Kenya to build an International Airport at Taveta near KIA

Lowasa na wenzako leo ndio mnasikia kuhusu ujenzi huo?leo ndio mnamshtuka kuwa kia itakufa siyo?wakati Kamara aliposhauri juu kuangalia na kuboresha viwanja vyetu ukiwemo KIA ninyi hamkuwa kwenye system?au sasa hivi mnatafuta umaarufu ambao ulishatoweka?kenya airways wanafanya biashara kubwa sana nbi to mbs trip zisizopungua 6 kila siku na ndege zinajaa nauli zao nasikia siyo ghali sana.Hivi wakiomba njia ya nbi, kia, dar hadi mbs si mtawanyima?kwani mkiwapa tu shirika letu la ndege kirombo litakuwa mashakani.
 
tanzania tunafanya mambo kizamani sana na kuoneana wivu. wakenya wao wanaangalia biashara zaidi kuliko blabla. mzee shirima wa precion aliomba aendeshe air tz serikali kwa wivu ikakataa wanaona ni afadhali life kuliko kumpa mchagga. waache wakenye wafanye biashara sisi tubaki na blabla zetu
 
Kuwazuia Kenya wasijenge TAVETA international Airport - Holili ?????!!!!

Haluuu Viongozi wa Tanzania too late.

Kwanza anzeni kuboresha KIA kwanza. Wekeni vivutio ili ndege nyingi zitue. Tayari mmezidiwa kete na Jommo kenyatta airport na ndo maana wanajenga TAVETA airport.

hata kama mkiwazuia wasijenge TAVETA, bado biashara itabaki Jommo Kenyatta Airport Nairobi. Hivyo wanaweza kupanua Jomo kenyatta.

Kuwazuia wasijenge TAVETA bila kuboresha huduma za KIA ni sawa na Kutibu Malaria kwa Panadol.

Boresheni HUDUMA za KIA kwa njia zifuatazo.
-Kushusha landing tariffs
-Kushusha bei za mafuta ya ndege
-Kujenga double road/lanes KIA to Moshi/Arusha

-Kuboresha huduma za immigration
-kuboresha huduma za mizigo
 
Kwa CCM watakwambia pindi uchumi utakapo ruhusu vyote vita fanyika...sasa sijui lini............!!!!!!!!!!!
 
Kuwazuia Kenya wasijenge TAVETA international Airport - Holili ?????!!!!

Haluuu Viongozi wa Tanzania too late.

Kwanza anzeni kuboresha KIA kwanza. Wekeni vivutio ili ndege nyingi zitue. Tayari mmezidiwa kete na Jommo kenyatta airport na ndo maana wanajenga TAVETA airport.

hata kama mkiwazuia wasijenge TAVETA, bado biashara itabaki Jommo Kenyatta Airport Nairobi. Hivyo wanaweza kupanua Jomo kenyatta.

Kuwazuia wasijenge TAVETA bila kuboresha huduma za KIA ni sawa na Kutibu Malaria kwa Panadol.

Boresheni HUDUMA za KIA kwa njia zifuatazo.
-Kushusha landing tariffs
-Kushusha bei za mafuta ya ndege
-Kujenga double road/lanes KIA to Moshi/Arusha

-Kuboresha huduma za immigration
-kuboresha huduma za mizigo

wamelala ,,wanapenda siasa tuuu, bila kufanyia kazi mambo wanayo yasuggest, wanataka bade mambo yakiwa mabatya waje kusema kuwa walishasema ili tuwaone kuwa ni wema
 
Blaah blaah nyingi sana,tuwaache wakenya watufundishe.sie tuendeleze ufisadi.kwani hata fungu lingetolewa kwa ajili ya uwanja lingeliwa vile vile
 
Lowasa na wenzako leo ndio mnasikia kuhusu ujenzi huo?leo ndio mnamshtuka kuwa kia itakufa siyo?wakati Kamara aliposhauri juu kuangalia na kuboresha viwanja vyetu ukiwemo KIA ninyi hamkuwa kwenye system?au sasa hivi mnatafuta umaarufu ambao ulishatoweka?kenya airways wanafanya biashara kubwa sana nbi to mbs trip zisizopungua 6 kila siku na ndege zinajaa nauli zao nasikia siyo ghali sana.Hivi wakiomba njia ya nbi, kia, dar hadi mbs si mtawanyima?kwani mkiwapa tu shirika letu la ndege kirombo litakuwa mashakani.

Nashindwa kushangaa!
Tanzania tutaendelea kuwa wasindikizaji.Na bado!

Ugoigoi wa watendaji wetu kufikiri au watoa maamuzi wetu kutoa uamuzi sahihi na kwa wakati utatufikisha pabaya.
 
God bless us...!! Caz we're heading to stone age if this Government wl be in place for the next 5yrz...!!:embarassed2:
 
Wakuu Heshima mbele!

