Kenya: Vyama vya Upinzani vyatangaza kuungana, umati Mkubwa usiopimika

Profesa

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
905
624
Hawa ni wanachama wa CHADEMA, TLP, NCCR mageuzi, DP, NLD n.k.? Hapana, Msiba? Hapana! Hapa ni Kenya, vyama vya siasa na wanachama wao wameungana na wanaunda aliance. tatizo ni nini hapa kwetu? Kama si ulafi, uroho na ubinafsi uliopindukia wa viongozi wasiotaka mabadiliko ya nchi bali mabadiliko yao? Kila mtu anataka kuwa Raisi anaenda kufanya nini kule? hapa tunataka chama chenye sera nzuri ili hata wakibadili raisi bado sera zinatupeleka tunapotaka. Cheki hapa, ni live kwa sasa tunapoongea. Wanasiasa Tanzania mnajifunza nini hapa?

Photo0111.jpg
 

Attachments

  • Photo0110.jpg
    Photo0110.jpg
    219.3 KB · Views: 229
Hivi unajua kwa nini hiki kinaitwa cdm,hiki cuf na hiki nccr-mageuzi?. Unaweza unganisha walokole na waislamu katika ibada? Au una weza unganisha katoliki na waislamu katika ibada? Ukiona vyama vinaungana ujue kimoja hakipo kati ya vile vilivyoungana.
 
Hiko ni Kimbunga cha UHURUTO ambacho kinataka kumvaa Odinga, Peter Steven na wengine.

Vyama havijaungana ni muungano tu wa kutaka Urais. Uhuru Kenyata anagombania urais na mgombea mwenza ni RUTO.
 
Hivi unajua kwa nini hiki kinaitwa cdm,hiki cuf na hiki nccr-mageuzi?. Unaweza unganisha walokole na waislamu katika ibada? Au una weza unganisha katoliki na waislamu katika ibada? Ukiona vyama vinaungana ujue kimoja hakipo kati ya vile vilivyoungana.

tofautisha imani za dini na siasa....kama sera na mitazamo ya chama ina malengo yanayofanana muungano unawezekana
 
tofautisha imani za dini na siasa....kama sera na mitazamo ya chama ina malengo yanayofanana muungano unawezekana
mkuu ushirikiano nakubali na si muungano, hivi kwa mfano ccm waungane na cdm wakati falsafa zao ni tofauti? Mara nyingi muungano wa vyama vya siasa ni tamaa za madaraka za viongozi na ndo maana mbele ni giza.
 
Hiko ni Kimbunga cha UHURUTO ambacho kinataka kumvaa Odinga, Peter Steven na wengine.

Vyama havijaungana ni muungano tu wa kutaka Urais. Uhuru Kenyata anagombania urais na mgombea mwenza ni RUTO.
Kweli kabisa. Kilichowaunganisha hawa si dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi, bali dhamira za kibinafsi za kutaka uongozi
 
Katiba ya Kenya inaruhusu Muungano wa vyama katika kumsimamisha mgombea wa URAIS na Makamu wake. Katiba ya Tanzania hairuhusu muungano wa vyama kumsimamisha mgombea mmoja wa URAIS na Makamu wake. Ndiyo maana Uhuru Kenyata anagombea kiti cha URAIS wakati Ruto anakuwa mgombea mwenza wake, ingawa wanatoka vyama tofauti. Tanzania hii haiwezekani, mathalani Dr. Slaa (CDM) agombee kiti cha Urais halafu running mate awe Shariff Hamad (CUF). Katiba ya Tanzania inakataza hili lazima watoke chama kimoja.

Lakini kulingana pia geopolitics za Tanzania si washauri CDM kufanya ushrikiano/muungano na Chama chochote cha upinzani because vyama vya upinzani ACTIVE i.e CUF na NCCR-Mageuzi tayari vina ushirikiano na CCM chama tawala. Vyama vingine vya upinzani vilivyobaki ni almost vyama MFU.
 
