Kenya Seeks Diplomatic End To Ivory Sale Row With Tanzania

Mimi naona naanza kujenga chuki na serikali tena kwa kasi ya ajabu.

Tena inawezekna hata nchi jirani zinatumia pressure groups kuingiza mambo yaliyo na interest kwao katika sera zetu.Pia mimi naona hata kuna jambo ambalo hata usalama wa taifa unabidi uliangalie sana,hili suala la kujenga airport karibu na kwetu linaweza kuwa more than tourism strategy!
 
kwa kweli pia tunahitaji reform katika foreign policy yetu.Tuna mapungufu mengi,pia mawaziri wetu wa mambo ya nje nina mashaka nao sana na uwezo wao
 
kwa kweli pia tunahitaji reform katika foreign policy yetu.Tuna mapungufu mengi,pia mawaziri wetu wa mambo ya nje nina mashaka nao sana na uwezo wao

Una maana huyu wa sasa?? Wa sasa na aliyepita au wa sasa na wote waliopita??? Nafikiri kuna baadhi walikuwa na uwezo mzuri tu!!!
 
Una maana huyu wa sasa?? Wa sasa na aliyepita au wa sasa na wote waliopita??? Nafikiri kuna baadhi walikuwa na uwezo mzuri tu!!!

Wa sasa na aliyemtangulia.kama huyo aliyemtangulia nadhani alikua bomu zaidi na alidhani uwaziri wa mambo ya nje ni kusafiri tu.ukiangalia hata masuala ya radar,ndege ,kusaini EAC treaty bila kuangalia vipengele maalum vitakavyoyakwaza maslahi yetu nk.simaanishi Dr.Migiro.
 
i see kenya gets under the skin of most of you. TOUGHEN UP!!!!! whose fault that tanzania could not convience CITES that it was safe to sell the ivory stockpiles? it is tanzania's glaring incapability and weakness that is at fault. kenya successfully convienced CITES that it was unsafe to sell the ivory.

the fact is, kenya achieved the goals it set out to achieve at the CITES meeting while tanzania pathetically FAILED to achieve its goal. tanzania chose to stand against kenya on the issue of ivory and tanzania miserably LOST! deal with it and quit whining like little dogs. you win some you lose some that is the law of nature

and what is all this fuss about the aiport? first of all nobody is absolutely sure that the airport will get built. second, if kenya is building an airport on its land a few kilometers away from its border tanzania, what is preventing tanzania from building an aiport on its land just a stone throw away from it border with kenya?

kenya is not there to look after the intrests of tanzania, kenya will do what is good for kenya.
 
theres truth here bro,let us continue to our deadly sleep.
 
If one wants to learn about Kenya's hypocrisy then please read the article on the link below. It is well known that Kenya has relentlessly persuaded Tanzania to amend its constitution in order to allow foreigners to own land. Surprisingly, Kenya is now doing exactly the opposite of what it has been advocating for. They are now on the verge of passing a law that will bare foreigners from owning Ardhi in Kenya. This is the zenith of hypocrisy; why can’t these people practice what they have been preaching?

http://www.standardmedia.co.ke/Insi...=Moi says land clauses in draft law defective
 
deal with it and quit whining like little dogs. you win some you lose some that is the law of nature

kenya is not there to look after the intrests of tanzania, kenya will do what is good for kenya.

Nomasana,

Just Go on,spit your rhetoric hogwash here!

Nitakapo-hit back,mods msiniambie kitu coz sitasikiliza
 
Jamani naona hili jambo halijaisha, huenda ndio kwanza limeanza. Hebu angalia taarifa iliyotoka gazetini hivi karibuni;

Wabunge wakomalia Wakenya

Na Muhibu Said

18th April 2010

headline_bullet.jpg
Wasema kwamba ni majirani wabaya
headline_bullet.jpg
Wataka Mkataba wa Itifaki Soko la Pamoja Afrika Mashariki uvunjwe
headline_bullet.jpg
Hoja kuwasilishwa Bungeni kesho

Wabunge wamewajia juu Wakenya wakidai kwamba, ni majirani wabaya na kuitaka serikali kuvunja mkataba wa Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki, kutokana na kitendo cha watu hao kuiwekea Tanzania pingamizi la kuruhusiwa kuuza akiba ya pembe za ndovu.

