Kenya sasa ina kila sababu za kukamilisha kipande cha SGR kilichosalia maana Uganda wameamua kujenga SGR 2,700km

Siyo kweli, Muzungu alijenga reli ya Mombasa-Uganda kwa sababu ilikuwa ni nchi moja, hivyo ilikuwa ni kama tu kuunganisha Mikoa ya British East Afrika na Bandari ya Mombasa, lkn hakujenga Reli ya Mombasa ili kuhudumia nchi nyingine kwani Uganda na Kenya zilikuwa nchi moja iliyoitwa British East Afrika, hata huku kwetu Mjerumani hakujenga Reli ili kuhudumia nchi nyingine bali alijenga reli strategic kuhudumia nchi yake ambayo leo hii ni yetu.

Kwa kukusaidia zaidi unajua kwamba Mkoloni Muingereza alijenga reli kutoka Bandari ya Mtwara mpaka Nachingwea reli ambayo tulikuja kuing'oa baada ya Uhuru ? unajua ni kwa nini hiyo reli ilijengwa ? Ni kwa sababu Nachingwea Muingereza alilima Karanga kulikua na mradi mkubwa wa kilimo cha karanga ambapo lengo lake lilikuwa ni kuzalisha mafuta ya kula for export na ndio maana reli ikajengwa kuanzia Nachingwea mpaka bandari ya Mtwara ~270 km ili iweze kusafirisha hizo exports, reli ambayo kwa sababu ambazo sizijui tuliing'oa baada ya Uhuru, ...
Uganda na Kenya hazijawahi kuwa nchi moja, ila zilitawaliwa na mkiloni mmoja yaani muingereza, kutawaliwa na muingereza haina maana ni nchi moja, kwanini husemi Malawi na Zambia ni nchi moja kwasababu zote zilitawaliwa na muingereza?, kwanini Muingereza hakujenga reli toka Zambia hadi Malawi badala yake alijenga Zambia pekee na kuunganisha na Angola ambalo halikua koloni lake?, lengo ni kuunganisha nchi zenye mzigo mkubwa.

Mjerumani alijenga reli ya kati hadi Kigoma, ambayo iliungana na upande wa pili wa ziwa Tanganyaka katika mji wa Kalemii, mizigo toka Zaire ilifika Kalemii na kuvushwa ziwa Tanganyika hadi Kigoma na kuingizwa katika train.

Hizo reli ndogondogo unazozisema hazikujengwa na serikali ya Uingereza bali zilijengwa na wafanyabiashara/Wakulima/Wachimbaji binafsi kwa ajili ya kuhudumia mashamba au Migodi yao, mara tu biashara zao zinapotetereka, hizo reli pia hutetereka, kama ilivyokua reli za mashamba ya katani, machimbo ya almasi kule Mwadui na viwanda mbalimbali ambavyo viliunganishwa kwa njia ya reli.
 
Back
Top Bottom