Sasa Mkuu Profesa .. unajiandaa kufanya kazi kwenye Magazeti ya udaku nini

Hicho kichwa cha Habari yako si ungesema tu vyama vimeungana huko Kenya! ... wewe unatulazimisha tufungue habari yako ... kumbe ni habari ya Kenya!
 
Hivi unajua kwa nini hiki kinaitwa cdm,hiki cuf na hiki nccr-mageuzi?. Unaweza unganisha walokole na waislamu katika ibada? Au una weza unganisha katoliki na waislamu katika ibada? Ukiona vyama vinaungana ujue kimoja hakipo kati ya vile vilivyoungana.

Tatizo la Tanzania siyo imani ya kivyama. Ukitazama kwa makini na kwa undani tofauti za kiitikadi ni ndogo. Tatizo letu ni kwamba katiba haitoi fursa kwa vyama kugawana nafasi za madaraka pindi matokeo ya uchaguzi yakitoka.
 
Kutoungana kwa vyama vyetu ni by design and in favour of the ruling party, sheria ya vyama vya siasa na sheria ya uchaguzi zinavibana kwa namna flani vyama vyetu kuungana.
 
Siasa za Kenya ni tofauti kidogo na hapa nyumbani. Hata mazingira yao na sheria ni tofauti, hivyo haiwezi kuwa cut & paste.

Ila kuna mambo mazuri tunayoweza kuyachuja na kuyatumia hapa. Mfano mmoja ni kuwa watu/wananchi huwafuata watu (wanasiasa) zaidi ya itikadi za vyama. Ni wazi hili ni jambo tunaloliona hapa Afrika lakini mara nyingi sio zuri. Kwa sababu iwe mbunge au rais SERA, UTAIFA, ITIKADI na u-TASISI vinapata nafasi stahiki. Lakini ktk siasa za Kenya mwanasiasa ni vyote hivyo!
 
tayari naiona hoja muhimu ya mabadiliko ya kikatiba ambayo inatoa flexibility hasa pale ambapo upepo unakuwa sio, umuhimu wa kutoa mwanya kwa vyama kuungana uko wazi. shida ni ukomavu wa vyama, kasoro moja kubwa ya vyama vya Kenya ni kuundwa kwake ambapo chama kinaundwa muda mfupi kabla ya kampeni za uchguzi na inakubalika, haijalishi chama hicho kimekomaa au kimekuwepo kwenye harakati kwa muda gani, muhimu ni kuwa anaekiongoza ana washabiki kiasi gani. So ukiweza kujikusanyiwa wafuasi wengi unajiweka kwenye nafasi nuri ya kuitwa kwenye big aliances, hata kama hutashinda uchaguzi, ila nafasi yako ya uwaziri au unaibu huwezi ikosa kirahisi, kwa kutumia kura zako.
 
Mkubwa usitoke povu bado Kenya sio mfano sahihi kabisa kwa muungano wa vyama vya siasa. Manake kuna force nyingi inayolazimisha hayo yatokee huko na ukabila ndio msukumo mkubwa, Kenya hawako tayari kuona mjaluo anaongoza nchi wakati USA wameona sio tatizo Kenya wanaona tatizo.

Mtoa mada wape taarifa sahihi wachangiaji kuliko kuwapotosha na wataona hakuna kitu inafanyika bongo na nje ndio wakopoa. UHURUTO wanakesi iko mahakamani na lazima washike dola kujinasua kutokana na issue zao za ukabila katika chaguzi iliyopita.

Kama kweli mnahamasisha watu wabadilike kwa ajili ya mabadiliko basi Raila amepigania sana mabadiliko na kabila lake ndio limemghalimu kiukweli ni mwanaharakati wa mfano. Sema ameundiwa zengwe la uzee sasa hivi na vijana ndio wanataka kushika hatamu ila kabila moja limeongoza kwa miaka 70 kenya na linataka kuendelea kuongoza.

Bora bongo waiungane kuliko kuiga yanayotokea Kenya sio mfano sahihi.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom