MY TAKE:Kuna wale Malazy waliopinga safari ya rais Samia Suluhu kuja Kenya. Walisema kwamba rais Samia hapaswi kuja Kenya na alistahili kuendeleza roho mbaya na mikwaruzano aliyoanzisha mwendazake ambaye sitamtaja hapa. Lakini cha kushangaza ni kwamba baada ya rais Suluhu kutembea Kenya, sasa Kenya inanunua mahindi mara sita (×6) zaidi ya jinsi tulivyokuwa tukifanya hapo awali.
Kukupa tu mfano wa haraka, Mwezi wa April Kenya iliagiza gunia 16,137 za mahindi kutoka Tanzania. Baada ya rais Samia kutembea Kenya basi mwezi wa Mei Kenya iliagiza gunia 118,329 za mahindi kutoka Tanzania. Ongezeko hilo la kishindo la mwezi wa Mei ni karibu mara kumi ya agizo la mwezi wa April. Sasa wewe mwenyewe hebu fikiria ni vipi Kenya inaweza kuongeza agizo lake la mahindi kutoka Tanzania kwa zaidi ya mara sita au saba ndani ya kipindi cha mwezi moja. Bila shaka vita vya Magufuli viliumiza wakulima wenu na kuwanyima pesa nyingi sana. Bila shaka wanaofaidika sasa ni wakulima wa mahindi wa Tanzania. Hapa Kenya tunakula ugali sana na nchi yetu sehemu kubwa ni jangwa. Ujirani mwema baina yetu utawafaidi nyinyi majirani kwa sana maana nyinyi mnazalisha chakula na sisi tunanunua. Tujengane sio kutukanana na kufungiana mipaka kama alivyopenda kufanya mwendazake ambaye alikuwa na isolationist mindset, yaani alipenda kujifungia na kukataa kushiriki na majirani wenzake.
Wanaotaka kusoma taarifa kwa kiingereza, hii hapa chini.
Zezetas word kununuwa can also be viewed as i.e donation, wadanganyika is a donor or should be a donor country.