Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Wahadhiri hao wanalenga kushinikiza Serikali kutoa Sh5.2 bilioni za kugharamia nyongeza ya mishahara yao.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wahadhiri UASU Constantine Wasonga, alisema mgomo huo ulianza rasmi jana saa nane mchana.
Dkt. Wasonga alisema mgomo huo unatokana na hatua ya Serikali ya kukataa kutekeleza mkataba wa maelewano kuhusu nyongeza ya mishahara (CBA) wa 2013 - 2017.
"Tumeagiza Wahadhiri wa vyuo 31 vya umma kote nchini wasuse kazi na kujiunga na mgomo ambao ndio njia pekee inayoelewa Serikali", alisema Dkt. Wasonga jana baada ya Baraza Kuu la Uasu kukutana jijini Nairobi.
Alisema Serikali iliahidi kuwaongezea mishahara lakini kufikia sasa haijatimiza ahadi hiyo wala kuwasiliana na viongozi wa chama cha Uasu.