Bw Benjamin.

Bw. Benjamin anasema yeye ni mnufaika wa “Mpango wa Mkanda mmoja, Njia moja” ambao anaona ni mpango muhimu katika kumuwezesha yeye na watu wengine wa Kenya, haswa wakulima wa mashambani, kunufaika na kuboresha maisha yao.

Mwaka 2021 Bw. Benjamin alishiriki kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Viwanda ya China, na alitumia fursa hiyo kuitangaza chai ya Kenya, sio tu kwa wachina, bali pia kwa wengine walioshiriki kwenye maonyesho hayo.
 
Back
Top Bottom