Kenya- Uasi Bado Waendelea...

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,254
Naona majirani zetu mambo bambo kutulia. Kwa hivi karibuni, walijitokeza Mungiki, kisha uasi mkubwa baada ya matokeo ya uchaguzi, sasa kuna huu mwingine...habari zaidi hapa chini...


Waasi waibuka Kenya

Andrew Msechu na Mashirika ya Habari
Posted Date::3/13/2008

WATU wanane zaidi wameuawa katika wilaya za Laikipia na Narok, nchini Kenya kufuatia mashambulizi ya waasi wenye silaha yaliyofanyika juzi usiku.


Mauaji hayo pamoja na uchomaji wa nyumba vimeendelea, huku mamia ya wakazi wa wilaya hizo zinazozunguka Mlima Elgon, wakiendelea kukimbia makazi yao, ili kuwapisha askari polisi na askari wa jeshi la ulinzi wanaofanya operesheni maalum ya kuwasaka wanamgambo hao.


Vikosi hivyo vya usalama vilisema kuwa, wanamgambo hao waliojiwekea ngome zao kwenye maeneo ya misitu minene inayozunguka Mlima Elgon, wameainishwa kuwa ni wa vikosi vya wapiganaji wa Sabaot Land Defence Force, Moorland Forces na The Political Revenge Movement.


Mkuu wa Wilaya ya Laikipia, Julius Mutula alikaririwa na Gazeti la The Standard jana akisema kuwa, watu hao wenye silaha wamekuwa wakivamia watu katika makazi yao na kuwaua kwa kuwapiga risasi, lakini vyombo vya dola vimekuwa vikifanya kazi ya kuwatafuta waasi hao.


Mauaji hayo ambayo chanzo chake hakijajulikana, yametokea huku wananchi wa Kenya wakiwa katika juhudi za kutafuta njia ya kuponya majeraha yaliyotokana na machafuko yaliyoibuka mara baada ya Uchaguzi Mkuu wa Desemba 27, mwaka jana nchini humo, yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 1,200.


Mbunge wa Laikipia, Ndiritu Muriithi alivilaumu vyombo vya usalama nchini humo, kutokana na kutokuwa makini katika kushughulikia tatizo hilo, huku idadi ya vifo na uchomaji wa nyumba ukiongezeka kila siku katika eneo hilo.


Watu zaidi ya 15 wameripotiwa kuuawa katika siku tatu zilizopita na nyumba kadhaa zimechomwa moto katika maeneo hayo.


Muriithi aliliambia Gazeti la The Nation la Kenya kuwa, zipo taarifa zisizo rasmi kwamba watu hao wanaojificha katika misitu inayozunguka Mlima Elgon, wamekuwa wakikimbilia eneo la mpaka wa nchi hiyo na Uganda na kuna madai kuwa, sababu za maauji hayo ni visasi vinavyotokana na chuki za kikabila kutokana na wizi wa mifugo.


Katika eneo la Narok, zaidi ya watu wanne wameripotiwa kuuawa kufikia jana, nyumba 125 kuchomwa moto, baada ya kutokea kutoelewana kwa watu wa jamii ya Munyas.


Hata hivyo, askari walioanza operesheni hiyo tangu juzi katika eneo hilo la Mlima Elgon, walikaririwa wakisema kuwa tayari wameshawakamata washukiwa 30 wanaodhaniwa kuwa washiriki wa vikosi hivyo vya waasi.


Washukiwa hao walidaiwa kuwa walikuwa wakijificha katika misitu na mapango yaliyopo kwenye eneo la Mlima Elgon, lakini kutokana na helikopta na magari ya kijeshi yanayotumika kuwatafuta mashambulizi yamepungua.


Wakati huo huo, viongozi wakuu wa Serikali na ODM, wameungana na kuunda kamati maalum ya kushughulikia masuala ya Bunge la nchi hiyo.


Viongozi hao waliopo kwenye kamati hiyo yenye uwiano wa idadi sawa kutoka kila upande, wanajumuisha Makamuwa Rais, Kalonzo Musyoka na Raila Odinga wa PNU.