Hatua hiyo ya wabunge, imechukuliwa ikiwa ni siku moja kabla ya hoja kuhusu itifaki hiyo, kuwasilishwa bungeni kesho na inahofiwa huenda isipitishwe na wabunge.
Pingamizi la kuuza pembe za ndovu, liliwekwa na Kenya katika mkutano wa maliasili uliofanyika Doha, nchini Qatar, kwa kuituhumu Tanzania kwamba, inachangia katika kuendeleza ujangili, baada ya nchi hiyo (Kenya) kukamata majangili katika mbuga zao, wakiwamo Watanzania.

Kenya imeweka pingamizi hilo, licha ya Tanzania kuendesha kampeni kuomba iruhusiwe kuuza akiba yake ya pembe za ndovu ili fedha zitakazopatikana zisaidie kusimamia na kuhifadhi maliasili, hasa ya wanyamapori dhidi ya ujangili.

Nchi nyingine, ambayo Kenya na Mali zimeziwekea pingamizi la kuuza pembe hizo sanjari na Tanzania, ni Zambia. Wabunge hao, ambao walionyesha dhahiri kuchefuliwa na kampeni hiyo ya Kenya, walionyesha hasira zao dhidi ya nchi hiyo katika semina kwa wabunge kuhusu itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki, iliyoandaliwa na Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, katika ukumbi wa Pius Msekwa, bungeni, mjini hapa jana.

Idadi kubwa ya wabunge waliochangia mada ya "Maudhui ya Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki" iliyowasilishwa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Deodorus Kamala katika semina hiyo, walikataa kuridhia mkataba hu ili wakisema kwamba, ili liwe fundisho kwa Kenya kuwa walichofanya Doha si ujirani mwema hivyo, haipaswi kushirikiana nao katika soko la pamoja.

Walisema Kenya katika mkutano wa Doha, walipaswa kuwa wamoja na Tanzania kwa kuwa wapo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na kama kuna jambo walikosewa, walipaswa kuficha ili wakazungumze baada ya mkutano kwa vile halikuwa na uhusiano na uuzaji wa pembe za ndovu. Wa kwanza kuonyesha hasira zake, ni Mbunge wa Masasi, Raynald Mrope (CCM), ambaye aliitaka serikali kutokubali kuridhia itifaki hiyo hata kama Rais Jakaya Kikwete alishatia saini mkataba huo.
Alisema anapendekeza suala hilo kwa vile Kenya haikuonyesha huruma kwani Tanzania imetumia gharama kubwa kutunza pembe hizo .

"Tusikubali itifaki hii kama walivyotufanyia kwenye pembe za ndovu katika mkutano wa Doha ili iwe adhabu wajue tumekasirishwa na jambo hili," alisema Mrope.
Mbunge wa Lulindi, Suleiman Kumchaya (CCM), alisema Kenya na Tanzania walipaswa kuwa wamoja katika mkutano huo na kama kulikuwa na jambo, walipaswa kuvumilia ili wazungumzie nyumbani kuliko walichofanya.

"Dalili hizi za kupingana katika mambo madogo ni ishara kuwa wenzetu si wamoja katika jumuyia, walitusaliti, walitudhalilisha, tukadharaulika, halafu leo mnatuambia turidhie itifaki ya Soko la Pamoja, hata kidogo waheshimiwa tusikubali. Kawaambie Doha imetia doa," alisisitiza Kumchaya.

Mbunge wa Kahama, James Lembeli (CCM), ambaye alikuwapo katika mkutano wa Doha kama sehemu ya ujumbe wa Tanzania, alisema kitendo cha Kenya kuikwamisha Tanzania isiuze pembe hizo, ni dalili kuwa hawapendi maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania, hivyo Bunge lisiridhie itifaki kwa kuwa si watu wazuri kuingia nao katika soko la pamoja.

