Kenya: Waziri wa Fedha, Henry Rotich kukamatwa

Duh! Akikamatwa huyo nitaamini hii serikali ina haja ya kumaliza ufisadi, maana ni mmojawapo wa mawaziri wenye nguvu sana seriklini. Nilikua nimeanza kumchoka rais Uhuru kwenye hili la ufisadi.
Japo huyu waziri hujituma sana, mchapa kazi wa kueleweka, sijui shetani gani kamuingia hadi atajwe kwenye mambo ya kihivi.
Waliokamatwa wote ni wakuu sana, watu wa karibu kwa rais Uhuru, tuone huu mchezo unavyokwenda, rais aonyeshe uongozi, asizuie wala kuingilia kati.
Rushwa na ufisadi Kenya mnauita aggressive na uchapa kazi
 
Mkuu wa mashtaka nchini Kenya Nurdin Hajj ametoa warrant ya kukamatwa waziri wa fedha wa Kenya na maofsa wengine 28 akiwemo mtunza hazina mkuu was serkal mapema leo vyombo vya habari vya Kenya vimeripoti

Tuhuma za ufisadi wa pesa za ujenzi wa mabwawa ya maji zilichukua sura Mpya tangu mwaka jana hivyo kuhitajika uchunguzi zaidi ulio zusha mvutano kati ya makamo wa rais samoei rutto na kinara wa upinzani Raila Odinga

Maafsa kadha wa kigeni pia kujumuishwa katika kamatakamata hiyo


Chanzo Kenya media houses


=============

Waziri wa fedha Kenya Henry Rotich amejisalimisha kwa maafisa wa upelelezi hii leo, muda mfupi baada ya mkurugenzi wa mashtaka nchini kuagizwa akamatwe.

Kwa mujibu wa Nairobi News, Waziri Rotich alipelekwa kwa gari hadi katika makao makuu ya idara ya upelelezi ambako anahojiwa kuhusu malipo yaliotolewa kwa ujenzi wa mabwawa mawili nchini.

Anatuhumiwa kukiuka muongozo wa utoaji wa kandarasi iliopewa kampuni ya Italia CMC de Ravenna yenye thamani ya zaidi ya dola milioni 450 kwa ujenzi wa mabwawa.

Hapo awali, mkurugenzi wa mashtaka Kenya aliagiza kukamatwa kwa waziri wa fedha Henry Rotich na ashtakiwe kuhusu ufisadi

Mkurugenzi huyo wa mashtaka Noordin Haji amekuwa akizungumza katika vyombo vya habari kuhusu uamuzi wa kumshtaki waziri wa fedha Kenya Henry Rotich, na maafisa wengine wa serikali kuhusu kandarasi zilizotolewa kwa kampuni ya Italia kujenga mabwawa mawili

Aisee Uhuru is for real!

Huwezi compare na hii bure huku TZ!
 
Duh! Akikamatwa huyo nitaamini hii serikali ina haja ya kumaliza ufisadi, maana ni mmojawapo wa mawaziri wenye nguvu sana seriklini. Nilikua nimeanza kumchoka rais Uhuru kwenye hili la ufisadi.
Japo huyu waziri hujituma sana, mchapa kazi wa kueleweka, sijui shetani gani kamuingia hadi atajwe kwenye mambo ya kihivi.
Waliokamatwa wote ni wakuu sana, watu wa karibu kwa rais Uhuru, tuone huu mchezo unavyokwenda, rais aonyeshe uongozi, asizuie wala kuingilia kati.

Hii ni PR tu. Nurdin na Kinoti wamekuwa watu wa domo siku zote. Yaani wanapenda media utadhani ni slay queens.
 
Kukamatwa ni rahisi tatizo ni kufungwa. Hawawezi fungwa jela. Halafu wacha tuone kama ataresign since Kenyatta said that anyone charged in court must resign. Kuna kamiti hapo ina watu ninety percent kutoka kabila moja ndio ujuwe Kenya bado tuna ujinga ya tribalism na sijui itaisha lini? Ile siku mtu ataajiriwa based on competency rather than tribe tutakuwa sawa. It is unacceptable for a tender committee of a govt body KVDA to have everyone except one person coming from one community. Halafu munaexpect nini when such cronism and nepotism is malignant in the KE govt. Corruption will probably never end. Halafu ngoja usikie upuzi ya "watu wetu wanaangamizwa"

Hivyo ndivyo kunaenda na Regional Development Authorities. Hebu angalia bodi ya Lkae Basin Development Authority. http://www.lbda.co.ke/index.php/who-we-are/board-of-directors
 
Back
Top Bottom