Kenya wana "Vetting cabinet nominees" sisi tunateuana na kuapishana tu

Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
2,400
4,073
Naangalia bunge la Kenya ni ukweli usiopingika hata kama hatuupendi wakenya wana katiba bora kabisa mara milioni kuliko katiba ya Tanzania. Sisi kila kitu ni teuzi tu.

Kenya makatibu wakuu wanaomba hiyo nafasi na kujadiliwa na kuchujwa na vyombo husika hata wananchi wanaalikwa kusema kile wanachokijua kama kimefichwa na muombaji na mwisho bunge huitimisha na kumwachia rais ateue mmoja kati ya waliopendekezwa nafasi kama za jaji mkuu,igp dci dpp sio nafasi za kupeana zinaombwa na kujadiliwa na kuchunguzwa kimaadili na vyombo husika kisha hupendekeza majina ya waliokidhi vigezo.

Ili tuwe na utawala bora na watendaji makini ni muhimu upatikanaji wa viongozi ufanyiwe mabadiliko makubwa kuna watu wana uwezo mkubwa na makini wa kufanya kazi lakini kwa mfumo wetu wa kuteuli hawawezi kupatikana ila nafasi hizo ingekuwa zinatangazwa lila mwenye sifa aombe na kuwe na utaratibu wa kuchujana nchi ingepiga hatua kubwa kimaendeleo.

Kuiga katiba ya Eenya kwenye baadhi ya mambo tusione aibu.

20221017_102646.jpg
 
Usipende kusifia kila kitu mradi tu kinafanyika kwa jirani yako wakati vipo vingi tu nchini mwako ambavyo jirani yako ndio anapaswa kujifunza kutoka kwako, unaandika na kusifia weee halafu mwisho unasema majina yanajadiliwa vizuri na vyombo husika bila kuvitaja vyombo hivyo, Sasa Nani kakwambia kuwa sisi Tanzania vyombo vya kuweza kumchunguza mtu na kumfahamu hata ya sirini havipo?

Kwani unafikiri Tanzania majina hayafanyiwi uchunguzi ufuatiliaji utafiti na mchujo wa Hali ya juu? Unafikiri watu hawachunguzwi? Unafikiri watu wanawekwa tu bila kufahamu historia zao za kitaaluma kielimu kiujuzi kiuzoefu na kimaadili? Unafikiri Tanzania Haina vyombo vya kumfuatilia mtu nyendo zake na uzalendo wake kwa Taifa letu? Au unataka wawe wanakuja kukwambia wewe kuwa tupo katika kumchunguza fulani ili tumteue kuwa IGP au DPP au CAG?

Acha mawazo ya kinyonge mbele ya mataifa jirani, acha unyonge kwa majirani, acha kujidunisha, Acha kujishusha na kujidhalilisha, acha kujiona huna thamani mbele za wenzako, acha kujidunisha, Tanzania Ni Taifa kubwa Sana lenye heshima na linaloheshimika Sana hapa Barani Afrika na Duniani kwote, Huwa hatuteteleki Wala kuteteleshwa sisi, Watanzania Ni miamba ya kila nyanja ukanda huu, Ni nchi ambayo huwezi ukaitenga Wala kuipuuza kwa lolote lile

Kama unapenda Kenya hamia huko uone Kama hutatamani kurudi haraka Sana Tanzania mahali ambapo Ni kimbilio la wanyonge waliokata Tamaa na kupoteza matumaini
 
Usipende kusifia kila kitu mradi tu kinafanyika kwa jirani yako wakati vipo vingi tu nchini mwako ambavyo jirani yako ndio anapaswa kujifunza kutoka kwako, unaandika na kusifia weee halafu mwisho unasema majina yanajadiliwa vizuri na vyombo husika bila kuvitaja vyombo hivyo, Sasa Nani kakwambia kuwa sisi Tanzania vyombo vya kuweza kumchunguza mtu na

Usipende kuwa mbishi. Unaelewa maana ya Vetting?. Bunge linamhoji waziri mmoja mmoja Kama haliridhishi linamtema. Sio huki watu wanateuana kisa alishindwa ubunge anapewa uwaziri juu na ubunge wa kuteuliwa no Vetting.