Mbunge wa Shinyanga Mjini, Dk. Charles Mlingwa (CCM), alipendekeza Tanzania iwe ya mwisho kuridhia itifaki hiyo kwa kuwa haina faida kwa Tanzania zaidi ya kuwanufaisha Kenya yenye bidhaa nyingi katika masoko ya Afrika Mashariki. Alisema Kenya ina historia ndefu ya kuikwamisha Tanzania katika masuala ya uchumi akitoa mfano wa mwaka 2002 wakati Tanzania ilipoomba kibali cha kuongeza mgawo wa uwindaji wa chui, lakini Kenya ilipinga.

"Hatuna sababu ya kuharakia kuridhia itifaki hii kwa sababu za kisiasa bila kuzingatia maslahi ya kiuchumi, kwa walichofanya Doha, wabunge tukatae itifaki hii wajue tumekasirika," alisema Dk. Mlingwa. Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela (CCM), alisema kutokana na kitendo kilichofanywa na Kenya, hakuna haja ya kuridhia hata kama Rais ameshatia saini mkataba huo kwani wenzetu wameonyesha uadui wa wazi. Anne alienda mbali zaidi kwa kuitaka serikali ifanye sensa ya haraka katika hoteli zote za kitalii zinazomilikiwa au kuongozwa na Wakenya ili kubaini kama kuna Wakenya walioingia kinyemela na kupewa ajira, wafukuzwe haraka kwa vile ni wabaguzi katika masuala ya ajira na kupendekeza ajira zifungwe kwa wanajumuiya.
 
This is what we call prudent leadership, and thanks Waheshimiwa Wabunge for leading the course. Many people are infuriated with EAC, they don't want their country to be part and parcel of this gimmick. It is only a stupid Mbunge who will ignore the sentiments of his/her constituents. It is imperative for Wabunge to understand that they were elected to represent their constituents and not otherwise. There is nothing wrong with disagreeing with the president on volatiles issues of the likes of EAC, especially when nation’s interests are at stake. Once again thanks Waheshimiwa for having the audacity to call a spade a spade.
 
KITENDO cha Kenya kuongoza kampeni ya kupinga Tanzania isiuze meno ya tembo katika mkutano huko mjini Doha, Qatar kimewachefua wabunge wa Tanzania na wameionya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuwa makini na nchi hiyo na itambue kwamba Kenya si rafiki wa Tanzania.

Wakichangia mada ya “Maudhui ya Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki” iliyowasilishwa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Deodorus Kamala katika semina hiyo, wabunge hao walisema

Mbunge wa Masasi, Raynald Mrope (CCM),
alisema “Tusikubali itifaki hii kama walivyotufanyia kwenye pembe za ndovu katika mkutano wa Doha ili iwe adhabu wajue tumekasirishwa na jambo hili,”.

Mbunge wa Njombe Magharibi, Yono Kevela (CCM),
alisema wabunge wakatae kuridhia itifaki hiyo kwa maelezo: “Tuachane na soko hili kwa sababu wananchi wetu bado hawajapewa elimu ya kutosha kwa nini tuhangaike nalo. Hii ni kuwatengenezea ulaji watu wa Kenya, hivyo sisi wawakilishi wa wananchi tusiingie kichwakichwa katika kusaini itifaki hii.”

Mbunge wa Lulindi, Suleiman Kumchaya (CCM),
alisema “Dalili hizi za kupingana katika mambo madogo ni ishara kuwa wenzetu si wamoja katika jumuyia, walitusaliti, walitudhalilisha, tukadharaulika, halafu leo mnatuambia turidhie itifaki ya Soko la Pamoja, hata kidogo waheshimiwa tusikubali. Kawaambie Doha imetia doa,”.

Mbunge wa Kahama, James Lembeli (CCM),
ambaye alikuwapo katika mkutano wa Doha kama sehemu ya ujumbe wa Tanzania, alisema kitendo cha Kenya kuikwamisha Tanzania isiuze pembe hizo, ni dalili kuwa hawapendi maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania, hivyo Bunge lisiridhie itifaki kwa kuwa si watu wazuri kuingia nao katika soko la pamoja.Akaonya kuwa Bunge linaweza kuridhia leo; lakini vijana hao wakawalaani hadi wanakwenda kaburini.

Mbunge wa Shinyanga Mjini, Dk. Charles Mlingwa (CCM),
Alisema Kenya ina historia ndefu ya kuikwamisha Tanzania katika masuala ya uchumi akitoa mfano wa mwaka 2002 wakati Tanzania ilipoomba kibali cha kuongeza mgawo wa uwindaji wa chui, lakini Kenya ilipinga.