Hatua hiyo ilifikiwa baada ya mjadala mzito juu ya namna kamati hiyo ya watu 20 itakavyoundwa, uliopozwa na hatua ya Musyoka kuwasilisha majina hayo baadaye. Kamati hiyo ndiyo inayotarajiwa kuweka taratibu za uendeshaji wa kikao kizima cha Bunge hilo.


Wanasiasa maarufu walioungana baada ya kuteuliwa kuunda kamati hiyo kutoka upande wa PNU ni Martha Karua, Profesa George Saitoti, Amos Kimunya, Uhuru Kenyatta, Kiraitu Murungi, Henry Kosgey na Mutula Kilonzo. Pia yumo Moses Wetangula.


Kwa upande wa ODM ni William Ruto, Charity Ngilu, Profesa Anyang� Nyong�o na Najib Balala ambao wameungana na wabunge wengine katika kuunda kamati hiyo.


Wengine ni Kiraitu Murungi, George Thuo, Omingo Magara, Jakoyo Midiwo, Adan Keynan na Ali Mohammed Mohamud.


Tayari Waziri wa Sheria wa Kenya, Martha Karua alishatangaza miswada miwili yenye nia ya kuwahalalisha kisheria Waziri Mkuu na naibu mawaziri wake wawili.

Source: Mwananchi.co.tz


61 Kenyan militia members held
13/03/2008 09:57 - (SA)


Eldoret - Security forces have arrested 61 suspected members of a tribal militia in western Kenya just days after the army launched a massive crackdown on the group, said a local official on Wednesday.

"We have arrested 61 people who were trying to escape to other districts neighbouring Mont Elgon because they were acting in suspicious manners," said Western Provincial Commissioner Abdul Mwasera.

On Sunday, Kenya's army launched a major crackdown on the rag-tag Sabaot Land Defence Force (SDLF) militia, accused by police of killing at least 500 people in the past year alone and displacing thousands of others.

Last week, the SDLF attacked a village in the area and killed 15 people, hacking, shooting and burning them to death.

100 people arrested

The government had imposed a dusk-to-dawn curfew for the Mount Elgon region, located some 300km northwest of Nairobi.

Although Mwasera said he was unaware of any victims in the crackdown, local residents said one person was killed at a school on Tuesday evening, where security forces arrested roughly 100 people.

The forces also prevented a number of Kenyan journalists from covering their operations on the ground, confiscating some of their work material.

The SLDF was demanding the annulment of a government settlement scheme, which it deemed unfair because it displaced the small Sabaot tribes from their ancestral land.

The group intensified attacks in 2006 and killed several villagers and destroyed homes in the fertile Mount Elgon region near the border with Uganda.

The violence in the flashpoint area was not directly linked to the turmoil that erupted after Kenya's disputed December elections, but tribal and land disputes had been exacerbated in recent weeks.

Source: News24.com


SteveD.
 
Religious groups and human rights activists Tuesday piled pressure on President Kibaki and ODM leader Raila Odinga to name a clean and lean Cabinet immediately.
In Nairobi, over 100 placard-carrying lobbyists were tear-gassed and dispersed by police as they tried to gather to press for a Cabinet of 24 or less members...MORE SCENES!!!
 
Huo ni mtihani mkubwa sana kwa Kibaki na ndiyo maana anaendelea kuomba ODM wakubali angalau baraza liwe zaidi ya 34 lakini si zaidi ya 40.

PNU ina vyama washirika vingi na lazima angalau kila chama kiwe na mtu mmoja ambaye atateuliwa kuingia kwenye cabinet. Zaidi ya hilo pia lazima kuwe na balance ya uwakilishi kwa kuangalia mikoa waliyotoka. Tatizo ni namna gani ataanza ku-balance? Ndiyo maana akina Karua na Mungatana wanaanza kuomba nafasi zaidi kupitia NARK-K. DP nao watakuja na same requests, akina Kombo nao wanategemea wapewe japo nafasi moja, KANU na ODM-K nao wanategemea wapewe mgao wao. Hapa ndipo nadharia ya kisungura cha Lowassa inapotumika na kuonyesha kwamba huwezi kukigawa kisungura na kila mtu akaridhika.

