Mohamedy cadinaly
JF-Expert Member
- Apr 24, 2012
- 2,452
- 2,220
Wanatumiwa na mabeberuNimeangalia KTN News usiku wa leo, kweli Kenya wanafanya coverage kubwa sana kwenye msiba wa Rais Magufuli usiku kucha.
Wamebase kwenye negative tu za Rais Magufuli kiasi hakuna jema kabisa.
Kwanza wanaaminisha dunia kuwa Magufuli hajafariki kwa ugonjwa wa moyo ila ni Covid-19. Kwa station kubwa namna hii kuuaminisha dunia kuwa kafariki kwa Corona na sio Moyo kama ilivyoripotiwa na Makamu wa Rais sio jambo la kiungwana kabisa tena kwa media kubwa kama KTN.
Mahojiano yao yame-base kwa wale wakosoaji wa serekali tu na sijaona wenye +ve kuhusu serekali. Wanarudia tu speech za Magufuli ambazo zilikua na utata kama vile ng'ombe wa Kenya waliokamatwa Tanzania, mimba kwa watoto wa kike, upinzani na siasa, matumizi ya njia za uzazi wa mpango, idadi ya viongozi waliofariki kwa kuhisiwa corona.
Ikiangalia unaweza kudhani aliyefariki ni Rais wa Kenya na sio wa Tanzania maana coverage ni kubwa Kenya kuliko Tanzania. Kwa Kenya imekua kama vile furaha kwao maana wamepenyeza sana propaganda zao sana.