MOTOCHINI
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 27,778
- 30,748
Ukishangaa ya Mussa
Utayaona ya Kenya (ulimwengu wa pili)
SHIRIKA la kupambana na funza hapa nchini—Ahadi Kenya—Jumatano limetangaza kuwa litasambaza viatu kwa wanafunzi milioni mbili hapa Kenya.
Mradi huo utazinduliwa mwezi ujao huku watakaonufaika wakiwa ni wanafunzi katika shule za msingi za umma.
Akiongea Jumatano mjini Murang’a, Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw Stanley Kamau alisema tayari ameahidiwa viatu hivyo na wahisani mbalimbali wa hapa nchini na pia wa kutoka ng’ambo.
“Kwa vile asilimia 80 ya waathiriwa ni wale wa umri wa kwenda shuleni, watoto takriban 4 milioni wameathirika.
Tusipojitokeza kwa hali na
mali kupambana na hali hii, malengo ya masomo katika mpangilio wa milenia tunafaa tuyasahau kwa kuwa hatutayaafikia,” akasema.
Alisema hatua hiyo ni ya kuwahakikishia wanafunzi hao hali njema ya afya ili kuepukana na uvamizi wa funza ili wawe na umakinifu wa kusoma badala ya kuchukua wakati mwingi wakijikuna miwasho ya funza viungoni.
“Aidha, hata ikiwa watakaonufaika hawamo hatarini ya kuvamiwa na funza, ni wajibu wa kila Mkenya aliye na nia njema kwa maendeleo
kuwatunuku wasio na uwezo vifaa vya kuwainua kimaisha,” akasema.
Alisema kero la funza limekuwa jinamizi kubwa mashinani ya hapa nchini hasa mashuleni.
“Hili sio jinamizi ambalo limewakamba watu wa Murang’a pekee kama ilivyo dhana ya wengi. Ni kero la kitaifa ambalo hata linafaa
kutangazwa kama janga la kitaifa. Kila pembe ya nchi imeathirika,” akasema.
Alisema kwa sasa watu 5 milioni kote nchini wameathirika na janga hili.
Kuaga dunia
Alisema tayari watu 2.6 milioni wametibiwa kote nchini tangu mwaka wa 2007 huku wengine 300 kufikia Mei wakiripotiwa kuaga dunia
kufuatia uvamizi wa funza.
Bw Kamau alisema viatu hivyo vitasambazwa katika kila Kaunti ili kuwapatia afueni wahasiriwa wa janga hili.
Alipendekeza pia serikali itenge hazina ya wahasiriwa wa funza katika makadirio yake ya bajeti kupitia kwa Wizara ya Afya.
Alisema uvamizi wa wadudu hao kwa wanafunzi ni tisho kubwa la kuafikia malengo ya Milenia kuhusu masomo na pia Ruwaza ya Kiuchumi ya 2030.
Wanafunzi 2 milioni kupewa viatu kuzuia uvamizi wa funza