Swali je hizo nafasi 17 zinatosha kuzigawa kwa vyama vyote na mikoa yote ili iweze ku-reflect ushirikiano wao? Kama ingekuwa ni serikali ya Kibaki peke yake ingekuwa rahisi sana.

Niliwahi kusema kwamba vyama shiriki vilivyom-support Kibaki havikuona mbali sana, sasa ndio itakuwa wazi kwenye mgao wa cabinet slots watakapogundua kwamba hivyo vyama vilitumika kumwongezea kura Kibaki na hivyo kupunguza kazi ya kuiba kura na akafanikiwa kuingia Ikulu kwa mbinde.

Yangu macho .... ngoja nione hatima ya PNU!
 
Keil,

The issue is delivery of services na sio kugawa viti
as a means of saying thank you to his allies.Hapo ndipo
panakoseka tu maana kila mtu anaangalia maslahi yake not
thiinking that this is about public service...kwani what is
the problem with Kibaki not giving out these seats?...hao wapambe wake need to realise that the cake is smaller now
that ODM has been invited to the party!!
 
Realy Kenya ni problem.hivi wakianza tena sijui nani atakwenda kusuluhisha.Muafaka wao unatoa harufu mbaya sijui wenzangu mnaonaje.

Ahadi ni deni ndio kinacho msumbua Kibaki.Kazi kwako mwana wane
 
Realy Kenya ni problem.hivi wakianza tena sijui nani atakwenda kusuluhisha.Muafaka wao unatoa harufu mbaya sijui wenzangu mnaonaje.

Ahadi ni deni ndio kinacho msumbua Kibaki.Kazi kwako mwana wane

Kibaki anataka kujitia eti amesahu kua alitia sahihi mbele
ya ulimwengu mzima...ana ile kitu inaitwa selective amnesia.
Fujo likianza tena I don't see people going back there kama
ilivyokua awali...as a matter of fact sasa radar zinalenga
kwa Mugabe...Kenyans better be careful maana the goodwill came
once...all that is remaining ni for wao wenyewe kumaliza
shughuli!
 
Nakumbuka maneno ya Kitila, Wakenya wanapenda sana madaraka. Yaani kila mtu anataka kuwa waziri.

Hapo wanachopigania ni ni uwaziri tu na wala sio Wakenya.
 
Nakumbuka maneno ya Kitila, Wakenya wanapenda sana madaraka. Yaani kila mtu anataka kuwa waziri.

Hapo wanachopigania ni ni uwaziri tu na wala sio Wakenya.



Ni kweli Wakenya wanapenda sana madaraka. Mfano huyu Waziri mkuu mtarajiwa yupo tayari wakenya wafe wengi zaidi ili tu aingie madarakani.
 
Swali hapa ni je Mungiki nd'o walimbwaga ama ni serikali?

Mungiki Leader’s Wife Executed

Published on April 12, 2008, 12:00 am

By Cyrus Ombati


The wife and driver of Mungiki national chairman, Maina Njenga, have been murdered and their bodies dumped in a forest.
Mrs Njenga and her driver were found murdered and thrown in Gakoye Forest,Gatundu, after they went missing in Nairobi, on Tuesday.
The bodies of Virginia Nyakio, and the driver, George Njoroge, were found dumped in Gakoe Forest in Gatundu on Wednesday, a day after their abduction.
The mutilated bodies had deep cuts in the head, neck and other parts of the body when they were discovered alongside two other decaying bodies.
Police brought them to the City Mortuary and booked them as unknown...UKITAKA MAELEZO ZAIDI
 
Ijapokua Raila na Mzee Kubaka wameelewana katika maswala ya
uundaji wa baraza la mawaziri, huku nje hawa mabwana wa Mungiki bado wanaleta zegere.Nairobi was at a standstill yesterday na miji kama Naivasha na Nakuru pia ilikua affected!