Hivi wakuu hamjui mnapoteza muda bure kuishauri hii serikali wakati ndiyo kwanza imo kwenye harakati za ushindi 2015!

Miezi minne tu baada ya uchaguzi mkuu, tayari vibwanga na mikiki mikiki ya kuwania ushindi 2015 imeanza, leo hii uwashauri kuhusu shughuli za maendeleo watakusikiliza kweli. Bure kabisa. Sijawahi kuona serikali ya kipuuzi kiasi hiki duniani. Yaani hata Somalia wasiokuwa na serikali angalau wanajua kile wanachokifanya.

Yaani badala ya kuwa na mawazo ya kuendeleza KIA ili iweze kuleta ushindani wa kweli, wao wanakaa na kujadili namna ya kuzuia maendeleo ya nchi nyingine. Hapa mnategemea nini wakuu?

Sababu ya kujengwa uwanja wa ndege wa KIA inajulikana. Lakini tangu uwanja ule ulivyotelekezwa na serikali hii, ni aibu tupu unapotumia uwanja huu. Wizi, miundominu mibovu, gharama zisizo na ulazima na mauchafu mengine yanayo fanana na hayo ni ujinga kusema eti TAVETA Airport isijengwe.

Wacha Kenya wajenge na waTanzania tutapitia huko kuliko maviwanja ya ndege ya Tz ambayo yamejaa ushenzi mtupu.
 
Tatizo la wakenya kujenga TAVETA Airport siyo challenge kwa serikali kuboresha uwanja wa ndege wa KIA tu. Wakenya wamefanya tathmini ya mambo mengi sana ambayo yatawaletea faida kubwa kutokana na biashara ya utalii hasa kwenye mlima wa Kilimanjaro. Wanataka waweze kupokea watalii wote watakaokuwa na nia ya kutembelea mlima Kilimanjaro, kwani wataweza kushukia hapo mpakani holili kwa urahisi na watatumia uwezo wao mkubwa walionao kutuzidi katika matangazo. Pia bila shaka watajenga Hotel za kimataifa zenye huduma bora kuliko za kwetu, hivyo wataweza kukaa na watalii mudawote na kuwaleta Tanzania kwaajili ya kupanda mlima na pindi wakishuka moja kwa moja wanaelekea kenya. Hii itatufanya tuambulie only park fee na kukosa mapato mengi kwenye mahoteli na biashara nyingine pia. Hivyo basi, serikali inabidi ifanye jitihada za kufanya maboresho makubwa katika uwanja wa ndege wa KIA kama ulivyopendekeza, tufanye jitihada kubwa zaidi za kujitangaza kiutalii ikiwemo mlima Kilimanjaro ambao wengi wakijua upo Kenya kutokana na wakenya kujitangaza sana, pia kufanyike kufanyike maboresho katika mahoteli yetu hasa katika huduma. Tusipokuwa makini tutashindwa kupata mapato na kubaki kulialia tu kwa uzembe wetu wa kutotaka kufikiria na kuona mbali.
 
tunatakiwa tuache kutumia hii mikataba katika kufanya biashara. biashara ni kuongeza tija katika mwenendo wetu wa kutoa huduma, hilo ndio suluhisho na sio kenya kutojenga Taveta.
Mfano sasa hiovi viwanda vyetu vya textile vimekufaa na pamba tunalima, je ikiwa kenya, au uganda au burundi, au rwanda wajenge viwanda vya nguo, jirani na nchi yetu, je huko mbeleni tukiwa na nia au uwezo wa kujenga kiwanda cha nguo tutazuiwa kwa kuwa kuna kiwanda kama hicho nchi jirani.
Mimi nafikiri tujiulize kwanini watu wanapanda ndege kuanzia nairobi nk au kwanini ndege nyingi hutua kenya kuliko kwetu. Tz tuna potentia nyingi sema ujinga wa viongozi ndio kikwazo, mfano mza tunaweza kuwa na uwanja mkubwaa na wa kimataifa kutoa huduma za ndege kwa Rwanda, Burundi, Uganda na Sehemu za Magharibi ya Kenya kama sirari, kisumu nk. tunaweza kuwa na flight za nchi za west africa tokea mza au french speaking countries tokea mza. watu wakatoka Burundi, rwanda Zaire kuja kupanda ndege Mza.
 