Kenya wapo juu kiuchumi na kisiasa lazima tukubali ukweli na tujifunze kwao.
 
Usipende kuwa mbishi. Unaelewa maana ya Vetting?. Bunge linamhoji waziri mmoja mmoja Kama haliridhishi linamtema. Sio huki watu wanateuana kisa alishindwa ubunge anapewa uwaziri juu na ubunge wa kuteuliwa no Vetting.

Kenya wapo juu kiuchumi na kisiasa lazima tukubali ukweli na tujifunze kwao.
Economist unamwamini Nani Kati ya mtu anayeweza kuchunguzwa vizuri na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama na Yule atakayeulizwa na wabunge pekee ambao kwa kiasi kikubwa wanakuwa hawafahamj hata undani wa mtu husika? Mara ngapi mmekuwa mkiwalalamikia wabunge wetu kuwa hawajafanya uchaguzi wa watu mliokuwa mnawataka walipoenda bungeni kuomba kura hasa kwenye ubunge wa Afrika mashariki? Mimi naviamini na Nina Imani kubwa sanaaaaaaaaaaaa na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama katika suala zima la kuwachunguza watu na kupendekeza uteuzi wao

Ninajivunia kuwa Mtanzania na ninajivunia vyombo vyetu vya usalama ambavyo vina nafasi kubwa Sana katika suala la uteuzi wa watu kulingana na sifa zao na mienendo yao
 
Sisi hatufiki hata nusu ya wakenya. Kuanzia kwenye siasa,uchumi mpaka maendeleo. Sisi tunajua kuchonga mdomo tu. Lakini mambo yote wanaachiwa akina miguru wajipigie.

Kenya katiba yao ni bora sana. Uchaguzi huu uliopita ingekuwa huku angepitishwa tu yule alietakiwa na viongozi wengi. Au wangepindua katiba kenyatta aendelee kama alivyosema yule chiz wa nchi jirani. Lakini umeona kilichotokea?. Kenya wako mbali sana wanatuachia manyoya tuendelee kuibiwa na hawa viongozi kwa katiba mbovu ya mwaka 47
 
Naangalia BUNGE la KENYA ni Ukweli usiopingika hata kama hatuupendi WAKENYA wana KATIBA BORA KABISA MARA MILIONI kuliko KATIBA ya TANZANIA.
Sisi kila kitu ni TEUZI Tu
Kenya MAKATIBU Wakuu Wanaomba hiyo Nafasi na kujadiliwa na kuchujwa na Vyombo husika hata Wananchi wanaalikwa Kusema kile wanachokijua kama kimefichwa na Muombaji na Mwisho BUNGE huitimisha na Kumwachia RAIS Ateue MMOJA kati ya Waliopendekezwa NAFASI kama za
JAJI MKUU,IGP DCI DPP sio Nafasi za Kupeana Zinaombwa na kujadiliwa na Kuchunguzwa Kimaadili na Vyombo husika kisha hupendekeza Majina ya Waliokidhi Vigezo.
Ili tuwe na UTAWALA BORA na Watendaji Makini ni Muhimu Upatikanaji wa Viongozi ufanyiwe Mabadiliko Makubwa kuna Watu wana Uwezo Mkubwa na Makini wa Kufanya kazi lakini kwa Mfumo wetu wa KUTEULI hawawezi Kupatikana ila NAFASI hizo ingekuwa Zinatangazwa lila Mwenye Sifa Aombe na kuwe na Utaratibu wa Kuchujana NCHI ingepiga Hatua kubwa KIMAENDELEO
KUIGA KATIBA ya KENYA kwenye Baadhi ya MAMBO tusione AIBUView attachment 2389877
Wakenya wapo civilized mara 1000 zaidi yetu, sisi tunaswangwa tu kama ngombe zizini - watu 6 wanachagua nani awe kiongozi wetu mkuu, na huyo tunapiga kura kumpitisha utake ama usitake, afu na yeye anachagua anaowataka - huna room ya kuuliza why and how kama unajipenda.
 
