Kenya wanatupa somo kwamba wao ni mabingwa wa demokrasia. Chebukati anatuonesha jinsi ya kusimamia uchaguzi

Mganguzi

JF-Expert Member
Aug 3, 2022
1,023
2,742
Demokrasia iliyopo Kenya kwa sasa ni darasa kubwa kwetu. Kenya wamepiga hatua kubwa sana ya kusimamia uchaguzi, na ndio faida na umuhimu wa tume huru ya uchaguzi. Kuwa na tume huru ya uchaguzi ni jambo lingine lakini pia kumpata mwenyekiti asiyegemea upande wowote ni jambo lingine. Chebukati ameonesha hilo, matokeo ya vituoni ndio main key.

Ingekuwa nchi nyingine za Afrika Mashariki tungesikia vihoja vya mabomu ya machozi na mikwara ya polisi, wizi wa masanduku ya kura na masanduku kukutwa yameshapigwa kura tayari. Rais aliye madarakani tungesikia akitoa matamko ya kutishia wakurugenzi wa halmashauri kwamba wakimtangaza mpinzani ameshinda hawana kazi tena.

Kwanini kwetu haiwezekani, ni uroho wa madaraka, asili ya uchawi na roho ya wizi au laana ya wizi? Watu hawategemei sera bali wizi. Bunge la Makinda lilikuwa tamu sana kwa sababu wabunge wa upinzani walikuwa wengi, bunge lilikuwa la kiume kwelikweli. Wakati Job Ndugai pia bunge lilikuwa la kiume kwelikweli, bila kusahau bunge la Samwel Sitta. Sasa hivi tuna bunge la upande mmoja, hayo yote ni matokeo ya kukosekana Tume Huru ya Uchaguzi.

Tuwape heshima yao wakenya na ikiwezekana twende tukajifunze, sio vibaya. Tuache uoga turuhusu watu wamenyane kwa sera na mshindi apatikane aliye halali kabisa. Uchaguzi ukiisha nitafunga safari nikapige picha na Wefula Chebukati, mwalimu wa Demokrasia Afrika Mashariki.​
 
Wewe sijui huna macho. Uchaguzi wa Kenya ulichafuliwa na Chebukati. Alijengewa nyumba ya Ksh millioni 300 na Ruto na akaruhusu Wavenezuela kudukua. Ukweli ni kuwa sheria ya uhaguzi KE ni nzuri, lakini mwenyekiti ni mbovu.
 
Back
Top Bottom