nchi hii inaongozwa kwa matukio ya kipuuzi.....hawana mpango wala mikakati

waache wakenya wafanye watakavyo....sisi hatuna mtu pale magogoni
 
Tatizo la wakenya kujenga TAVETA Airport siyo challenge kwa serikali kuboresha uwanja wa ndege wa KIA tu. Wakenya wamefanya tathmini ya mambo mengi sana ambayo yatawaletea faida kubwa kutokana na biashara ya utalii hasa kwenye mlima wa Kilimanjaro. Wanataka waweze kupokea watalii wote watakaokuwa na nia ya kutembelea mlima Kilimanjaro, kwani wataweza kushukia hapo mpakani holili kwa urahisi na watatumia uwezo wao mkubwa walionao kutuzidi katika matangazo. Pia bila shaka watajenga Hotel za kimataifa zenye huduma bora kuliko za kwetu, hivyo wataweza kukaa na watalii mudawote na kuwaleta Tanzania kwaajili ya kupanda mlima na pindi wakishuka moja kwa moja wanaelekea kenya. Hii itatufanya tuambulie only park fee na kukosa mapato mengi kwenye mahoteli na biashara nyingine pia. Hivyo basi, serikali inabidi ifanye jitihada za kufanya maboresho makubwa katika uwanja wa ndege wa KIA kama ulivyopendekeza, tufanye jitihada kubwa zaidi za kujitangaza kiutalii ikiwemo mlima Kilimanjaro ambao wengi wakijua upo Kenya kutokana na wakenya kujitangaza sana, pia kufanyike kufanyike maboresho katika mahoteli yetu hasa katika huduma. Tusipokuwa makini tutashindwa kupata mapato na kubaki kulialia tu kwa uzembe wetu wa kutotaka kufikiria na kuona mbali.
dah hapo umenigusa sana mtu wangu ukizingatia nilikua pande za kili hv majuz tu, am sure kenya watatupiga bao la kisigino coz kutoka kia mpaka marangu ambayo ndio njia rahis kwa wapandaji wa mlima ni mbali sana bt kutnka hapo taveta ni karibu mno so lazima kenya watajenga na acommodation nyingi tu so watalii watalala kenya na tz wataingia kupanda mlima tu afta that wanarudi kenya then bado hujataja tourism company za kenya zitakazotoa magari kwa watalii hao kuwaleta tz ikibidi mpaka ngorongoro,tarangire n.k yan ni faida juu ya faida ila tumlaumu nani kama sio hii serikali yetu ya kipumbavu inayopiga wanafunz virungu vyuon kwa kudai elfu kumi ya matunzo bila kujua kuwa huu mlima wetu tu ukitumika ipasavyo unaweza kusomesha wanafunz hao kwa kuwapa elfu 20 achilia mbali hiyo 10 wanayodai! Juzi kati hapa nimetembelea ngorongoro crater kidogo wanajitahid but cna hakika kama kweli hakuna ufisadi wa wa hayo mapato wanayopata hata hvyo bado ubunifu zaidi unahitajika ili kuweza kuvuna mapato stahili kwa neema hizi tulizojaliwa na muumba!
 
Imesemwa tunamakubaliano fulani katika jumuiya ya afrika mashariki kuhusu ujenzi wa infrastructure kama hizo, na kwamba kwa ujenzi wa uwanja wa ndege taveta ambapo ni karibu na kia wanakuwa wamekiuka makubaliano tajwa, kama hivyo ndivyo tuna haki ya kuwazuia. Pili kama lengo letu ni kuziunganisha nchi za eac katika ea federation haiingii akilini kwa nini kenya wajenge uwanja huo hapo wakati wa kia upo na kutokana na federation utakuwa wetu wote, inakuwa ni matumizi mabaya ya resources, inatakiwa watumie fedha hizo kufanyia kitu kingine.
 
Kuwazuia Kenya wasijenge TAVETA international Airport - Holili ?????!!!!

Haluuu Viongozi wa Tanzania too late.

Kwanza anzeni kuboresha KIA kwanza. Wekeni vivutio ili ndege nyingi zitue. Tayari mmezidiwa kete na Jommo kenyatta airport na ndo maana wanajenga TAVETA airport.

hata kama mkiwazuia wasijenge TAVETA, bado biashara itabaki Jommo Kenyatta Airport Nairobi. Hivyo wanaweza kupanua Jomo kenyatta.

Kuwazuia wasijenge TAVETA bila kuboresha huduma za KIA ni sawa na Kutibu Malaria kwa Panadol.

Boresheni HUDUMA za KIA kwa njia zifuatazo.
-Kushusha landing tariffs
-Kushusha bei za mafuta ya ndege
-Kujenga double road/lanes KIA to Moshi/Arusha

-Kuboresha huduma za immigration
-kuboresha huduma za mizigo

Hawa mpaka wapate kitu kidogo.
 
Hawa Wabunge wa Serikali yetu waliidhalilisha san KIA sasa watafanya nini? CCM ndio chanzo kung'ang'ania kuwa na Uwanja Mmoja tu wa Kimataifa kumiliki watanzania wanaondoka Nchini na Wanaoingia Nchini

Aibu kwa chama tawala
 
Back
Top Bottom