Usipende kusifia kila kitu mradi tu kinafanyika kwa jirani yako wakati vipo vingi tu nchini mwako ambavyo jirani yako ndio anapaswa kujifunza kutoka kwako, unaandika na kusifia weee halafu mwisho unasema majina yanajadiliwa vizuri na vyombo husika bila kuvitaja vyombo hivyo, Sasa Nani kakwambia kuwa sisi Tanzania vyombo vya kuweza kumchunguza mtu na kumfahamu hata ya sirini havipo? Kwani unafikiri Tanzania majina hayafanyiwi uchunguzi ufuatiliaji utafiti na mchujo wa Hali ya juu? Unafikiri watu hawachunguzwi? Unafikiri watu wanawekwa tu bila kufahamu historia zao za kitaaluma kielimu kiujuzi kiuzoefu na kimaadili? Unafikiri Tanzania Haina vyombo vya kumfuatilia mtu nyendo zake na uzalendo wake kwa Taifa letu? Au unataka wawe wanakuja kukwambia wewe kuwa tupo katika kumchunguza fulani ili tumteue kuwa IGP au DPP au CAG?

Acha mawazo ya kinyonge mbele ya mataifa jirani, acha unyonge kwa majirani, acha kujidunisha, Acha kujishusha na kujidhalilisha, acha kujiona huna thamani mbele za wenzako, acha kujidunisha, Tanzania Ni Taifa kubwa Sana lenye heshima na linaloheshimika Sana hapa Barani Afrika na Duniani kwote, Huwa hatuteteleki Wala kuteteleshwa sisi, Watanzania Ni miamba ya kila nyanja ukanda huu, Ni nchi ambayo huwezi ukaitenga Wala kuipuuza kwa lolote lile

Kama unapenda Kenya hamia huko uone Kama hutatamani kurudi haraka Sana Tanzania mahali ambapo Ni kimbilio la wanyonge waliokata Tamaa na kupoteza matumaini

Kenya ni best kuliko sisi, hapa majizi ya kura yanateuana ili kulinda madaraka wanayoyapata kihuni. Matokeo yake mfumo huu umezalisha chawa kibao wa kusifia viongozi ili wapate vyeo. Kenya hawana lolote la kujifunza kutoka kwetu kuhusu demokrasia na utawala bora. Kenya anayepata madaraka anayapata kwa uwezo wake na sio mbeleko.
 
Kenya ni best kuliko sisi, hapa majizi ya kura yanateuana ili kulinda madaraka wanayoyapata kihuni. Matokeo yake mfumo huu umezalisha chawa kibao wa kusifia viongozi ili wapate vyeo. Kenya hawana lolote la kujifunza kutoka kwetu kuhusu demokrasia na utawala bora. Kenya anayepata madaraka anayapata kwa uwezo wake na sio mbeleko.
Kwani sisi Ni wakabila Kama Kenya?
 
Kwani sisi Ni wakabila Kama Kenya?

Hiyo sifa ya kutokuwa na ukabila ni sifa ya kijinga na wala haihusiani na mada husika kuhusu utawala bora. Hiki chama cha kizee kinachohodhi madaraka kwa shuruti lazima kitoke kwa machafuko, kisha tujenge mfumo madhubuti wa kutokujuana bali kujali uwezo. Wakenya pamoja na ukabila wao hawana upendeleo wa kijinga kama huu unaoletwa na ccm.
 
Back
Top Bottom