A night of terror as Mungiki raid homes
--------------------------------------------------------------------------------

Published on April 15, 2008, 12:00 am

By Amos Kareithi, Evelyne Ogutu and Mutinda Mwanzia

Hundreds of Mungiki members staged night raids in Gatundu and Thika districts, leaving a trail of bloodshed and destruction.
The men, wielding G3 rifles and teargas canisters, attacked with military precision, killing three people.
Residents told of a night of terror as Mungiki gangs engaged police in running battles.
Ms Damaris Waithera, a resident, said: "I was woken up by bursts of gunfire. Then I heard people running near my house. I was too terrified to venture out … then the groans."
What scared her most was when she heard an enraged gangster say: "Nimwamugutha ngui ici. Nainyui ni mugwitikia turi arume (You have hit him. You will know that we, too, are men).The woman said the man who had allegedly been stabbed fell near her doorstep, groaned for some time and then died.

nh_150408_01.jpg

Police officers flush out a man from a house during the search for Mungiki members in Dandora, Nairobi, yesterday. Picture by Jonah Onyango

Two other men were killed a few metres away, where dried blood was visible despite the heavy downpour.
Near where the two men had fallen, two poles lay across the road, a crude barricade near a heap of smouldering tyres throughout the morning.
"I was woken by cat calls and whistles. The first burst of gunfire was at 3.45am, followed by ceaseless shooting," said a witness at Nyamarigu village.
The man, too scared to give his name, said when he went out of his house, he was ordered to go back.
"We do not want you to die... These things do not concern you," the resident was told.
Other witnesses recalled that a milk vendor fled after he was confronted by the youths at the roadblock. He abandoned his vehicle and took cover in a nearby farm.
Hours later, the vehicle was found in a church compound with everything intact.
The Gatundu DC, Mr Dan Mesis, said: "We did not know that such attacks were in store."
He added: "We do not know whether they are Mungiki, but we are investigating."
He explained that the group was organised and struck simultaneously at dawn.
The DC said bodies of the victims were taken to the City Mortuary because the local one was small.
Villagers said some people were warned on Sunday night.
In Thika, the situation was different as the attacks had been anticipated and were thwarted at Kiandutu and Kiang'ombe slums.
Thika DC, Mr John Litunda, said: "They burnt two matatus at the Thika bus park. There was commotion in town and businesses closed."
Meanwhile, travellers were stranded for hours when Mungiki barricaded the busy Kangundo-Nairobi road.
They lit bonfires and erected barriers on the road as early as 5.30am near Ruai and Njiru trading centres.
Commuters were huddled in groups discussing the events of the morning.
Matatus plying the Kangundo route suspended their trips to Nairobi for nearly five hours before officers intervened.
The officers helped put out the fires and removed boulders from the road.
By 9am, matatus had begun business on the route via Jogoo Road to the city. They were, however, very cautious.
Commuters from Komarock, Kayole, Saika and Umoja I estates were hard hit by the mayhem.
Some matatus took advantage of the situation and increased fare.

__________________
 
Wakuu mnaona vile mgambo wa Kenya walivyo sop-sop!!..LOL!
"Arrooo arfonso kucha hapaa!!!"
 
Nakumbuka maneno ya hayati mwalimu Nyerere, kuhusiana na nchi jirani zinazo tuzunguka... Kama hatutoshiriki kuwapatia amani basi hata sisi pia tutaathirika kwa namna moja au nyingine.

Nasikia Askari wa JWTZ wamefanikisha kukikomboa kisiwa cha Anjuan kule Comoro.

Je Tanzania kwa uwezo wake wa kijeshi hivi hawawezi kweli kwenda kutuliza fujo na ikwezekana tukae kule japo kwa miaka miwili mitatu hivi sina niya ya Tanzania itawale Kenya lakini ni katika kuwasaidia ndugu zetu hawa, kama vile tunavyo wasaidia Wakomoro, Warundi na vijinchi vingine vinavyo tuzunguka....

Ni mtazamo tu wa maoni...!
 
Back
Top Bottom