Kenya yaipa UNHCR siku 14 kufunga kambi ya Daadab na Kakuma

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Kenya imeamuru kambi mbili kubwa zaidi za wakimbizi nchini humo zifungwe ndani ya kipindi cha wiki mbili.

Serikali ya nchi hiyo imelipatia shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi, UNHCR, siku kumi na nne kufunga kambi za Dadaab na Kakuma, zinazowahifadhi wakimbizi wapatao laki tano.

Imesema kinyume cha hivyo, wakimbizi hao watasafirishwa hadi kwenye mpaka wake na Somalia.

Ujumbe huo uliwasilishwa Jumanne na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Fred Matiang'i alipokutana na maafisa wa shirika hilo la wakimbizi kwenye afisi yake mjini Nairobi.

"Hatua hiyo imechukuliwa kwa sababu za usalama wa kitaifa," alisema Matiang'i.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, Matiang’i alimwambia mwakilishi wa UNHCR nchini Kenya, Fathiaa Abdala, kwamba hakutakuwa na mjadala wowote kuhusu suala hilo.

Mnamo mwaka wa 2013, serikali ya Kenya ilikuwa imekubali kuwahamisha wakimbizi hao kwa awamu tatu, lakini kufikia sasa, ni wakimbizi 14,000 pekee, ambao wamehamishwa.

Kati ya masuala mengine, serikali imekuwa ikilalamika kwamba, licha ya ahadi za mara kwa mara, za misaada kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, kwa kiasi kikubwa imeendela kuubeba mzigo wa kuwahifadhi wakimbizi hao peke yake.

Kenya ilitaka kuzifunga kambi hizo mwaka wa 2016 kufuatia mashambulizi ya liyoaminika kutekelezwa na wanamgambo wa asili ya Somalia.

Kambi hizo zimekuwepo tangu maika ya tisini wakati ambapo vita vya wenyewe kwa wenyewe vilianza nchini Somalia, na ambavyo vinaendelea hadi sasa. Wengi wa wakimbizi hao ni raia wa Somalia.
 
Kenya wako sahihi kama un hawawezi kuzuia silaha zisiende kwa alshabab kwanini Kenya waendelee kubeba mizigo isiyowahusu, wawachukue wawapeleke huko zinazotoka hizo silaha labda watajirudi
 
Watu laki tano unawaamishaje bila maandalizi ya wanakoenda? Waziri matiangi haoni kwamba takwimu zinaupinga uamuzi wa serikali yake?
 
Kweli kabisa hata nchi za ulaya zilikataa kupokea wakimbizi toka libya na pengine kumbe walijua hata magaidi ujipenyeza humo humo na leo ulaya kila kukicha ugaidi unasumbua.
 
Kweli kabisa hata nchi za ulaya zilikataa kupokea wakimbizi toka libya na pengine kumbe walijua hata magaidi ujipenyeza humo humo na leo ulaya kila kukicha ugaidi unasumbua.
Zilikubali bwana waliokataa ni poland na austria tu kwa ulaya magharibi tu.
 
Kesi zilizopo zichambue.zilikubali mara ya kwanza
Ninachofahamu hadi sasa bado wanachukua ila kwa number ndogo sana tofauti na mwanzo na sababu kubwa ni corona virus na ya pili ni hiyo uliyotaja kuwa wakimbizi wanafanya uhalifu sana kwenye hizi host countries hali iyopelekea wanasiasa wa mlengo wa kulia wanaopinga wakimbizi kupata umaarufu.
 
Back
Top Bottom