Kenya: Wasichana wa kidato cha pili wajaribu kumuua mwenzao sababu ya mwanaume, Wafukuzwa shule

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Wanafunzi watatu wa shule ya upili ya wasichana ya Makueni wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Makueni kwa jaribio la kumuua mwenzao kwa kumwekea sumu kwenye chakula

Watatu hao walio na umri wa miaka 15 na wa kidato cha Pili walipanga njama ya kutumia kemikali walizoiba katika maabara ya shule ili kumwua mwenzao anayemng’ng’ania mvulana mmoja wa shule jirani ya wavulana ya makueni

Watatu waliokula njama ya kutekeleza mauaji hayo ni Beatrice Musomi, Mercy wanjiku na Purity Akinyi ilhali aliyelengwa kuuawa ni mwenzao pia aliye na umri wa miaka 15 Faustine Kivuva.

Watatu hao waliiba kemikali za phenolpthaline indicator, hydrochloric acid, benedicts solution ambapo Akinyi ndiye aliyefaa kuweka kemikali hiyo kwa chakula cha Kivuva .

Lakini njama hiyo ilitibuka wakati Ainyi aliposita kutekeleza wajibu wake na kumfanya Mercy Wanjiku kuripoti njama yao kwa kiranja wa darasa Brenda Keter ambaye baadaye alimfahamisha Naibu mwalimu mkuu Bi. Dorcas Nzioka.

Mwalimu huyo ndiye aliyeripoti tukio hilo kwa polisi kuhusiana na tukio hilo ambalo limewatamausha wanafunzi wenzao na shule nzima ya wasichana ya Makueni .


=============

WANAFUNZI watatu ambao walikuwa wakipanga kumtilia sumu mwenzao katika Shule ya Wasichana ya Makueni kuhusiana na mzozo dhidi ya mvulana walifukuzwa shuleni Jumatano, baada ya mpango wao kutibuliwa.

Wanafunzi hao wa kidato cha pili na ambao wana miaka 15 walikuwa wameshirikiana kumtilia mwenzao wa darasa hilo sumu katika chakula, baada ya kuiba kemikali katika maabara ya shule.

Hata hivyo, naibu wa mwalimu mkuu shuleni humo Dorcas Nzioka alisema kuwa mpango wao ulijulikana mnamo Alhamisi, baada yao kukosana kuhusu ni yupi angetia kemikali hiyo katika chakula.

Kulingana na kamanda wa polisi eneo la Makueni Timothy Maina, wanafunzi hao walipokosana kuhusu yupi aliyefaa kutia sumu hiyo walianza kuzomeana, mmoja wao alifahamisha kiranja kuhusu kiini cha mzozo, naye kiranja akaambia walimu.

Wanafunzi hao wanadaiwa kupanga kumtilia sumu mwenzao kama mbinu ya kumuadhibu, kwa kuchukua mpenzi wa mmoja wao. Mvulana husika ni mwanafunzi katika shule jirani ya Makueni Boys.

Bi Nzioka aliripoti kisa hicho kwa polisi, ambao walifika shuleni humo na kuwakamata wanafunzi hao.

Polisi, hata hivyo, hawakuwazuilia wanafunzi hao seli, badala yake wakiwarejesha shuleni ili waadhibiwe kulingana na sheria za shule.

Bi Nzioka jana alisema kuwa shule inashughulikia kesi hiyo, japo hakutoa maelezo zaidi kuihusu.

Hata hivyo, mtu aliye na ufahamu kuhusu jinsi kesi yenyewe inaendeshwa alifahamisha Taifa Leo kuwa usimamizi wa shule uliwatuma nyumbani wanafunzi hao. Hata hivyo, mtu huyo hakutaka kutajwa kwa kuwa haruhusiwi kutoa habari kwa vyombo vya habari.
 
Back
Top Bottom