Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,241
Naona majirani zetu mambo bambo kutulia. Kwa hivi karibuni, walijitokeza Mungiki, kisha uasi mkubwa baada ya matokeo ya uchaguzi, sasa kuna huu mwingine...habari zaidi hapa chini...
SteveD.
Source: Mwananchi.co.tz
Waasi waibuka Kenya
Andrew Msechu na Mashirika ya Habari
Posted Date::3/13/2008
WATU wanane zaidi wameuawa katika wilaya za Laikipia na Narok, nchini Kenya kufuatia mashambulizi ya waasi wenye silaha yaliyofanyika juzi usiku.
Mauaji hayo pamoja na uchomaji wa nyumba vimeendelea, huku mamia ya wakazi wa wilaya hizo zinazozunguka Mlima Elgon, wakiendelea kukimbia makazi yao, ili kuwapisha askari polisi na askari wa jeshi la ulinzi wanaofanya operesheni maalum ya kuwasaka wanamgambo hao.
Vikosi hivyo vya usalama vilisema kuwa, wanamgambo hao waliojiwekea ngome zao kwenye maeneo ya misitu minene inayozunguka Mlima Elgon, wameainishwa kuwa ni wa vikosi vya wapiganaji wa Sabaot Land Defence Force, Moorland Forces na The Political Revenge Movement.
Mkuu wa Wilaya ya Laikipia, Julius Mutula alikaririwa na Gazeti la The Standard jana akisema kuwa, watu hao wenye silaha wamekuwa wakivamia watu katika makazi yao na kuwaua kwa kuwapiga risasi, lakini vyombo vya dola vimekuwa vikifanya kazi ya kuwatafuta waasi hao.
Mauaji hayo ambayo chanzo chake hakijajulikana, yametokea huku wananchi wa Kenya wakiwa katika juhudi za kutafuta njia ya kuponya majeraha yaliyotokana na machafuko yaliyoibuka mara baada ya Uchaguzi Mkuu wa Desemba 27, mwaka jana nchini humo, yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 1,200.
Mbunge wa Laikipia, Ndiritu Muriithi alivilaumu vyombo vya usalama nchini humo, kutokana na kutokuwa makini katika kushughulikia tatizo hilo, huku idadi ya vifo na uchomaji wa nyumba ukiongezeka kila siku katika eneo hilo.
Watu zaidi ya 15 wameripotiwa kuuawa katika siku tatu zilizopita na nyumba kadhaa zimechomwa moto katika maeneo hayo.
Muriithi aliliambia Gazeti la The Nation la Kenya kuwa, zipo taarifa zisizo rasmi kwamba watu hao wanaojificha katika misitu inayozunguka Mlima Elgon, wamekuwa wakikimbilia eneo la mpaka wa nchi hiyo na Uganda na kuna madai kuwa, sababu za maauji hayo ni visasi vinavyotokana na chuki za kikabila kutokana na wizi wa mifugo.
Katika eneo la Narok, zaidi ya watu wanne wameripotiwa kuuawa kufikia jana, nyumba 125 kuchomwa moto, baada ya kutokea kutoelewana kwa watu wa jamii ya Munyas.
Hata hivyo, askari walioanza operesheni hiyo tangu juzi katika eneo hilo la Mlima Elgon, walikaririwa wakisema kuwa tayari wameshawakamata washukiwa 30 wanaodhaniwa kuwa washiriki wa vikosi hivyo vya waasi.
Washukiwa hao walidaiwa kuwa walikuwa wakijificha katika misitu na mapango yaliyopo kwenye eneo la Mlima Elgon, lakini kutokana na helikopta na magari ya kijeshi yanayotumika kuwatafuta mashambulizi yamepungua.
Wakati huo huo, viongozi wakuu wa Serikali na ODM, wameungana na kuunda kamati maalum ya kushughulikia masuala ya Bunge la nchi hiyo.
Viongozi hao waliopo kwenye kamati hiyo yenye uwiano wa idadi sawa kutoka kila upande, wanajumuisha Makamuwa Rais, Kalonzo Musyoka na Raila Odinga wa PNU.
Hatua hiyo ilifikiwa baada ya mjadala mzito juu ya namna kamati hiyo ya watu 20 itakavyoundwa, uliopozwa na hatua ya Musyoka kuwasilisha majina hayo baadaye. Kamati hiyo ndiyo inayotarajiwa kuweka taratibu za uendeshaji wa kikao kizima cha Bunge hilo.
Wanasiasa maarufu walioungana baada ya kuteuliwa kuunda kamati hiyo kutoka upande wa PNU ni Martha Karua, Profesa George Saitoti, Amos Kimunya, Uhuru Kenyatta, Kiraitu Murungi, Henry Kosgey na Mutula Kilonzo. Pia yumo Moses Wetangula.
Kwa upande wa ODM ni William Ruto, Charity Ngilu, Profesa Anyang� Nyong�o na Najib Balala ambao wameungana na wabunge wengine katika kuunda kamati hiyo.
Wengine ni Kiraitu Murungi, George Thuo, Omingo Magara, Jakoyo Midiwo, Adan Keynan na Ali Mohammed Mohamud.
Tayari Waziri wa Sheria wa Kenya, Martha Karua alishatangaza miswada miwili yenye nia ya kuwahalalisha kisheria Waziri Mkuu na naibu mawaziri wake wawili.
Source: News24.com
61 Kenyan militia members held
13/03/2008 09:57 - (SA)
Eldoret - Security forces have arrested 61 suspected members of a tribal militia in western Kenya just days after the army launched a massive crackdown on the group, said a local official on Wednesday.
"We have arrested 61 people who were trying to escape to other districts neighbouring Mont Elgon because they were acting in suspicious manners," said Western Provincial Commissioner Abdul Mwasera.
On Sunday, Kenya's army launched a major crackdown on the rag-tag Sabaot Land Defence Force (SDLF) militia, accused by police of killing at least 500 people in the past year alone and displacing thousands of others.
Last week, the SDLF attacked a village in the area and killed 15 people, hacking, shooting and burning them to death.
100 people arrested
The government had imposed a dusk-to-dawn curfew for the Mount Elgon region, located some 300km northwest of Nairobi.
Although Mwasera said he was unaware of any victims in the crackdown, local residents said one person was killed at a school on Tuesday evening, where security forces arrested roughly 100 people.
The forces also prevented a number of Kenyan journalists from covering their operations on the ground, confiscating some of their work material.
The SLDF was demanding the annulment of a government settlement scheme, which it deemed unfair because it displaced the small Sabaot tribes from their ancestral land.
The group intensified attacks in 2006 and killed several villagers and destroyed homes in the fertile Mount Elgon region near the border with Uganda.
The violence in the flashpoint area was not directly linked to the turmoil that erupted after Kenya's disputed December elections, but tribal and land disputes had been exacerbated in recent weeks.
SteveD.