“Hatuna sababu ya kuharakia kuridhia itifaki hii kwa sababu za kisiasa bila kuzingatia maslahi ya kiuchumi, kwa walichofanya Doha, wabunge tukatae itifaki hii wajue tumekasirika,” alisema Dk. Mlingwa. Alisema kitendo cha Kenya kuamua kujenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Taveta karibu na mpaka wetu, lengo lao hasa ni kutaka kuua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), alipendekeza Tanzania iwe ya mwisho kuridhia itifaki ya soko la pamoja.

Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela (CCM),
alisema kutokana na kitendo kilichofanywa na Kenya, hakuna haja ya kuridhia hata kama Rais ameshatia saini mkataba huo kwani wenzetu wameonyesha uadui wa wazi. Anne alienda mbali zaidi kwa kuitaka serikali ifanye sensa ya haraka katika hoteli zote za kitalii zinazomilikiwa au kuongozwa na Wakenya ili kubaini kama kuna Wakenya walioingia kinyemela na kupewa ajira, wafukuzwe haraka kwa vile ni wabaguzi katika masuala ya ajira na kupendekeza ajira zifungwe kwa wanajumuiya.

Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai (CCM),
alisema kwa vile Tanzania imeshaingia kwenye itifaki hiyo, ni vigumu kutoka, hivyo akapendekeza kwamba, nguvu zote sasa zielekezwe kwenye sarafu moja akisema kwamba, itainua thamani ya fedha ya Tanzania.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema),
alisema wazo la kujitoa kwenye itifaki hiyo kwa sasa baada ya mkataba wake kusainiwa na Rais, ni sawa na treni inayotoka Kigoma, ambayo ikishaanza kuondoka stesheni ni vigumu kuisimamisha. Hata hivyo, alisema baada ya kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki, Tanzania ndiyo inayoongoza kwenye hatua ya Forodha na kutoa mfano wa mfanyabiashara, Said Bakhresa, ambaye anaongoza. Aliwataka wabunge kuunga mkono kwa vile itifaki hiyo itakuwa na manufaa kwa vijana watakaokuja baadaye kwani asilimia ya vijana wa Tanzania wako chini ya miaka 18 hivyo, wanastahili kuiboresha jumuiya na si kutoka.

Mbunge wa Bumbuli, William Shellukindo (CCM),
aliwataka wabunge kuchukua tahadhari katika kujadili suala hilo ili kuepuka kuzua mgongano baina yao na kusema kwamba, kama kuna makosa, ambayo Kenya imeyafanya yapelekwe kwenye jumuiya yakajadiliwe huko.

Mbunge wa Ulanga Magharibi, Dk. Juma Ngasongwa (CCM),
aliitaka serikali kuwa makini na waangalifu katika kufikia maamuzi, badala ya kuingia kichwa kichwa.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda
alikiri kuwa ni kweli Wakenya wamejaa hapa nchini na akahoji:

“Kwa nini Watanzania hawaendi huko kwao? Alihoji na kuwataka Wabunge wawe wazi ili Kenya wapate ujumbe huo kwamba Tanzania imekasirika. Lakini aliwaomba wabunge kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali katika kuliendea jambo hilo na kuwaomba waridhie kusainiwa kwa itifaki hiyo na kuongeza kuwa serikali itashughulikia mapendekezo waliyoyatoa.

Nini mawazo yako kuhusu “Maudhui ya Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki” yatakayowasilishwa kesho bungeni ingawa tayari Rais alisaini itifaki hiyo baada ya kupata baraka ya Baraza la Mawaziri.

Source: Magazeti ya Habari Leo na Nipashe
 
Wabunge waache propaganda, wao wafanye kweli tu ya kwamba wasiipitishe ili kama Rais mtu mmoja atatupeleka huko kwa nguvu basi tujuwe wazi ni nani aliyetupeleka huko.

Hii kitu ya doha, haijatokea kwa makosa ila Mungu bado anatuonya kwa viji sms kama vya doha. Hizo pembe hata wangeziuza zisingefanya kitu chochote ni sawa na kama ambavyo hawajaziuza. Lakini pale kulikuwa na message tukufu na sahihi kwa watanzania ya kwamba ni akina nani tunataka kuungana nao.
 
