Kenya tops again, ranked the second best investment destination in Africa

Hii inawezekana na ni ukweli kutokana na ujenzi wa miundombinu bora iliyojengwa na kibaki na waasisi wengine. Kwa sasa projects za Uhuru faida zake hazionekani ila zitakuja kuonenaka.
Kwa upande wa Tanzania, mambo kwa sasa sio kama media inavyosema. Tukirudi katika uhalisia, kipindi cha magufuli pesa ilikuwa ngumu sana kupatikana kutokana na serikali iliamua kupunguza mzunguko wa pesa. Hili lilisababisha wananchi kuitafuta pesa kwa jasho, shidaaaah ila serikali ilijaza acc zake n kuweza kuwekeza maridadi kwenye miundombinu amazing. Ninachojua ipo siku miundombinu mingi ya magufuli itaanza kudhalisha faida angalau kwa wastani wa asilimia 60 tu. Mzunguko wa pesa utapoongezwa kutokana na mifuko ya serikali kujaa, hapo ndipo Kenya mtajua kuwa maendeleo ni miundombinu bora. Wacha tuwekeze ila wakati wetu utapofika, kila mtu atajua baba wa ukanda wetu ni nani, mama wa ukanda wetu ni nani. Muda haudanganyi. Nyie endeleeni kuibeza miradi yetu, juhudi za raisi wetu n taifa letu kwa ujumla. Kwa tunaoviona jinsi vitu vilivyo kwa ground, surely tumerelaaaaaaaaax, tunajua wakati wetu unafika tu.

Narudia tena, kinachowaponza ni katiba, kwamba kwenu huko rais anaamua ujenzi upi anaupa kipau mbele, tumeona hata kwenye kampeni zake anasema wazi bila kuficha kwamba huwa ananyima maeneo ya upinzani maendeleo, sisi kwetu hapa maendeleo yote haya yapo kikatiba zaidi kwa mujibu wa ruwaza ya 2030, kila kiongozi awe wa upinzani au wa serikali hujinadi namna gani atatekeleza hiyo ruwaza.

Kila barabara, reli na vyote vipo kwenye ruwaza, akija rais mpya atalazimika kukomaa nayo, leo hii kuna ujenzi unaendelea tena mambo makubwa na hauskii tukilia kubanwa kwenye mzunguko wa hela maana uandishi wa hii ruwaza uliandaliwa kwa utaalam mkubwa, nyie huko rais ghafla bila kuomba ushauri ananunua mindege kwa pesa taslim na kusabaisha ukata mkubwa vijijini na mitaani.

Mjifunze kuhusisha wataalam wa masuala ya uchumi, acheni hulka ya kukurupuka.
 
Huyo jamaa atawapa tabu sana, ndio mara ya kwanza kuona CCM mumekabwaa kooni kihivi, jamaa alikaidi marisasi, mumezuia wapinzani kufanya mikutano kwa miaka miine, sasa siku hizi chache bado mnawabana, ila Lissu akishindwa nahisi upinzani utafutwa kabisa, uchaguzi wenu ni full maigizo tu, yaani hata mkuu wa polisi anamwambia Mbowe bila aibu kwamba hawezi kumshinda jamaa wa CCM.
Eti mara ya kwanza, unazuga humjui lowasa wa 2015, na ulivyokuwa unamshabikia.
Huyu nae anaishia kama lowasa, tena mwaka huu ndio mteremko
 
Eti mara ya kwanza, unazuga humjui lowasa wa 2015, na ulivyokuwa unamshabikia.
Huyu nae anaishia kama lowasa, tena mwaka huu ndio mteremko

Lowassa yule mzee mlisema alikua mradi, kwanza alikua amechoka hata kampeni zenyewe alikua akiongea machache anaachia, ila huyu dogo jameni kawatoa kamasi hadi mkalazimika kumpiga stop ban ya siku saba ili mumchelewesha, hakupumzika hayo masiku, alikua akienda Kariokoo "kununua" nyanya shughuli inasimama.

Sasa amerejea kwenye shughuli full, naona mipicha amesimamisha shughuli kote kote huko mikoani watu wanamsubiri kwa hamu kila mahali, halafu huyu alivyo na ujasiri, hamtomuweza kwa bao la mikono, atawazingua sana tena yaani dah! Mtu anapigwa risasi 30 na bado anausaka urais, huyu jamaa sijaona kama yeye Afrika, MaCCM mnalo, najua kila mmoja wenu raundi hii tumbojoto, mnajitia mzuka tu wa kuongea ongea ila kiundani mnahaha sana.

Yaani mpaka mumshinde awaachie lazima mtakua mumekipata cha moto. Nahisi baada ya hapo sidhani kama mtakua na yeyote wa kuwabaisha tena.
 
Back
Top Bottom