Kenya yaiangukia miguuni tena AU kuhusiana na kesi zake zilizoko ICC

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
MusyokaKalonzo01.bmp
Serikali ya Kenya kwa mara nyingine tena imeutaka Umoja wa Afrika kuisaidia katika jitihada zake za kutaka kesi zake za washukiwa wakuu wa machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 zilizoko katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ziahirishwe. Akihitimisha duru ya pili ya ziara za kidiplomasia katika kanda ya Afrika Magharibi, Makamu wa Rais wa Kenya Kalonzo Musyoka, kwa mara nyingine tena ameitaka AU iisaidie nchi yake katika ombi lake la kutaka kesi za watuhumiwa 6 wa machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu wa 2007, zilizoko katika mahakama ya ICC ziahirishwe kwa muda wa mwaka mmoja ili nchi hiyo iweze kuunda mahakama itakayoweza kuzishughulikia kesi hizo katika viwango vya kimataifa na pia kwa kuhofu kuwa kupelekwa mjini Hague Uholanzi watuhumiwa hao ambao baadhi yao ni wanasiasa watajika, huenda kukasababisha machafuko mapya nchini Kenya.
Wiki iliyopita, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikatalia mbali ombi hilo la Kenya la kutaka kesi hizo ziakhirishwe.
 
Back
Top Bottom