Hivi watanzania tunajipendekeza kwa kitu gani kwa wakenya? wana nini cha ziada cha kutupatia? Haya ni mauzauza ya milenia ya 3! Naona tumechoka na ustaarabu tulio nao; umekuwa monotonous. Sasa tunataka mabadiliko ya aina yoyote tu, alimradi ni hali mpya. Tutakumbuka tulikotoka, lakini tutakuwa tumechelewa. Ile mijamaa haina utu kabisa.
 
Mlikuwa hamuwajui wakenya siku zote? Sisi tuliopata bahati ya kufanya nao kazi tunawajua vizuri sana. Ni wao tu wapate na wanakutumia as long as interest zao haziharibiki.Vinginevyo ni kuwa nao makini sana na hii community ikianza bila kuwa na mpangilio tutaonja joto ya jiwe!
 
Wabunge waache propaganda, wao wafanye kweli tu ya kwamba wasiipitishe ili kama Rais mtu mmoja atatupeleka huko kwa nguvu basi tujuwe wazi ni nani aliyetupeleka huko.

Hii kitu ya doha, haijatokea kwa makosa ila Mungu bado anatuonya kwa viji sms kama vya doha. Hizo pembe hata wangeziuza zisingefanya kitu chochote ni sawa na kama ambavyo hawajaziuza. Lakini pale kulikuwa na messege tukufu na sahihi kwa watanzania ya kwamba ni akina nani tunataka kuungana nao.
MkamaP nakubaliana na wewe wabunge wakipinga ni wananchi wamepinga kama Rais pekee akikubali na nasikia ameshasaini basi tutajua nani katulazimisha na historia itamuumbua, yale yale ya EAC iliyokufa 1977 na Muungano wetu na Zanzibar yanajirudia zilianzishwa na viongozi wakuu Nyerere, Kenyata na Idd Amini kwa EAC na Nyerere na Karume kwa upande wa Muungano bila kuwashirikisha wananchi sijui kwa nini viongozi wetu wanakuwa wazito kujifunza.
 
Viongozi wetu ni wakati mwingine kweli inabidi ukubali tu ni watu wa aajabu.

mtu kama JK anaishindwa nini kutambua ya kwamba ka mgogoro ka zanzibar kammeshinda akabwaga manyanga, na tena ukiangalia wazanzibar ni watu asilimia kubwa tunashea nao damu sisi watu wa bara na tena wazanzibar ni watu wazuri poa kabisa. nabado tunayumba, leo hii pamoja na ujambazi wa hapa na pale kuna uwezekano mkubwa kule zanzibar ukisahau ka begi kako kuna msamalia mwema atakusutua aisii muungwana umesahahu kibegi chako hapa.

Kama tunakuwa na utata na wazanzibar hakika hawa manyang'au sijui atawaweza vipi? Tatizo la JK hawezi toa sura ya mbuzi na kusema hiki hapana ,anabaki kuburuzwa tu na akina Raila.

Wabunge waache propaganda waikatae hiyo kitu, ili mtu mmoja atuingize huko twende kila mmoja akijuwa kabisa ni nani aliyetupeleka huko.Watu wanafikiri wako bado ktk enzi za Nyerere .

Na uhakika fulani watanzania asilimia 99% hawataki hiyo kitu, sasa mtu unashindwa kuelewa anaenda kusaini madude gani. Uchumi wetu hao wanaojifanya kusaini hayo majidudu waache kufisadi fedha na mda na badala yake wa focus ktk kuindeleza nchi kwa kubuni mambo muafaka na sio hizo pumba wanazoongelea.
 
Zitto hajui anachoongea, simply kwa sababu Rais amesaini bado hiyo sio sheria mpaka itakapopitishwa na Bunge.

Huyu jamaa anachotaka ni bunge wa EAC , ndio maana napigia debe jambo la kijinga. Watoto miaka kumi na nane watabenefit nini wakati tuna msingi mbovu wa elimu, ni kitu gani kilichofanywa kuwawezesha hawa watoto kubenefit kutoka kwenye hii jumuia.

Zitto ni mtu aliyejaa nadharia, na anayeangalia vitu kwa mtazamo mdogo. Kabla ya kufikiria jumuia, tuangalie ni jinsi gani waluo na wakikuyu wanaweza kuungana .
 
Wakuu naafiki kabisa.

Aaachiwe hii kazi Mkuu mwenyewe ili historia ije kumsuta. Wabunge wafanye kweli. Tena tutawatafuta hata wabunge walioipigia kura kuipitisha. Wawe radhi kama kweli ni majasiri na wanjua walifanyalo ni sahihi basi wajitolee watoe ukweli nani ameunga nani amekanusha, kama Senate ya Marekani inavyofanya.

Mh. Zitto anaongea kusema itakuwa na manufaa kwa vijana wa umri wa miaka 18, anashindwa kuona kuwa anawaandalia hao vijana utumwa mbaya sana. Hakuna future katika jumuiya hiyo tutambue kabisa. Kama alivyozungumza Ndahani, msiowajua jitahidini muwafahamu kwanza. Kama hujawahi kufanya nao kazi usijifanye unawajua hao. Fanya nao kazi ujue walivyo wabaya, ni nyoka, hiyo kitu waliyofanya huko Doha ndiyo style yao tena imenikumbusha mambo mengi sana ya kiofisi yanaofanana sana.

Hakuna kitu hapo, wanatungoja tuingize shingo wenyewe kwenye hicho kitanzi. Mwacheni JK asaini mwenyewe hiyo kitu!
 
Zitto hajui anachoongea, simply kwa sababu Rais amesaini bado hiyo sio sheria mpaka itakapopitishwa na Bunge.

Huyu jamaa anachotaka ni bunge wa EAC , ndio maana napigia debe jambo la kijinga. Watoto miaka kumi na nane watabenefit nini wakati tuna msingi mbovu wa elimu, ni kitu gani kilichofanywa kuwawezesha hawa watoto kubenefit kutoka kwenye hii jumuia.

Zitto ni mtu aliyejaa nadharia, na anayeangalia vitu kwa mtazamo mdogo. Kabla ya kufikiria jumuia, tuangalie ni jinsi gani waluo na wakikuyu wanaweza kuungana .

Tatizo kweli unashindwa kuelewa ni nini haswa.

Ukiangalia hata european union hawa jamaa kabla ya kuungana kila nchi ilikuwa imejidhatiti vilivyo kwa sheria na wanazitekeleza. mfano kufanya kazi humo mtu kutoka nchi hizo hizo kwenda nyingine lazima apate working permit.

Pili mwananchi wa nchi husika analipwa karibu mara 5 zaidi ya mgeni kwa kazi ileile, kitu ambayo inapelekea wananchi sasa wanarudi ktk nchi nchi zao maana wanaona huko wanakokimbilia wanafanywa watumwa na pessa hailipi tena.

sasa hawa wa kwetu sizani hata kama wameweka sheria fulani yakumbana, na hata kama wameweka sheria zetu hazitekeleziki na ndio maana tunasema hiyo EAF pembeni kwanza, mpaka tutakapoiweka nchi yetu sawa na kupatikana watu wwa kutekeleza sheria na kusimamia misingi ya haki na imala ndipo nafikiri tutakapopata agalau ka wazo ka hiyo EAF.

Kusaini kwa sasa hilo dubwana EAF ,kweli unashindwa kuelewa uwezo kabisa wa viongozi.Nao viongozi lazima watambuwe ya kwamba wapo pale kuwakirisha mawazo ya wananchi na si kuwakirisha mawazo yao.
 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikiri kuwa ni kweli Wakenya wamejaa hapa nchini na akahoji “Kwa nini Watanzania hawaendi huko kwao?

Alihoji na kuwataka Wabunge wawe wazi ili Kenya wapate ujumbe huo kwamba Tanzania imekasirika. Lakini
aliwaomba wabunge kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali katika kuliendea jambo hilo na kuwaomba waridhie kusainiwa kwa itifaki hiyo na kuongeza kuwa serikali itashughulikia mapendekezo waliyoyatoa.

Huyu Waziri Mkuu wetu haishi kunishangaza na kauli zake?
 
Back
Top Bottom